Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Hongera kwa hatua uliyopiga, kwenye maisha epuka kupambana na mwanamke kwa namna yoyote ile, sheria zimewapendelea sana wao. Nikushauri rudi dawatini ukakabidhi hiyo nyumba kimaandishi kwamba ni mke na watoto. Baada ya hapo kaendelee na maisha mengine, Mungu hata kuacha na utafanikiwa zaidi ya hivyo ulivyoacha leo. Muhimu tengeneza amani ya moyo wako,mtumaini na kumuomba Mungu siku zote za maisha yako,fanya kazi bidii na maarifa, inshalaah utafanikiwa. All the best chief.
Unampotosha mwenzio,yaani amuachie nyumba huyo shetani,bora wagawane
 
Hii chukua kama funzo uweze kujifunza zaidi mbeleni kuhusu wanawake...
Na ukipata taraka kata mawasiliano nae kabisa na ufunge moyo usiwasiliane nae mwaka mzima.
Hakikisha kwenye kugawana vitu usimuachie vitu vyako binafsi
Huyo mwanamke hakukupenda toka mwanzo na alikubali kuolewa na wewe kwa sababu na sasa hivi hiyo sababu kashaipatia ufumbuzi na wewe huna faida Tena kwake......
NB; vijana mnapo amua kuona hakikisha unaemua anahitaji kuolewa na sio mtu anahitaji kuolewa kwa sababu siku hiyo sababu yake ikipata ufumbuzi hatahitaji Tena hiyo ndoa.!!!!! Na ataivunja kwa gharama yoyote ile na kumbuka mwanamke akiwa na lake hashauriki.
Nimekuelewa vizur dada angu
 
Mkuu hiyo kesi ishamaliza wewe nenda nae hivyohivyo wacha mamlaka iamue yalimkuta rafiki yangu haya Miaka zaidi ya 3 ni vituko tu mwisho mwanamke akaenda ngazi hizohizo. Mwisho wakaachana na kugawana mali.

So kwenye wito wowote ww nenda na lolote litakalo amuliwa na mamlaka kama kugawana mali just do it than fanya maisha yako. Huyo ashalishwa sumu na kuna mtu anamjaza usengerema. Ile hii karma itamrudia usiwe na shaka na watoto wape huduma zozote na utapata ufumbuzi.
 
Umeniona mkuu. Niseme watoto ndio wamekua udhaifu wangu mkubwa sana, ila kwasasa nimeamua nikaze moyo tu
Mpe talaka yake gawaneni hicho anachotaka!watoto watauliza TU baba yupo wapi na wewe utakua unaenda kuwaona Kila mara!!
Kuoa wasomi wenye ajira kujitafutia pressure tu mkuu!Ninae wa aina hiyo tena wa huko huko!UBINAFSI UNAZIDI KWAO KADRI MASHAKA NA CHANGAMOTO ZAO ZINAPOISHA HASA UNAPOZIMALIZA KAMA MWANAMME NDIO WANAANZA UBINAFSI NA VITUKO KIBAO!!UKIWAACHIA KILA KITU TENA HAWANA UWEZO WA KUENDESHA KABISA NA WANAANZA KUTUMIA WATOTO KUPIGA SIM ,NA HAWATAKI KUKIRI KWAMBA WALIKOSEA WANAKUTAFUTIA VIJSABABU VINGINE ILI URUDI KWENYE UTATUZI WA CHANGAMOTO WANAZOPITIA!!

WAJINGA MNO!
 
Nakupa ushauri wa kiume:-
  • Usitake talaka kwa sasa, mpaka ufanikishe hatua inayofuata chini.​
  • Uza mali zako zote kwa sasa, kabla mambo hayajapamba moto; kisha ukajenge kwingine kimya kimya.​
  • Ukifanikisha hilo, mpatie talaka.​
  • Kuna wazungu wengi wanatafuta wanaume wa kuwaweka ndani; nashauri uwatafute, kwa sababu ulimwengu ni kiganjani kwa sasa. Hii itakupunguzia msongo wa mawazo kama mkeo atakuwa anatoka na mtu mwenye uchumi mkubwa kuliko wewe.​
  • Baada ya hapo, piga pigo za 'cowboy' na ufurahie maisha.​
 
Sisi wenye 'D' 2 tumetizama Kwa jicho la kungulu jamaa ana kitu kinaitwa dependency disorder 😤 😤 ni kitu kibaya zaidi kweny maisha tafuta upande wako
Unatushangaza sis vijana wadogo huna sifa za kuwa mwanaume Bora huna msimamo wa kiume ndyo maana anakupelekesha na ataendelea kukupelekeaha by emotional kuwa baba mkamilifu

Amua Kuanza upya jifunze furah Yako isimtegemee mtu mwingne siku akikuumiza utaumia mara 4 ya maumivu ya kawaida.ila pole sanaaa
 
Wakuu heshima kwenu. Poleni na majukumu.
Ndugu yenu numerudi tena kuwajuza yale yanayoendelea kunisibu, maana najua hapa wamejaa watu wenye upeo wa kushauri, kutia moyo ,kuonya, kukufungua jicho upate alert na wengine weeengi sana.

Wiki kadhaa zimepita toka nilete mikasa yangu na mazonge ya wife.

Soma: Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu

Pia nikaleta huu: Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?

Sasa ni hivi, kwakifupi ni kwamba, baada ya wife kuamua kuondoka nyumbani, nikamtafuta mara kadhaa simu zikawa hazipokelewi, basi na mimi nikaamua kupiga kimyaa tu.
Si kupiga simu wala kutuma message.

Katika mazingira hayo, ya kutowasiliana, yeye akiwa kwao huko mitaa ya Boko, mimi nikaanza kupokea "samansi" kupitia ngazi za serikali.

Nikapelekwa dawati la jinsia polisi
Nikapelekwa baraza la kata
Nikaitwa kikao cha familia

(Koote huko, ni yeye, na msimamo wangu ulikua, kutafuta suluhu maisha yaendelee ila mwenzangu akagoma na kusisitiza dai la Talaka)

Nikaitwa tena polisi na kutiwa lockup
NIkatolewa kwa dhamana.
Niliporudi home nikakuta kahamisha karibia 50% ya kila kitu mle ndani, ikiwemo vitu vyake na vya watoto wetu wanne vyooote.

Nikafuatilia na kugundua kule baraza la kata ameshachukua form no.3 kwaajili ya kufungua shauri la talaka mahakamaani

Kipindi hiki chooote ni yeye anacheza offensive game ya kuniburuza namna hiyo anavyotaka, mimi nimetulia kwenye mode ya Deffensive game. Sitaki kushindana na mama watoto, hasa ukizingatia aliondoka na watoto.

Nikaona isiwe kesi, huyu mama kweli kadhamiria kuni destroy.

Ikumbukwe kuwa muda wote huo , niko busy na shughuli zangu za kibiashara na kusafiri mikoani, hivyo nalazimika kusitisha kazi na kuja kuitika wito mpaka nawekwa ndani, na kipindi hiki chote niliamua kuacha nyumba na kuhamishia makazi mwanza. Home pakawa pamebaki hapana mtu.

Baada ya muda nikapata wito wa mahakama, wife kafungua kesi ya kutadai talaka.

MImi nimetulia zangu tu wala sishindani naye.
Kila anachofanya, mimi napambana nacho, nachomoka, simtumii text, wala kumpigia kusema labda kumlaumu,au kumtishia au kumuomba msamaha aachane na hizi ishu, au kusalimia watoto, nimekaa kimyaa tuuu.

Mawazo nikaona yananizidia, nisije changanyikiwa, nikarudi nyumbani nyanda za juu kusini kwa baba na mama. Hii kwa kiasi kikubwa ikanisaidia.

ONA SASA,

Sasa week hii karibia na kesi, nikasafiri kurud Dar, kwakua nilikua na majukumu ya kikazi, nikaona isiwe tabu, nikatafuta taarifa za pale nyumbani panaendeleaje ? Nikamtafuta mtu wa jirani, akafika home akakuta pamevunjwa geti na nilimpomsihi anisaidie kuingia ndani na kukagua, akakuta 95% katika vitu vilivyobakishwa na wife alipotoroka nikiwa lockup, pia vimeibiwa.

Basi nilipomalizA majukumu yangu, nikaona nipite pale home, kisha nikaenda ku report polisi juu ya tukio, maana nikawaza, wife kafungua kesi ya talaka na moja ya madai yake ni mgawanyo wa mali kwa maana ya nyumba, sasa japo sikua na hamu tena na chochote juu ya mali, nikataka nipotezee tu hata nisifike home ila nikaona hii isije niletea shida kwenye kesi ya mgawanyo wa mali ikaonekana mimi kwa namna moja au nyingine nime temper na mali ambazo kesi ya wife inataka zigawanywe baada ya talaka.

Nikaona acha nipeleke taarifa niwe katika safe side.

Baada ya kumaliza ku report nikarudi tena nyumbani, na kushuhudia hali halisi, baada ya hapo, nikamuita kijana mmoja jirani yangu, nikamwambia achukue kila kitu kilichobaki mle ndani ambavyo wezi waliviacha.
Vitu vile vikubwa kubwa kama makabat na furniture ,na baadhi ya vyombo. Nikamwambia avichukue tu, nimempa, maana hawa wezi wanaweza wakarud tena wakaiba, hivyo bora jirani unufaike wewe ninayekujua. By the way sina mpango tena wa kurud kufanya maisha hapa.

Tukaachana nikaondoka kurudi hotel niilipofikia kusubiri siku ya kesi mahakamani maana imekaribia.

Sasa kitu cha kushangaza ni kwamba, yale niliyokua najiuliza na ku assume kichwani, ndiyo hayo hayo alikua akiyafikiri yule askari aliyenichukua maelezo. Maana yeye siku natiwa lockup na wife, yeye alikuwepo mpaka siku natoka, so mgogoro wetu anaujua.

Akaniuliza katika maelezo "je, katika tukio hili, unamtuhumu nani?".

Nikajibu "simtuhumu mtu wala sijui ni nani aliyetenda"

Akafunga maelezo na kufungua jalada kisha kunipa RB yangu.
Ila "off record" akaniambia " laiti kama mimi ningekua mpelelezi wa kesi hii, ningemtia hatiani mke wako kama mtuhumiwa namba 1"

Nikasema "hapana mimi sifahamu".
Japo kiukweli, ninasukumwa kuamini hili.

Ninaamini kabisa, wife amefikia hatua mbaya sana ya chuki juu yqngu na anajaribu kuni provoke indirectly na kuni push nichukue hatua ngumu, baada ya kuona kila chokochoko zake, mimi naamua kuzipuuzia, na kuingia gharama ya kukubali maumivu anayonisababishia.

Ikumbukwe chanzo cha mgogoro mzima ni mimi kufumania picha zake za uchi akiwa katika safari ya kikazi nikamhoji, akani temea shit, nikamchapa. Ila ndio hivyo anakomaa kuvunja ndoa.

Wakuu, na hayo tu.
NIwatakie mchana mwema
Pole sana braza MUNGU anakupa jaribu unaloliweza ila unapokuwa na mke wa ndoa kuwa na Moja kichwani kwa kila jambo...
 
Tuendelee kukataa ndoa
 

Attachments

  • SGN_02_10_2025_1739195992029.png
    SGN_02_10_2025_1739195992029.png
    355.4 KB · Views: 3
  • SGN_02_10_2025_1739195321930.png
    SGN_02_10_2025_1739195321930.png
    1.9 MB · Views: 4
Back
Top Bottom