Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

Kwanza pole kwa madhila,binafsi nimegundua kwamba wanaume walio serious na kusaka maisha ni rahisi sana kuteswa na wake zao.Wanawake walio katika ndoa za mitala ama mwanaume mchepukaji ni watulivu kwa waume zao.Ushauri kwa mleta mada ni kuwa ajitahidi upate mwanamke haraka ili iwe fimbo ya kumchapa nayo kwani sidhani kama kuna mwanaume wa kumuoa akiwa na watoto wanne kwa maisha yalivyo kiurahisi bali mume wake ndiyo alitumika kama daraja kwa wanaume walaghai. .Akibaki singo atasumbuliwa lkn akiwa na mwanamke hata kama hajamrasmisha ni fimbo kwa yule mpumbavu.
 
Mimi Intelligent businessman ni raisi wa chama cha ma jobless pro max, makamu ni Bolotoba,
katibu ni min -me, wakili wa ma jobless ni Selikavu, waziri wa mambo ya ndani Thecoder, msajili wa chama Cha ma jobless ni dosho12, mratibu wa mipango ni Edo kissy

Msemaji wa chama Cha ma jobless pro max ni makutupora

Kidumu chama Cha ma jobless pro max View attachment 3231981
Ningekuwa mimi ndio mmiliki wa mtandao,watu ambao mpo serious kama nyie,nawapa lebo kabisa katika id zenu

Nimeona katiba yenu mpo makini sana
 
Wakati wa kuwana hakikisha watoto wawili unabaki nao ww acha ubwege Tena pambana kiume watoto wawili wabaki kwako ukishindwa hilo Hauna tofauti na lokole
Ni vyema watoto wakalelewa na mmoja tu ili kuepusha mpasuko wa watoto wenyewe kwa wenyewe huko mbeleni. Hii inaweza ikaja kuwa vita mbaya zaidi.
 
Pole sana Mkuu
Nadhani mahusiano yenu yapo hatua mbaya
Nakupongeza zaidi unavo handle situation
Nashauri kama talaka mpe tu
Tuendelee na maisha mengine, japo kama ametembea na watoto kwenye mgao wa nyumba unaweza pata 10%
Umeandika kama huna kichwa. Apate 10% kwa sababu zipi? Kisa watoto. Hao watoto wameshirikiana na wazazi wao kuijenga hio nyumba? Kama hujui kitu ni bora kukaa kimya kuliko kubwabwaja ushuzi kama huu.
 
Mleta mada fata hiki alichoandika jamaa. Labda na mimi niongezee kidogo.

1. Endelea kukaa kimya hivyo hivyo, kwa kesi yako uliyosimulia, mwanamke amekukosea sana na kwa kuwa ameshahamisha moyo wake kwenda kwa mwanaume mwingine, amekuwa kiburi zaidi.

2. Mali zinatafutwa, yamkini kwa sasa unaona inaweza ikakuchukua muda kupata zingingine ila amini kwamba huyo mwanamke akiondoka kwako, milango yako mingi itafunguka zaidi. Usije ukathubutu kumuachia mali zote, nenda nae mahakamani, gawaneni hizo mali kisha wekeza kwa sehemu kwa ajili ya wanao, anza tena maisha mengine mapya, usiingie haraka haraka kuanzisha mahusiano ya kifamilia na mwanamke mwingine. Umeshaumwa na nyoka tayari, so maumivu unayajua deeply. Womean are all the same japo najua ktk hili utakataa. Sikiliza mzee, popote penye anguko la mwanaume spiritually au physically basi behind yupo mwanamke. Kumbuka anguko la Adamu pale Eden, mfalme Ahabu, Samson akaangushwa na mwanamke. Angalia matajiri wakubwa duniani akina Elon Musk, Bill Gates, Putin n.k wote hawa wametalakiana na wake zao na hawataki kuoa tena, sasa jiulize wewe una akili kuliko hawa wanaozungukwa na jopo la wanasaikolojia, watu wa rohoni n.k? Mtume Petro alisisita kukaa na mwanamke kwa akili sana sababu alijua mlango wa shetani kuingiza maangamizi kwa mwanaume ni mwanamke.

3. Huyo mwanamke utafika wakati atajirudi tu kwako, kwa sasa una maumivu makali sana. Na unatamani hata aje akuombe msamaha ili mrudiane muendelee kulea familia. Kati ya makosa makubwa ambayo utakuja kuyafanya ni kuja kumsamehe huyo mwanamke kwa sasa wala kwa baadae.

Endelea kujikaza kwa kutomjibu wala kumtafuta.
Nimekuelewa sana chief
 
Kwa jinsi nilivyomfuatilia tangu uzi wake wa mwanzo ni kuwa baada ya mvurugano mkewe ametaka taraka moja kwa moja isipokuwa yeye ndio anataka usuluhishi.....mkewe anafanya visa ili apewe taraka Yale.....kwa njia ya khiyari imeshindikana kwa ndio kaamua kwenda mahakamani.......

Jamaa anaonekana bado anampenda mkewe na ndio maana anapata tabu na anapata ugumu wa kutoa talaka
Ni kwel kuhusu kumpenda, sio uongo, haikua rahisi kukubali hii hali upesi
 
Umeandika kama huna kichwa. Apate 10% kwa sababu zipi? Kisa watoto. Hao watoto wameshirikiana na wazazi wao kuijenga hio nyumba? Kama hujui kitu ni bora kukaa kimya kuliko kubwabwaja ushuzi kama huu.
Nimekudharau sana
 
Nilikua na attend kote aliko niita kwanza kwasababu nilikua naletewa wito wa kiserikali kwa nyaraka, sasa nikawa naona yaweza kuwa kosa kukaidi.
Pili nilikua naenda kwakua nilikua nataman tusifikie hatua ya kuvunja ndoa maana nilikua najiaminisha yamkini ni hasira tu ,tunaweza tukamaliza kwa kuongea wakiwepo na third parties. Kumbe waapi!!.
Yani ulifuma picha za uchi za mkeo akiwa safari kikazi afu hizo picha hakutuma kwako afu kakupeleka dawati eti na wewe unataka yaishe 😂 , inaonekana huyo mwanamke alikuwa anakuendesha kama gari bovu lakini nikupongeze tuu kwa kuwa mtulivu kwenye drama zake umetumia akili kutokunasa kwenye mitego yake. lakini ina uhakika baada ya talaka atakujaga kukumbeleza umsamehe mrudiane mlee watoto na wewe utakubali 😂
 
Back
Top Bottom