Sasa naona HEAC/TCU wanataka kutuletea kiini macho kuwa suala la bogus degrees ni rampant kwenye private universities only, Mzumbe na vyuo vingine vya serikali wanafanya kama mambo poa!
Siri ya wahadhiri wasiofaa yafichuka
Rehema Isango
HabariLeo; Monday,January 01, 2007 @00:05
KUAJIRIWA kwa wahadhiri katika baadhi ya vyuo vikuu bila kuhusisha Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ni moja ya sababu za kuwa na wahadhiri wasio na sifa za kufundisha vyuoni. Pia upungufu wa wahadhiri nchini, umesababisha baadhi ya vyuo vikuu binafsi kuajiri wahadhiri wa kigeni bila kufuata taratibu zilizopo.
Katibu Mtendaji wa TCU, William Sabaya aliiambia HabariLeo hivi karibuni kuwa kama Tume yake ingekuwa inashirikishwa, basi kusingekuwa na matatizo hayo. "TCU imeshuhudia tatizo hilo kwa baadhi ya vyuo binafsi vilivyoanzishwa kwa kuwa vilikosa wahadhiri wa kutosha na wenye sifa kutoka nchini , hivyo kuingia gharama ya kuajiri wahadhiri na waendeshaji kutoka nje ya nchi" alisema Sabaya.
Sabaya alifafanua kuwa ,hatua ya kuajiri wahadhiri hao ilifanyika kwa kuzingatia taratibu zilizopo za Serikali, lakini vilishindwa kuihusisha TCU ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuhakiki ubora wa elimu ya juu na vyuo vikuu nchini.
Sabaya alisema kuwa ,baada ya kubainika kwa tatizo hilo, hivi sasa TCU inashirikishwa katika shughuli za kutathimini sifa za wahadhiri kutoka nje ya nchi wanaoomba vibali vya kufundisha katika vyuo vikuu nchini.
TCU imetaja sababu za wahadhiri wasio na sifa na uwezo wanaodaiwa kuwepo katika vyuo vikuu vya binafsi kuwa hali hiyo inatokana na upungufu wa wataalamu wenye sifa za kufundisha masomo ya vyuo vikuu katika soko huria.
Hivyo kusababisha kutegemea wahadhiri wachache wanaopatikana katika vyuo vya umma, kwa mpango wa ajira ya muda mfupi au kuajiri wataalamu wasio na sifa za kufundisha masomo ya vyuo vikuu.
Sababu nyingine ni uwezo mdogo wa wenye vyuo binafsi katika kupunguza gharama za uendeshaji, kwa kushindwa kulipa mishahara na marupurupu ya kuwavutia wahadhiri wenye taaluma na uzoefu kutoka ndani na nje ya nchi.
Sabaya alisema kuwa ,baadhi ya wamiliki wa vyuo katika kulinda mambo yao kadhaa kama vile imani, maadili na pengine siri za biashara na mwelekeo mzima wa chuo, kumekuwa na hali ya kutokuwa huru kuajiri wahadhiri na wafanyakazi ambao wanaweza kuwa tishio kwa mambo ambayo mmiliki ana wasiwasi nayo.
Sababu nyingine imetajwa kuwa ni kukosekana kwa uzoefu wa kuendesha vyuo vikuu kwa baadhi ya wamiliki, hivyo kushindwa kutafsiri vema katiba ya Jamhuri ya Muungano, sheria na kanuni za miongozo ya TCU hususan zile zinazoelekeza taratibu za kuajiri na udahili wa wanafunzi.
Alivitaja vyuo vilivyowahi kukabiliwa na upungufu huo kuwa ni Chuo Kishiriki cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Bukoba ambacho kimesitishwa toka mwaka 2000 na Chuo cha Kimataifa cha Teknolojia ya Udaktari (IMTU).
Sabaya alifafanua kuwa, TCU ilibaini kuwa IMTU ilikuwa na wahadhiri wasio na sifa za kufundisha baadhi ya masomo tangu mwaka 2003, na ilikiagiza kusitisha udahili wa wanafunzi katika kozi hizo kwa muda wa miaka miwili ili kupata muda wa kujiandaa kutafuta wahadhiri aliotakiwa.
Hata hivyo, HabariLeo imeshuhudia kuwepo na wahadhiri kadhaa katika vyuo binafsi ambao hawana sifa za kufundisha katika Chuo Kikuu maarufu kilichopo mkoani Iringa(Jina tunalo) na wengine wanaofundisha katika Taasisi ya uandishi wa habari na masuala ya biashara ya jijini Dar es Salaam.
http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=179