Baadhi ya kina dada acheni hii tabia ya kuchukua vitu vya wenza wenu mnapowatembelea

Baadhi ya kina dada acheni hii tabia ya kuchukua vitu vya wenza wenu mnapowatembelea

Hahah, ila mwanamke akivaa nguo yako hiyo ni dalili nzuri sana. Akifikia hapo inatakiwa umpe zawadi ya mimba tu.
 
Miaka 10 nyuma nilikua natoka na demu mmoja anakaa manzese Siku kaja kunitembelea kumbe kachukua cheni yangu Kali sana akaiva then akajifunga ushungi akasepa nayo Aisee yule demu alikua mswahili sana
 
Mtu anakuja kwako na kuanza kutamani vitu kisha kuchukua haijakaa poa. Mimi nilikuwa na track suit yangu nzuri sana ya bei mbaya ila tayari wameshachukua.

Mmoja alichukua jacket na mwingine akachukua track ya chini. Ni kama waligawana. Tshirts kadhaa pia zimechukuliwa.

Majuzi hapa nilinunua blender baada ya kuona ni bora nijitengenezee juice. Bahati mbaya kutokana na ratiba zangu za kuondoka mapema na kurudi usiku nikawa sijaitumia kabisa. Mdada alitaka aondoke nayo ikiwa ndani ya box sijafungua. Hii sio sawa.

Ninajua hali ni ngumu ila mjikaze mnapowatembelea watu wenu. Pia mkija njooni na vitu kama tray la mayai, kuku, hata debe la mpunga ni sawa, kinachobebeka kutoka huko kwenu njoo nacho.
Kwangu Mimi wanagawana kanga tu
 
Huyo wa blender katisha 😹
Mna-date vibaka na wezi kwann wasijichukulie vitu km vimezagaa zagaa.!!
 
Back
Top Bottom