Abiria wanaotumia Treni ya SGR kutoka Dar es salaam - Morogoro hadi Dodoma wametuhumiwa kuhujumu shirika la reli Tanzania TRC kwa kutolipa nauli ambazo zianendana na sehemu wanazoelekea au vituo wanavyoshukia.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro Christopher Mwakajinga amesema abiria wamekuwa wakikata tiketi za vituo vya njiani na pindi treni inapofika katika vituo hivyo wamekuwa hawashuki na kuendelea na safari hadi mwisho wa kituo cha Morogoro au Dodoma kinyume na tiketi walizokata.
Mwakajinga amesema kuwa kwa kushirikiana na TRC wameanzisha mfumo wa kuwabaini na kuwakamata abiria hao wanaofanya udanganyifu wa kukata tiketi ambazo haziendani na wanakoelekea