Baadhi ya abiria treni ya SGR wadaiwa kuihujumu TRC, nauli haziendani na safari zao

Baadhi ya abiria treni ya SGR wadaiwa kuihujumu TRC, nauli haziendani na safari zao

Abiria wanaotumia Treni ya SGR kutoka Dar es salaam - Morogoro hadi Dodoma wametuhumiwa kuhujumu shirika la reli Tanzania TRC kwa kutolipa nauli ambazo zianendana na sehemu wanazoelekea au vituo wanavyoshukia.

Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro Christopher Mwakajinga amesema abiria wamekuwa wakikata tiketi za vituo vya njiani na pindi treni inapofika katika vituo hivyo wamekuwa hawashuki na kuendelea na safari hadi mwisho wa kituo cha Morogoro au Dodoma kinyume na tiketi walizokata.

Mwakajinga amesema kuwa kwa kushirikiana na TRC wameanzisha mfumo wa kuwabaini na kuwakamata abiria hao wanaofanya udanganyifu wa kukata tiketi ambazo haziendani na wanakoelekea
 
Tanzania tuna tatizo la malezi.
Watu hawana maadili.

Ukisema maadili, watanzania wengi watafikiria ni kuvaa nguo ndefu, kusalimia shikamoo na kutotumia lugha za matusi.

Lakini hatusisitiziwi kuwa waaminifu, wachapakazi, wenye bidii, wawajibikaji, wazalendo n.k
Haya ndiyo maadili sasa!

Kama malezi yetu hayatabadilika, tutaendelea kuwa taifa la watu wa hovyo kwa muda mrefu sana.
Ubarikiwe kwa kuusema Ukweli.
 
20240821_092021.jpg
20240821_092017.jpg
20240821_091909.jpg
 
Wazee wa uzalendo wapo kazini ili waonekane wao hawana shida ila abiria wamekosa uzalendo Kwa kuhujumu.

Badala ya kusema BAADHI YA ABIRIA WANAHUJUMU SHIRIKA wangesema SHIRIKA HALINA MFUMO MZURI WA KUBAINI ABIRIA WAKATI WA KUSHUKA hivyo wanakuja na namna ya kudhibiti changamoto hiyo. Ukilaumu abiria wakati wanaingia (check-in) uliwakagua kwanini wakati wa kushuka ujitoe kwenye ukaguzi na kuwatupia lawama abiria Kwa kulipa nauli ya njiani alafu anakwenda mpaka mwisho.
 
Hii Taarifa kama Taasisi kuiweka public ni inajivua nguo,Udhaifu na uzembe wa Taasisi husika.
 
Back
Top Bottom