Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Wakuu heshima kwenu. Poleni na majukumu.
Ndugu yenu numerudi tena kuwajuza yale yanayoendelea kunisibu, maana najua hapa wamejaa watu wenye upeo wa kushauri, kutia moyo ,kuonya, kukufungua jicho upate alert na wengine weeengi sana.

Wiki kadhaa zimepita toka nilete mikasa yangu na mazonge ya wife.

Soma: Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu

Pia nikaleta huu: Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Sasa ni hivi, kwakifupi ni kwamba, baada ya wife kuamua kuondoka nyumbani, nikamtafuta mara kadhaa simu zikawa hazipokelewi, basi na mimi nikaamua kupiga kimyaa tu.
Si kupiga simu wala kutuma message.

Katika mazingira hayo, ya kutowasiliana, yeye akiwa kwao huko mitaa ya Boko, mimi nikaanza kupokea "samansi" kupitia ngazi za serikali.

Nikapelekwa dawati la jinsia polisi
Nikapelekwa baraza la kata
Nikaitwa kikao cha familia

(Koote huko, ni yeye, na msimamo wangu ulikua, kutafuta suluhu maisha yaendelee ila mwenzangu akagoma na kusisitiza dai la Talaka)

Nikaitwa tena polisi na kutiwa lockup
NIkatolewa kwa dhamana.
Niliporudi home nikakuta kahamisha karibia 50% ya kila kitu mle ndani, ikiwemo vitu vyake na vya watoto wetu wanne vyooote.

Nikafuatilia na kugundua kule baraza la kata ameshachukua form no.3 kwaajili ya kufungua shauri la talaka mahakamaani

Kipindi hiki chooote ni yeye anacheza offensive game ya kuniburuza namna hiyo anavyotaka, mimi nimetulia kwenye mode ya Deffensive game. Sitaki kushindana na mama watoto, hasa ukizingatia aliondoka na watoto.

Nikaona isiwe kesi, huyu mama kweli kadhamiria kuni destroy.

Ikumbukwe kuwa muda wote huo , niko busy na shughuli zangu za kibiashara na kusafiri mikoani, hivyo nalazimika kusitisha kazi na kuja kuitika wito mpaka nawekwa ndani, na kipindi hiki chote niliamua kuacha nyumba na kuhamishia makazi mwanza. Home pakawa pamebaki hapana mtu.

Baada ya muda nikapata wito wa mahakama, wife kafungua kesi ya kutadai talaka.

MImi nimetulia zangu tu wala sishindani naye.
Kila anachofanya, mimi napambana nacho, nachomoka, simtumii text, wala kumpigia kusema labda kumlaumu,au kumtishia au kumuomba msamaha aachane na hizi ishu, au kusalimia watoto, nimekaa kimyaa tuuu.

Mawazo nikaona yananizidia, nisije changanyikiwa, nikarudi nyumbani nyanda za juu kusini kwa baba na mama. Hii kwa kiasi kikubwa ikanisaidia.

ONA SASA,

Sasa week hii karibia na kesi, nikasafiri kurud Dar, kwakua nilikua na majukumu ya kikazi, nikaona isiwe tabu, nikatafuta taarifa za pale nyumbani panaendeleaje ? Nikamtafuta mtu wa jirani, akafika home akakuta pamevunjwa geti na nilimpomsihi anisaidie kuingia ndani na kukagua, akakuta 95% katika vitu vilivyobakishwa na wife alipotoroka nikiwa lockup, pia vimeibiwa.

Basi nilipomalizA majukumu yangu, nikaona nipite pale home, kisha nikaenda ku report polisi juu ya tukio, maana nikawaza, wife kafungua kesi ya talaka na moja ya madai yake ni mgawanyo wa mali kwa maana ya nyumba, sasa japo sikua na hamu tena na chochote juu ya mali, nikataka nipotezee tu hata nisifike home ila nikaona hii isije niletea shida kwenye kesi ya mgawanyo wa mali ikaonekana mimi kwa namna moja au nyingine nime temper na mali ambazo kesi ya wife inataka zigawanywe baada ya talaka.

Nikaona acha nipeleke taarifa niwe katika safe side.

Baada ya kumaliza ku report nikarudi tena nyumbani, na kushuhudia hali halisi, baada ya hapo, nikamuita kijana mmoja jirani yangu, nikamwambia achukue kila kitu kilichobaki mle ndani ambavyo wezi waliviacha.
Vitu vile vikubwa kubwa kama makabat na furniture ,na baadhi ya vyombo. Nikamwambia avichukue tu, nimempa, maana hawa wezi wanaweza wakarud tena wakaiba, hivyo bora jirani unufaike wewe ninayekujua. By the way sina mpango tena wa kurud kufanya maisha hapa.

Tukaachana nikaondoka kurudi hotel niilipofikia kusubiri siku ya kesi mahakamani maana imekaribia.

Sasa kitu cha kushangaza ni kwamba, yale niliyokua najiuliza na ku assume kichwani, ndiyo hayo hayo alikua akiyafikiri yule askari aliyenichukua maelezo. Maana yeye siku natiwa lockup na wife, yeye alikuwepo mpaka siku natoka, so mgogoro wetu anaujua.

Akaniuliza katika maelezo "je, katika tukio hili, unamtuhumu nani?".

Nikajibu "simtuhumu mtu wala sijui ni nani aliyetenda"

Akafunga maelezo na kufungua jalada kisha kunipa RB yangu.
Ila "off record" akaniambia " laiti kama mimi ningekua mpelelezi wa kesi hii, ningemtia hatiani mke wako kama mtuhumiwa namba 1"

Nikasema "hapana mimi sifahamu".
Japo kiukweli, ninasukumwa kuamini hili.

Ninaamini kabisa, wife amefikia hatua mbaya sana ya chuki juu yqngu na anajaribu kuni provoke indirectly na kuni push nichukue hatua ngumu, baada ya kuona kila chokochoko zake, mimi naamua kuzipuuzia, na kuingia gharama ya kukubali maumivu anayonisababishia.

Ikumbukwe chanzo cha mgogoro mzima ni mimi kufumania picha zake za uchi akiwa katika safari ya kikazi nikamhoji, akani temea shit, nikamchapa. Ila ndio hivyo anakomaa kuvunja ndoa.

Wakuu, na hayo tu.
NIwatakie mchana mwema
Tulikuuliza sababu ya kumchapa makofi ukaficha kumbe ni picha za uchi! Duu pole huyo wala siwezi mtetea.
 
Hili nalo neno😃, kabla hajatoa talaka aombe DNA 💯 Fanton Mahal pindua meza baba ukienda kwenye shauri la talaka omba DNA ya watoto
Hii maana yake nani atakua responsible kwenye hilo zoezi kuthibitsha watoto ni wangu?? Maana uliposema niombe DNA maana yake ni yeye atatakiwa kuthibitisha au ni mimi?
 
Mkuu hiyo kesi ishamaliza wewe nenda nae hivyohivyo wacha mamlaka iamue yalimkuta rafiki yangu haya Miaka zaidi ya 3 ni vituko tu mwisho mwanamke akaenda ngazi hizohizo. Mwisho wakaachana na kugawana mali.

So kwenye wito wowote ww nenda na lolote litakalo amuliwa na mamlaka kama kugawana mali just do it than fanya maisha yako. Huyo ashalishwa sumu na kuna mtu anamjaza usengerema. Ile hii karma itamrudia usiwe na shaka na watoto wape huduma zozote na utapata ufumbuzi.
Pamoja chief. Ahsante
 
Mkuu kwanza hongera kwa ukimya na huu ukimya ndio unaomtesa,kikubwa mpe kila kitu hamna haja ya 50:50 kwa ajili ya watoto alafu jikatae usiwahi hata kumuona.
N.B:hawa viumbe hawapumzikagi had waone umeingia kaburini.
 
Hii maana yake nani atakua responsible kwenye hilo zoezi kuthibitsha watoto ni wangu?? Maana uliposema niombe DNA maana yake ni yeye atatakiwa kuthibitisha au ni mimi?
mahakamani utaambiwa uende ustawi wa jamii kuchukua kibali na utaratibu jinsi ya kupima na gharama zake ni laki moja kupima,ila muhimu kujiongeza kwa wale maafisa wa ustawi ili jambo liende kiuwepesi afu kama mkeo alikuchezea rafu lazima alete upinzani kwenye hilo jambo na lazima atajaribu kuhonga, embu mpe na yeye heka heka kidogo na ikiwezekana kabla ya mahakamani watafute maafisa wa ustawi wa jamii uongee nao kabisa then ukifika mahakamani katika kujieleza sema ya kwako na usikubaliane na talaka moja kwa moja we kazia kwanza kwenye DNA ili mnapoachana uwe na uhakika unahudumia damu yako kiroho safi. Natamani kungekuwa na voice note nikuhadithie kisa cha jamaa yangu jinsi alivyolea mtoto si wake na huyo mwanamke walikutana chuo mwaka wa pili sijui ndo kuzaa kumbe alibambikiwa mimba sasa kaja kupata safari ya marekani yani kuhamia huko pale ubalozi lazima watoto wapimwe DNA kujiridhisha ni watoto wake huwezi amini huyo mwanamke alikataa kabisa mwanae kupimwa DNA , ikabidi jamaa atumie mbinu mbadala dah majibu yanatoka sio mtoto wake.
 
USHAURI WA BURE KWENU NYOTE MLIOPO HAPA
Haijalishi kama mko kwenye ndoa au ni mahusiano ya kawaida, mpenzi wako akitamka kwamba HAKUTAKI, usilazimishe na usipoteze muda, kwa upole, kubali matokeo, mpe anachotaka na endelea na maisha yako. Kutamka maneno kama SIKUTAKI, NAOMBA UNIACHE, NIPE TALAKA YANGU, USINITAFUTE, USINIPIGIE SIMU, FUTA NAMBA YANGU, n,k yanatoka moyoni mwake na ana sababu zake kutamka maneno hayo, hivyo ukilazimisha kutaka kuwa naye, ataendelea 'kukukataa kwa matendo' yake na si maneno tena, na hayo matendo yatakutesa sana, kwa akili yake yeye ni kwamba, 'mimi nilishasema kwamba sikutaki' na likiharibika jambo tafsiri yake ni 'uliyataka mwenyewe'.

Ukishakaa mbali naye, jipe muda wa kukaa peke yako bila mahusiano mapya, jikite katika kujijenga wewe binafsi na maisha yako kwanza, usikimbilie kuanza mahusiano mengine, kuwa mwenyewe kwa muda jifanyie tathimini ya maisha yako, jiulize unachotaka maishani mwako na katika mahusiano badala ya kukurupuka na kukimbilia mahusiano mapya.
 
Back
Top Bottom