Baada ya Wife kuniweka Lockup naona kama natengenezewa mazingira ya ku react nichukue hatua kali

kwa mlipofikia, hudhuria Mahakamani..maana hata usipohudhuria shauri litaendelea kusikilizwa upande mmoja na kama ni Talaka itatolewa, ukiwepo utakuwa na uwezo wa kuweka kumbukumbu sawa, na pia uhusike kwenye mgawanyo wa Mali, na mjadala kuhusu watoto wako.
Usipingane na ombi lake la Talaka Mahakamani, ameshaku-push sana, ni muda wa kumpa Haki yake,
Chapili...ni kuhusu watoto, Mahakama yaweza kumpa uangalizi (custody) ya watoto, lakini una Haki ya kuwaona na kufahamu kinachoendelea (access),
au Mahakama yaweza kwenye suala la watoto, kuwapa Rufaa muende Ofisi za Ustawi wa Jamii mkajadiliane mustakabali wa watoto wenu,
Option zote mbili, Hatakuwa na Haki ya kukunyima au kuzuia wewe kuwasiliana na kujenga mahusiano na watoto wako,
ikiwa unahusika kutunza watoto una Haki 100% ya kuwaona/kujua maendeleo ya watoto wako, ikiwa atabaki na uangalizi wa watoto, ni vyema vipindi vya likizo, kwa wale ambao ni wakubwa, ukawachukua ukakaa nao kwa muda huo wa likizo ili waendelee kujenga mahusiano nawewe, hii ni Haki yako sio ombi.
Yakikamilika haya, tuliza kichwa kwa muda, pata huduma za kiroho kwa mujibu wa Imani yako, usikimbilie kutafuta mbadala ili kuonesha kuwa ume move-on, tulia, Relaaax (Darasa), kila kitu kitakuja kwa wakati sahihi, then endelea kupush kete zako za 2025.
 
Ni kwel kuhusu kumpenda, sio uongo, haikua rahisi kukubali hii hali upesi
Usijali ndugu yangu wakati mwingine unalazimika kuachana na mtu si kwa sababu wewe haumpendi ila ni kwa sababu yeye analazimisha. Hatua hii ni ngumu sana, lakini nakuhakikishia hiyo hali unayojisikia itapita, jipe muda tu.

Sasa kitakachofuatia ni kwamba wakati wewe umesha move on na labda ushapata mtu mwingine yeye wakati huo ndio atarudi. Kwa sababu unatupa updates hapa endelea kuwa na subira huyo akishakuona na mtu mwingine na unafuraha ataanza kujirudisha
 
Ahsante chief. Nashkuru kwa ushauri wako
 
Nimekuelewa kaka, ahsante
 
Hii maana yake nani atakua responsible kwenye hilo zoezi kuthibitsha watoto ni wangu?? Maana uliposema niombe DNA maana yake ni yeye atatakiwa kuthibitisha au ni mimi?
achana na DNA ndugu yangu, hao watoto ni wako wewe walee, kama hamkuwa na maugomvi huko nyuma achana nayo, hii kitu labda kama umemfuma na mwanaume mwingine lakini kama hujamfuma we acha tu, utawatesa hata hao watoto kisaikolojia kitu ambacho sio kizuri.

Mpaka hapo watoto wameshaathirika sana na kama kuna waliokuwa wakubwa bora waende boarding school tu angalau itawaepushia machungu zaidi
 
Hio itakuwa ndoa ya dini isiokua ya kiislamu. Uislamu umeweka wazi talaka. Unangangania nini wewe kidume? Acha hizo, toa talaka katafute mke mwengine. Nakushauri silimu uone mke ndoa ya kiislam utaonjoy
 
Mkuu pole sana..wapo wanaopitia magumu katika ndoa zao kuliko wewe..Muhimu mwachie vyote anza maisha upya.
Wanawake huwa wanabadirika sana na si watu wa kuwamini hata kidogo hadi huwa najiuliza ndio huyu niliyekuwa natoka jasho kwa ajili yake au ni Mwingine?
Changamoto pia sheria zetu za ndoa zinampa nguvu sana Mwanamke katika maamuzi kuliko Mwanume na ukienda kwenye madawati ya jinsia yanamsikiliza zaidi mwanamke nakuona mwanaume ndio mwenye makosa.
 
Ni kwel kabisa mkuu. Hili usemalo ni kwel, sheria na taratibu za ku deal na haya mambo kwa kiasi kikibwa zinatubana sana sisi wanaume
 
Ni kwel, ni ndoa ya kikristo
Ubora wa Talaka Katika Uislamu

Ingawa talaka haipendekezwi, kuna nyakati inapokuwa bora kwa sababu zifuatazo:

i. Epuka Madhara na Dhuluma

Ikiwa ndoa imejaa manyanyaso, uonevu, au ukatili, talaka inakuwa suluhisho la kuokoa maisha ya mke au mume.


ii. Kulinda Dini na Maadili

Ikiwa ndoa inapelekea maasi, kama vile uzinzi, kutengana kiimani, au uhasama wa kudumu, basi talaka inahitajika ili kulinda dini ya wanandoa.


iii. Kurejesha Amani na Utulivu

Wakati ndoa imekuwa chanzo cha mateso badala ya furaha, talaka inawapa nafasi wanandoa kuanza upya kwa amani.


iv. Kuwezesha Ndoa Mpya Bora

Ikiwa ndoa ya awali haifanyi kazi, talaka inatoa fursa kwa mume na mke kupata wenza wanaowafaa zaidi kwa maisha yao ya baadaye.
KARIBU NA KATIKA UISLAMU. MTAFUTE SHEIKH WA KARIBU USILIMU
 
Pole mkuu kisa chako kina ukaribu wa kufanana na kisa changu , japo mimi niliacha kila kitu mpaka na kazi nikakimbia moja kwa moja bila kugeuka nyuma .
Daahh..hapa kwakwel ni too much, mtu anakubadilishia kabisaa mfumo wa maisha completelly
 
Ulivyompiga uliharibu sana maana unafahamu vyombo vya habari na Wana harakati wanasema Kila siku kuchapa/ kupigwa mwanamke ni kosa na udhalilishaji. Pia kwa hayo aliyokufanyia na ukimya wako katu hawezi kuthubutu kuishi na wewe Tena maana haamini atakuwa salama au una mkakati gani dhidi ya uhai wake. Mtu anapokufanyia maovu hata ukija mpa chakula na ana njaa ya kufa hawezi Kila kwani anadhani utalipiza kisasi kumbe huenda ushasahau kitambo.
 
Ni kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…