MrsPablo1
JF-Expert Member
- Jun 9, 2013
- 1,073
- 1,941
hapo ni kwa mkemia tuu, hosp za kawaida wife ataenda kuhonga, nina story za hivi vitu ila kuhadithia ndo shughuliHospital inayoaminika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hapo ni kwa mkemia tuu, hosp za kawaida wife ataenda kuhonga, nina story za hivi vitu ila kuhadithia ndo shughuliHospital inayoaminika.
Usijali ndugu yangu wakati mwingine unalazimika kuachana na mtu si kwa sababu wewe haumpendi ila ni kwa sababu yeye analazimisha. Hatua hii ni ngumu sana, lakini nakuhakikishia hiyo hali unayojisikia itapita, jipe muda tu.Ni kwel kuhusu kumpenda, sio uongo, haikua rahisi kukubali hii hali upesi
Ahsante chief. Nashkuru kwa ushauri wakokwa mlipofikia, hudhuria Mahakamani..maana hata usipohudhuria shauri litaendelea kusikilizwa upande mmoja na kama ni Talaka itatolewa, ukiwepo utakuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu sawa, na pia uhusike kwenye mgawanyo wa Mali, na mjadala kuhusu watoto wako.
Usipingane na ombi lake la Talaka Mahakamani, ameshaku-push sana, ni muda wa kumpa Haki yake,
Chapili...ni kuhusu watoto, Mahakama yaweza kumpa uangalizi (custody) ya watoto, lakini una Haki ya kuwaona na kufahamu kinachoendelea (access),
au Mahakama yaweza kwenye suala la watoto, kuwapa Rufaa muende Ofisi za Ustawi wa Jamii mkajadiliane mustakabali wa watoto wenu,
Option zote mbili, Hatakuwa na Haki ya kukunyima au kuzuia wewe kuwasiliana na kujenga mahusiano na watoto wako,
ikiwa unahusika kutunza watoto una Haki 100% ya kuwaona/kujua maendeleo ya watoto wako, ikiwa atabaki na uangalizi wa watoto, ni vyema vipindi vya likizo, kwa wale ambao ni wakubwa, ukawachukua ukakaa nao kwa muda huo wa likizo ili waendelee kujenga mahusiano nawewe, hii ni Haki yako sio ombi.
Yakikamilika haya, tuliza kichwa kwa muda, pata huduma za kiroho kwa mujibu wa Imani yako, usikimbilie kutafuta mbadala ili kuonesha kuwa ume move-on, tulia, Relaaax (Darasa), kila kitu kitakuja kwa wakati sahihi, then endelea kupush kete zako za 2025.
Nimekuelewa kaka, ahsanteUsijali ndugu yangu wakati mwingine unalazimika kuachana na mtu si kwa sababu wewe haumpendi ila ni kwa sababu yeye analazimisha. Hatua hii ni ngumu sana, lakini nakuhakikishia hiyo hali unayojisikia itapita, jipe muda tu.
Sasa kitakachofuatia ni kwamba wakati wewe umesha move on na labda ushapata mtu mwingine yeye wakati huo ndio atarudi. Kwa sababu unatupa updates hapa endelea kuwa na subira huyo akishakuona na mtu mwingine na unafuraha ataanza kujirudisha
achana na DNA ndugu yangu, hao watoto ni wako wewe walee, kama hamkuwa na maugomvi huko nyuma achana nayo, hii kitu labda kama umemfuma na mwanaume mwingine lakini kama hujamfuma we acha tu, utawatesa hata hao watoto kisaikolojia kitu ambacho sio kizuri.Hii maana yake nani atakua responsible kwenye hilo zoezi kuthibitsha watoto ni wangu?? Maana uliposema niombe DNA maana yake ni yeye atatakiwa kuthibitisha au ni mimi?
Itakuwa amechanganyikana na wa Mbozi huyo! Pole sana,limalize uendelee na maisha yakoWa huko huko kwetu chief
Mkuu Na Mimi Naomba Nimtake Radhi Pia Kwa Kumwambia Huyo Ni Msengenyaji.Naomba unisamehe kwa kukutukana wewe ni Fala.
Hio itakuwa ndoa ya dini isiokua ya kiislamu. Uislamu umeweka wazi talaka. Unangangania nini wewe kidume? Acha hizo, toa talaka katafute mke mwengine. Nakushauri silimu uone mke ndoa ya kiislam utaonjoyWakuu heshima kwenu. Poleni na majukumu.
Ndugu yenu numerudi tena kuwajuza yale yanayoendelea kunisibu, maana najua hapa wamejaa watu wenye upeo wa kushauri, kutia moyo ,kuonya, kukufungua jicho upate alert na wengine weeengi sana.
Wiki kadhaa zimepita toka nilete mikasa yangu na mazonge ya wife.
Soma: Mshkaji wangu anataka kumroga mama watoto wangu
Pia nikaleta huu: Nini madhara ya Kutoonekana mahakamani katika kesi ya Ndoa?
Sasa ni hivi, kwakifupi ni kwamba, baada ya wife kuamua kuondoka nyumbani, nikamtafuta mara kadhaa simu zikawa hazipokelewi, basi na mimi nikaamua kupiga kimyaa tu.
Si kupiga simu wala kutuma message.
Katika mazingira hayo, ya kutowasiliana, yeye akiwa kwao huko mitaa ya Boko, mimi nikaanza kupokea "samansi" kupitia ngazi za serikali.
Nikapelekwa dawati la jinsia polisi
Nikapelekwa baraza la kata
Nikaitwa kikao cha familia
(Koote huko, ni yeye, na msimamo wangu ulikua, kutafuta suluhu maisha yaendelee ila mwenzangu akagoma na kusisitiza dai la Talaka)
Nikaitwa tena polisi na kutiwa lockup
NIkatolewa kwa dhamana.
Niliporudi home nikakuta kahamisha karibia 50% ya kila kitu mle ndani, ikiwemo vitu vyake na vya watoto wetu wanne vyooote.
Nikafuatilia na kugundua kule baraza la kata ameshachukua form no.3 kwaajili ya kufungua shauri la talaka mahakamaani
Kipindi hiki chooote ni yeye anacheza offensive game ya kuniburuza namna hiyo anavyotaka, mimi nimetulia kwenye mode ya Deffensive game. Sitaki kushindana na mama watoto, hasa ukizingatia aliondoka na watoto.
Nikaona isiwe kesi, huyu mama kweli kadhamiria kuni destroy.
Ikumbukwe kuwa muda wote huo , niko busy na shughuli zangu za kibiashara na kusafiri mikoani, hivyo nalazimika kusitisha kazi na kuja kuitika wito mpaka nawekwa ndani, na kipindi hiki chote niliamua kuacha nyumba na kuhamishia makazi mwanza. Home pakawa pamebaki hapana mtu.
Baada ya muda nikapata wito wa mahakama, wife kafungua kesi ya kutadai talaka.
MImi nimetulia zangu tu wala sishindani naye.
Kila anachofanya, mimi napambana nacho, nachomoka, simtumii text, wala kumpigia kusema labda kumlaumu,au kumtishia au kumuomba msamaha aachane na hizi ishu, au kusalimia watoto, nimekaa kimyaa tuuu.
Mawazo nikaona yananizidia, nisije changanyikiwa, nikarudi nyumbani nyanda za juu kusini kwa baba na mama. Hii kwa kiasi kikubwa ikanisaidia.
ONA SASA,
Sasa week hii karibia na kesi, nikasafiri kurud Dar, kwakua nilikua na majukumu ya kikazi, nikaona isiwe tabu, nikatafuta taarifa za pale nyumbani panaendeleaje ? Nikamtafuta mtu wa jirani, akafika home akakuta pamevunjwa geti na nilimpomsihi anisaidie kuingia ndani na kukagua, akakuta 95% katika vitu vilivyobakishwa na wife alipotoroka nikiwa lockup, pia vimeibiwa.
Basi nilipomalizA majukumu yangu, nikaona nipite pale home, kisha nikaenda ku report polisi juu ya tukio, maana nikawaza, wife kafungua kesi ya talaka na moja ya madai yake ni mgawanyo wa mali kwa maana ya nyumba, sasa japo sikua na hamu tena na chochote juu ya mali, nikataka nipotezee tu hata nisifike home ila nikaona hii isije niletea shida kwenye kesi ya mgawanyo wa mali ikaonekana mimi kwa namna moja au nyingine nime temper na mali ambazo kesi ya wife inataka zigawanywe baada ya talaka.
Nikaona acha nipeleke taarifa niwe katika safe side.
Baada ya kumaliza ku report nikarudi tena nyumbani, na kushuhudia hali halisi, baada ya hapo, nikamuita kijana mmoja jirani yangu, nikamwambia achukue kila kitu kilichobaki mle ndani ambavyo wezi waliviacha.
Vitu vile vikubwa kubwa kama makabat na furniture ,na baadhi ya vyombo. Nikamwambia avichukue tu, nimempa, maana hawa wezi wanaweza wakarud tena wakaiba, hivyo bora jirani unufaike wewe ninayekujua. By the way sina mpango tena wa kurud kufanya maisha hapa.
Tukaachana nikaondoka kurudi hotel niilipofikia kusubiri siku ya kesi mahakamani maana imekaribia.
Sasa kitu cha kushangaza ni kwamba, yale niliyokua najiuliza na ku assume kichwani, ndiyo hayo hayo alikua akiyafikiri yule askari aliyenichukua maelezo. Maana yeye siku natiwa lockup na wife, yeye alikuwepo mpaka siku natoka, so mgogoro wetu anaujua.
Akaniuliza katika maelezo "je, katika tukio hili, unamtuhumu nani?".
Nikajibu "simtuhumu mtu wala sijui ni nani aliyetenda"
Akafunga maelezo na kufungua jalada kisha kunipa RB yangu.
Ila "off record" akaniambia " laiti kama mimi ningekua mpelelezi wa kesi hii, ningemtia hatiani mke wako kama mtuhumiwa namba 1"
Nikasema "hapana mimi sifahamu".
Japo kiukweli, ninasukumwa kuamini hili.
Ninaamini kabisa, wife amefikia hatua mbaya sana ya chuki juu yqngu na anajaribu kuni provoke indirectly na kuni push nichukue hatua ngumu, baada ya kuona kila chokochoko zake, mimi naamua kuzipuuzia, na kuingia gharama ya kukubali maumivu anayonisababishia.
Ikumbukwe chanzo cha mgogoro mzima ni mimi kufumania picha zake za uchi akiwa katika safari ya kikazi nikamhoji, akani temea shit, nikamchapa. Ila ndio hivyo anakomaa kuvunja ndoa.
Wakuu, na hayo tu.
NIwatakie mchana mwema
Leta hata visa viwili tu MrsPablo1 tujifunzehapo ni kwa mkemia tuu, hosp za kawaida wife ataenda kuhonga, nina story za hivi vitu ila kuhadithia ndo shughuli
Ni kwel, ni ndoa ya kikristoHio itakuwa ndoa ya dini isiokua ya kiislamu. Uislamu umeweka wazi talaka. Unangangania nini wewe kidume? Acha hizo, toa talaka katafute mke mwengine. Nakushauri silimu uone mke ndoa ya kiislam utaonjoy
Ni kwel kabisa mkuu. Hili usemalo ni kwel, sheria na taratibu za ku deal na haya mambo kwa kiasi kikibwa zinatubana sana sisi wanaumeMkuu pole sana..wapo wanaopitia magumu katika ndoa zao kuliko wewe..Muhimu mwachie vyote anza maisha upya.
Wanawake huwa wanabadirika sana na si watu wa kuwamini hata kidogo hadi huwa najiuliza ndio huyu niliyekuwa natoka jasho kwa ajili yake au ni Mwingine?
Changamoto pia sheria zetu za ndoa zinampa nguvu sana Mwanamke katika maamuzi kuliko Mwanume na ukienda kwenye madawati ya jinsia yanamsikiliza zaidi mwanamke nakuona mwanaume ndio mwenye makosa.
Ubora wa Talaka Katika UislamuNi kwel, ni ndoa ya kikristo
Daahh..hapa kwakwel ni too much, mtu anakubadilishia kabisaa mfumo wa maisha completellyPole mkuu kisa chako kina ukaribu wa kufanana na kisa changu , japo mimi niliacha kila kitu mpaka na kazi nikakimbia moja kwa moja bila kugeuka nyuma .
Ulivyompiga uliharibu sana maana unafahamu vyombo vya habari na Wana harakati wanasema Kila siku kuchapa/ kupigwa mwanamke ni kosa na udhalilishaji. Pia kwa hayo aliyokufanyia na ukimya wako katu hawezi kuthubutu kuishi na wewe Tena maana haamini atakuwa salama au una mkakati gani dhidi ya uhai wake. Mtu anapokufanyia maovu hata ukija mpa chakula na ana njaa ya kufa hawezi Kila kwani anadhani utalipiza kisasi kumbe huenda ushasahau kitambo.Nilikua na attend kote aliko niita kwanza kwasababu nilikua naletewa wito wa kiserikali kwa nyaraka, sasa nikawa naona yaweza kuwa kosa kukaidi.
Pili nilikua naenda kwakua nilikua nataman tusifikie hatua ya kuvunja ndoa maana nilikua najiaminisha yamkini ni hasira tu ,tunaweza tukamaliza kwa kuongea wakiwepo na third parties. Kumbe waapi!!.
Ni kweli.Ulivyompiga uliharibu sana maana unafahamu vyombo vya habari na Wana harakati wanasema Kila siku kuchapa/ kupigwa mwanamke ni kosa na udhalilishaji. Pia kwa hayo aliyokufanyia na ukimya wako katu hawezi kuthubutu kuishi na wewe Tena maana haamini atakuwa salama au una mkakati gani dhidi ya uhai wake. Mtu anapokufanyia maovu hata ukija mpa chakula na ana njaa ya kufa hawezi Kila kwani anadhani utalipiza kisasi kumbe huenda ushasahau kitambo.