PreGE2025 Baadhi ya G-55 wakiwemo Benson Kigaila, John Mrema, Catherine Ruge na Salum Mwalimu wajiondoa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
kila leo conferences.........................nasikia wanakwenda CHAUMA. Wote na Lisu takataka walivyobehave wakati wa kampeni! Takataka tupu, na hili John linaendelea kuwa takataka kiwango cha lami!
Kwani wakienda Chauma tatizo liko wapi? Maalim alipoona CUF haina tija alihamia ACT-WAZALENDO. Viongozi wengine wa CDM wa sasa walitokea NCCR Mageuzi, TLP n.k. CHADEMA kwa muda sasa wamesema kuwa hawa wahitaji basi huu ndio wakati wa kufanya kweli na kuonyesha umma kuwa njia wanayofuata ni sahihi na itakijenga chama. Sasa hivi hamna kisingizio kuwa kuna watu wanawachimba. Kila la heri G55.

Amandla...
 
Kupitia ukurasa wake wa X, John Mrema ametangaza leo kuwa na mkutano na waandishi wa habari Golden Tulip, Masaki.

View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

View attachment 3326774
===

Updates

Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.

Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
View attachment 3326835

Soma pia:

Tuliwambia Tundu Lissu amekitia kiberiti Kichaka, panzi, popo, panya, nyoka na kila mnyama watakimbia tu.

Sisi watanzania tunawatakia kila la kheri huko waendako. Muhimu tuendelee siasa za haki, amani na mshikamano kwa Taifa letu
 
Kwa sasa sio mali ya familia ya ya Mtei na Mbowe.

Dalili kuwa uchaga na Uchagadema unaenda kuisha.

Watanzania wanaihitaji Chadema hii ili ipambane kulinda rasilimali za umma.

Dalili zaonyesha ndio maana CCM inatumia mabavu.

Idu wa Igunga.
Hadi wewe 'mataga' unaihitaji Chadema ipambane kwa niaba yako?

Mag3 Yoda digba sowey
 
Kuhamia CCM itakuwa Worst decision ever, CCM ni jabali na ina Political figures wengi tu Potential hao G55 hakuna ata mwenye influence kama watakuwa Paid kwenda Chama tawala Ili kudraw attention ya issue ya Lissu itakuwa ni for a very short time kama walivofanya Leo, The rest hawana Platform yoyote ya Kuvurukuta Chama cha Mapinduzi
 
Waliamini Kwa asilimia mia kuwa watashinda ule uchaguzi wa ndani ya CHADEMA na ndiyo maana wakaja na ile kauli mbiu Yao ya HAKUNA KUHAMA CHAMA!

Sasa kinyume cha matarajio yao Tundu Lissu ndiyo AKASHINDA. Leo wao ndiyo wamehama chama.
Tundu Lissu anaendelea kutetemesha.

Hadi magereza yatabomoka.

Tujipe muda tu
 
Kupitia ukurasa wake wa X, John Mrema ametangaza leo kuwa na mkutano na waandishi wa habari Golden Tulip, Masaki.

View: https://www.youtube.com/live/Z_apgr0qkZM?si=Lj9DabbYPf6LP8KC

View attachment 3326774
===

Updates

Katika mkutano huu na waandishi wa habari wajumbe wote wa sekretarieti ya CHADEMA Taifa iliyopita wapo isipokuwa watu wawili ambao ndiyo hawakuwepo hapo kwa mujibu wa John Mrema. Ambao ni;
  • Catherine Ruge - Aliyekuwa Katibu Mkuu BAWACHA-Taifa
  • Julius Mwita - Aliyekuwa katibu wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa
  • John Mrema - Aliyekuwa Mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje
  • Salum Mwalimu - Aliyekuwa Naibu Katibu mkuu CHADEMA, Zanzibar
  • Benson kigaila - Aliyekuwa Naibu katibu mkuu CHADEMA, Bara
Wanaeleza kuwa baada ya ushindi, Freeman Mbowe alikubali maridhiano yawepo mara baada ya makundi yaliyopo wakati wa kampeni, ila walishangazwa na kumuona aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti Tundu Lissu aliendelea kumshambulia Freeman Mbowe kama vile kampeni bado zinaendelea, ameeleza Benson Kigaila.
View attachment 3326841
Kigaila anaendelea kueleza kuwa Kuna makundi ngazi ya chini kwenye chama wana vikao vya kuwaengua ama kuwafuta uanachama wanachama waliokuwa wanamuunga mkono Freeman Mbowe.

Wanaeleza pia kuwa ndani ya Chama kuna udikteta uchwara na hivyo wapo kwa ajili ya kuupinga udikteta huo ndani ya chama. Aidha hakuna haki ya kusikilizwa ndani ya chama wala hakuna haki ya watu kuhoji na wanaofanya hivyo wanaitwa wasaliti, njaa. Wanahoji Je, kati ya wao na aliyepinga maridhiano chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe nani msaliti?

G-55 wanasistiza kama unataka kuzia uchaguzi na hakuna mkakati wa kuzuia uchaguzi maana yake umeamua CCM wapite bila kupigwa.

Rasmi wamesema wamejiondoa CHADEMA lakini hawatokwenda CCM, muda ukifika wataeleza ni wapi wanapohamia. Sababu kubwa ni kutokutaka kuwa sehemu ya kifo cha CHADEMA kutokana na yanayoendelea. Hayo yamesemwa na Benson Kigaila aliyekuwa Naibu katibu mkuu Chadema (Bara)
View attachment 3326835

Soma pia:

Kweli chadema ya sasa imefanikiwa kutowa uchafu kiurahisi kabisa. Uchafu wote wa Mbowe umejitowa bila hata kutumia nguvu. Mungu bariki chadema maana imekuwa mkombozi wa taifa sasa baada ya kuongozwa na dalali kwa miaka ishirini na moja. Hata ccm lazima tutawatowa madarakani kwa mwendo wa akili. Maana wao wanafikiri bundiki za polisi zitawabakiza madarakani. No Reform No Election ni mwaarubaini ya majambazi.
 
Back
Top Bottom