Baadhi ya mama ntilie wanatulisha uchafu

Baadhi ya mama ntilie wanatulisha uchafu

Nimemkumbuka yule mama kwenye 3 Idiots alikuwa anasukuma chapati mmewe mgonjwa akakohoa akatumia kisukumio kumkuna kifuani halafu akaendelea kusukumia chapati wakati wageni wanaendelea kula [emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23] ila yule hakuwa mama ntilie ilikuwa ni nyumbani kwa mmoja wa wale rafiki zake na Rancho (nimesahau jina lake), jamaa kwao walikuwa na maisha duni sana.

Halafu jamaa walikuwa wanaona namna chakula kinavyoandaliwa[emoji23][emoji23][emoji23] hatari sana.
 
Lakini kuna baadhi yao ni wasafi sana kiasi kwamba bila kuweka oda huwezi pata chakula
 
Hii ni sekta moja wapo inayowapati kina mama wengi sana kipato, lakini tatizo limekuwa kwenye kuboresha mazingira yao ya kazi.

Hii imenitokea zaidi ya mara tatu maeneo tofauti tofauti, nimeagiza msosi kabla bado sijala nikasema ngoja nikague kijiko aiseeeh ni aibu, nimeletewa kijiko kinaonekana kimetoka kutumika muda si mrefu bado kina mabaki ya chakula. Kwa maana hiyo hakijasafishwa vizuri

Maeneo ya kulia chakula hasa mezani, nzi kibao unakula chakula mara nzi kadondokea kwenye chakula inatia kinyaa.

Mama ntilie kama mpo humu naomba mbadilike mnatulisha uchafu, jitahidini kuwa wasafi.
Mkuu inaoneka huko kwa mama ntilie siyo mahali sahihi kwako.maana wengine hayo yote yameshazoeleka wala maji ya kunywa ya kichemshwa hayahitaji kabisa
 
...what you resist persist..

Nakumbuka enzi za chuo kuna kile chakula cha chini kabsa (maukoko/mabaki) wajuba tulikuwa tukikita stuff au joro....aisee kile chakula maandalizi yake ukiyaona unaweza sema anae enda kula ataharisha au atakosa choo kbsa but maajabu wajuba adi tunamalizia chuo hakuna Alie sumbuliwa na tumbo wa choo...

...muda mwengine vile vinavyotutokea maishani mwetu ni matokeo ya mawazo yetu...
 
Back
Top Bottom