Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

JF na ndoto za alinacha!!! Million moja itoshe? Thubutu
 
Mtumishi una uwezo wa kukopeshwa na Benki Kwa dhamana ya mshahara

Lakini ukishaanzisha biashara, unakopea biashara yako pia

Ukisema usubiri Mtaji uupate baada ya kulipwa kiinua mgongo, lazima maisha yakuchakaze Mkuu

Tuchukue tahadhali
Of course hela ya kustaafu si hela ya kuchezea. Ni hela ya kununua Bond tu. Siye tulistaafu miaka 6 iliyopita
 
JF na ndoto za alinacha!!! Million moja itoshe? Thubutu
Pension pekee haitoshi, ndiyo maana tunashauri kuweza kujiongeza Kwa kufanya Uwekezaji

Mfano unapokea Posho ya Mwezi shilingi 500,000

Lakini kupitia Uwekezaji wako unapata maybe 2,500,000 Kwa Mwezi

Mtu wa hivyo hawezi kuchukia maisha yake ya kustaafu Bali atayafurahia, na Uzee wake utakuwa murua kabisa

Kama utakuwa na maisha ya unga unga mwana ndiyo itakuwa shida mno Uzeeni kwako
 
Of course hela ya kustaafu si hela ya kuchezea. Ni hela ya kununua Bond tu. Siye tulistaafu miaka 6 iliyopita
Hongera sana Mkuu kuweza kustaafu na kuwekeza pia
 
Unawazo zuri sana lakini shughuli unazopendekeza ni ngumu kwa wastafu hasa wa hali ya chini... Me mtendaji wa kijiji nikafungue kampuni ya kitalii? Au niwekeze mtandaoni
 
Lakini mzee mwenzangu hujawahi kuniambia nani hasa anaufubaza moyo wako humu🤣🤣🤣au hutaki ijulikane ili uendelee kula mema ya jf🏃🏃🏃
Humu sijabahatika Mzee mwenzangu, maombi yangu yote yamekuwa rejected

Wanasema wanaogopa naweza kupewa yale mambo katikati ya safari nikapandisha Presha

Kwa kweli Sina bahati kabisa 🤗
 
Unawazo zuri sana lakini shughuli unazopendekeza ni ngumu kwa wastafu hasa wa hali ya chini... Me mtendaji wa kijiji nikafungue kampuni ya kitalii? Au niwekeze mtandaoni
Shukrani Mkuu

Biashara sio lazima ziwe hizo, unaweza kufanya Uchaguzi sahihi kadri utakavyoweza

Muhimu kabla hujawekeza, Fanya tathmini ya kina

Hata ukifungua workshop ya kutengeneza grill na milango ya mbali, bado inaweza kuwa fursa nzuri

Maana Siku hizi Kuna mashine nyingi nzuri za Kichina Kwa bei rahisi

Ni kuchagua site nzuri tu, maana Siku hizi mahali pengi watu wanajenga
 
Hongera sana Mkuu kuweza kustaafu na kuwekeza pia
Hela huwa haitoshi ujue. Na gharama za uzee ni kubwa ajabu.

Jambo la msingi katika kujiandaa kustaafu ni pamoja na kuwafunza wategemezi wako kuwa hakuna urithi. Hakikisha kila mmoja ajifunze kujitegemea. Utapata shida sana iwapo kila mmoja anasubiri pension yako. Ukiwa na wategemezi au ndugu hata watoto wanauliza zitaingia lini, juwa chamoto unacho. Hata wewe binafsi, kama unasikilizia zitaingia lini, juwa kustaafu ni kugongwa na kitu kizito kichwani.

Imagine hata shemeji yako anayeoa dada yako anakuuliza lini utapokea pension yako.

Uanzishwaji wa miradi ni jambo jema isipokuwa kitu uaminifu ni tatizo kwa sasa.

Nipende kusema kuwa maisha hayana fomula, kama wengi hapa JF tunavyofikiria, after all hapa JF mwanamme anaanzisha nyuzi kuhusu wanawake wanavyojihisi wakati hajawahi kuwa kuwa mwanamke. Vijana wanaongelea maisha ya kustaafu wakati sasa hivi anatafuta ajira baada ya kutoka chuo, n.k.
 
Shukrani sana Kwa mchango wako Mkuu

Kuna jambo la maana hapo umesema kuhusu kuwajulisha Wategemezi wako kuondoa hiyo mind set ya kutaka kutegemea pension yako

Of course hili jambo, baadhi ya familia nimewahi kusikia wakiuana kabisa kwasababu ya pension ya Mzee

Barikiwa sana Mkuu, na Mwenyezi Mungu akupe afya njema
 
Wewe unaweza kuyapenda!!! Aaah hapana jamani🤣🤣
Ila huyo Mpare ametushangaza sana, Siku ile ya harusi tulilishwa pilau/biriyani na Kuku Choma za kutosha

Na alihaidi nawe Mjukuu, ungeenda kula hayo masotojo

Sasa hii ya kukulisha Makande ya Upareni hatukuitegemea 😜
 
Ila huyo Mpare ametushangaza sana, Siku ile ya harusi tulilishwa pilau/biriyani na Kuku Choma za kutosha

Na alihaidi nawe Mjukuu, ungeenda kula hayo masotojo

Sasa hii ya kukulisha Makande ya Upareni hatukuitegemea 😜
Ni huzuni babu😭😭😭
 
Ni huzuni babu😭😭😭
Ila hata ungeolewa na yule Kijana wa Njombe, bado ungelishwa Makande

Useme Makande ya Njombe ungelishwa na Maparachichi 😜
 
🤣🤣🤣🤣 hunitakii mema babu!!
Hahaha............kule ungefundishwa Kilimo cha Miti, wakati Upareni umefundishwa biashara na Ubahili

Hapo ushindwe wewe tu, kuninunulia ile Kiko niipendayo 🤗
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…