Baada ya WB na Denmark kusitisha misaada na uhusiano wanaofuata ni Scandinavia, EU, UK, Canada na Marekani

Yaani unalilia msaada kama mtoto mdogo. Kwa hiyo uko tayari kutatuliwa marinda alimradi tu upewe msaada? Aisee.
Sijui unajaribu kuzuis ukweli usiongelewe? Pole sana. Budget ya Tz, yategemea zaidi ya 50% misaada/mikopo toka kwa wadau wa maendeleo toka nje.
Kujifanya eti hujali sio ajabu, LAKINI hiyo, haitofuta adha tutakayokuja pata watz, kutokana na kiburi cha makusudi kilichokithiri cha watawala wetu hata baada ya kushauriwa kiungwana kuhusu kuheshimu haki za binadamu na kuachana kuwakandamiza watz wenzao na kuheshimu katiba nasheria za nchi. Zimbabwe ya Mugabe ni mfano hai. Amen.
 
Hatuna namna aliyetangulia katangulia, 40% wanayotoa wazungu ndiyo pesa yenye uhakika, 60% ya pesa za ndani hata 30% yake tunashindwa kutimiza.
 
Kipindi cha Kikwete mlikua hamtaki tuwe ombaomba au mmesahau na je upo tayari mkuu kupewa msaada kwa masharti ya kuwa shoga tuje tukutolee barua?
Muulize Dr. Mpango kama serikali iko tayari kupewa msaada wa masharti, kama haiko tayari tusisikie kwenye bajeti anasema nusu yake tunategemea wahisani vinginevyo muache usanii.
 
Muulize Dr. Mpango kama serikali iko tayari kupewa msaada wa masharti, kama hayuko tayari tusisikie kwenye bajeti anasema nusu yake tunategemea wahisani.
Mpango akikubali vipi naruhusiwa kuja kutoa posa kwa mzee wako?
 
Hiyo haijalishi sisi hatuogopi chochote maana sisi ni matajiri sana ndiyo maana tunanunua ndege kwa keeshii na tunanunua korosho kwa keshiii
 
Hatuna namna aliyetangulia katangulia, 40% wanayotoa wazungu ndiyo pesa yenye uhakika, 60% ya pesa za ndani hata 30% yake tunashindwa kutimiza.
Tunashindwa kutimiza kwa sababu hatujajipanga kujiletea maendeleo wenyewe bila kuwategemea wahisani. Hata wao wanalijua hilo, tatizo letu kubwa ni ile kasumba waliyoturithisha wenyewe kwamba wao ni watu bora wenye akili baada ya mungu. Jiamini mtu wangu... kwa kasi hii ya JPM utasikia mengi, Kelele kama hizi zilikuwepo sana tu hata enzi za Nyerere.
 
Dr mihogo hajambo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…