Baadhi ya Mawaziri Serikali ya Awamu ya Sita wamekuwa na Utajiri wa ghafla usio kifani

Baadhi ya Mawaziri Serikali ya Awamu ya Sita wamekuwa na Utajiri wa ghafla usio kifani

leteni huo ushahidi wa utajir wao, la si hivyo hayo ni majungu tu munapika kama kawaida
bitimkongwe siku hizi kimyaaa......, kelele zimekoma.Kumbe mambo yalikuwa hayaja nyooka, sasa umeshiba mpaka umevimbirwa,hata Bweni hukumbuki tena.Sawa.......,ila noma bwana.
 
Kuna baadhi ya Mawaziri wa Awamu ya Sita wamekuwa na utajiri mkubwa na wa ghafla usioendana na kipato chao.

Hii inathibitishwa na maelezo ya Wabunge wenzao ambao hali zao ni ngumu kifedha kwa sasa. Mawaziri hao wamekuwa na tabia ya kugawa fedha ili Bajeti zao ziungwe mkono kwa mujibu wa maelezo ya mtoa taarifa kutoka Bungeni.

Kwa kuanza futailieni utajiri wa mawaziri wa sekta hizi;

1. Maji
2. Kilimo
3. Uchukuzi zamani Ujenzi
4. Mambo ya Nje zamani Nishati
5. Fedha
6. Mipango hasa baada ya Mkataba wa DP
7. Ardhi na danganya toto zake za PR
8. TAMISEMI, huyu yeye anakusanya bila aibu

Kama tungekuwa na vyombo imara vya uchunguzi wahusika hao wanatakiwa kuwa gerezani. Wanakula, wanaiba bila kunawa mikono.
Ongeza Afya, viwanda na Mazingira
 
mambo mengine bora hata kutokuyajua. maana inasaidia nini kuyajua kisha huna la kufanya

"kwenye wingi wa maarifa kuna wingi wa huzuni"
 
Hii nchi ukiaupata utajiri ukiwa serikalini utasemwa kuwa ni mwizi.

Pia ukiupata umasikini ukiwa serikalini utasemwa kwamba ni mzembe.
 
Hata mie nikipewa uwaziri nitawapiga tuu. Grabbing 6 figure in $ and investing heavily in real estates. Bakini na uzalendo wenu wazalendo.
Hapana kula mali ya umma ni moja ya laana kubwa sana ipo siku laana hiyo itarudi kwako namna yoyote,maana ukila mali ya uma jua kuna mjumuisho wa mambo mengi mabaya umefanya .
 
Hapana kula mali ya umma ni moja ya laana kubwa sana ipo siku laana hiyo itarudi kwako namna yoyote,maana ukila mali ya uma jua kuna mjumuisho wa mambo mengi mabaya umefanya .
Uko sahihi angalia wote waliokwiba mali ya umma wameishia vipi.
 
Ushawahi kuona minoti imewekwa na kujazwa kwenye mfuko wa Shangai kaja 😄
Tena mifuko mitano 😄
Hiyo nliambiwaga na dereva wa waziri mmoja awamu iliyopitapita huko 😄
Nkamjibu sijawahai,ila na nyie mafala ulishindwa kumpiga hela
Ungemtandika hela hamna kesi hapo 😄

Ova
 
Nchi ina ubadhirifu na majizi ya kila aina na kila wakati na haijalishi wakati huo nchi ipo chini ya kiongozi gani,kusema kweli hakuna wakati nchi hii imekuwa na unafuu katika vitendo vya kifisadi hilo wala tusiongopeane sasa tukitaka mafanikio jambo muhimu ni kuacha unafiki maana hata Mwenyezi Mungu ameshasema kamwe hatoweza kuwapa nusura waja wake hadi watakapoacha unafiki.
Nchi yetu au sisi wananchi tumekuwa wanafiki sana kwa sababu matusi, lawama,malalamiko, kashfa, kejeli na vijembe vya kila aina utavisikia tu pale nchi ikiwa chini ya uongozi wa akina fulani lakini ikiwa chini ya uongozi wa wale wengine watu wote wapo kimya hata lifanyike baya gani! Watanzania tuache chuki na unafiki kiongozi akiwa mbaya athari yake tutaipata wote haijalishi kiongozi huyo unafanya naye Ibada Msikitini au Kanisani.
 
Kuna baadhi ya Mawaziri wa Awamu ya Sita wamekuwa na utajiri mkubwa na wa ghafla usioendana na kipato chao.

Hii inathibitishwa na maelezo ya Wabunge wenzao ambao hali zao ni ngumu kifedha kwa sasa. Mawaziri hao wamekuwa na tabia ya kugawa fedha ili Bajeti zao ziungwe mkono kwa mujibu wa maelezo ya mtoa taarifa kutoka Bungeni.

Kwa kuanza futailieni utajiri wa mawaziri wa sekta hizi;

1. Maji
2. Kilimo
3. Uchukuzi zamani Ujenzi
4. Mambo ya Nje zamani Nishati
5. Fedha
6. Mipango hasa baada ya Mkataba wa DP
7. Ardhi na danganya toto zake za PR
8. TAMISEMI, huyu yeye anakusanya bila aibu

Kama tungekuwa na vyombo imara vya uchunguzi wahusika hao wanatakiwa kuwa gerezani. Wanakula, wanaiba bila kunawa mikono.
Wasitiwe ndani fyeka kabisa
 
Back
Top Bottom