BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Mchakato wa Upigaji Kura Jimbo la Siha umeanza kuingia doa baada ya kudaiwa kuwa upigaji Kura umekamilika lakini imetokea hali ya kutoelewana kati ya Wasimamizi wa Mchakato na baadhi Mawakala.
Inadaiwa kuwa Katibu wa CCM Wilaya ametoa maelekezo kuwa msafara wa kubeba Kura uondoke bila kufuatwa na baadhi ya Mawakala uamuzi ambao umepigwa na Mawakala hao.
Timu ya Mawakala wanaopinga wanaamini Kura zilitakiwa kuwekwa wazi, matokeo yajulikane kabla ya kwenda kuwasilishwa Ofisi ya Wilaya, wanadai kuwa yote hayo hayajafanyika na pia Katibu anataka msafara uende bila Wakala kadhaa jambo ambalo timu hiyo inajua kufanya hivyo ni sawa na kuruhusu kukubali Kura zao kupigwa juu kwa juu.
Washiriki wanaowania kupitishwa katika Kura za Maoni ndani ya CCM ili kupewa ridhaa ya kuwakilisha chama kwenye Ubunge ni; Dkt. Godwin Aloyce Mollel, Tumsifu Andree Kweka, Agrey Desile Mwanri, Petro Robert Kitingala, Meijo Lolionyo Laizer, Dkt. Aggrey Humphrey Mosha na Bertha Izack Mlay.