Maana ya kustaafu ni kupumzika baada ya kufanya kazi kwa miaka yako 60 na kuchoka kimwili na akili. Sitarajii eti mtu anasaafu halafu aendelee na kufuga ua kulima au kufanya biashara. Ukistaafu unatakiwa kupumzika warume! kwa maana hiyo jiwekee sasa vituo vya kukusanya pesa ukishastaafu. Tunataka tumuone mstaafu anaamka asubuhi, anapiga mazoezi yake ya kutembea tartiiiibu, akirudi home anaoga, anapiga breakfast health anapumzika chini ya kamwembe hapo nje na baadae anatoka kwenda kukusanya maokoto mdogo mdogo na kupiga umbea kidogo na majirani.... jioni anaingia kanisani au msikitini anamshukuru Mungu wake anarudi kulalala..... wekend anapanda SGR anaenda kusalimia wajukuu. huku ndio kustaafu