Hapa,hii biashara ya usafirishaji kwa wazee ni kujitafutia shida tu unless iwe anaifanya akiwa anaijua si chini ya miaka mitatu lakini kama mgeni ghafla atie 70Mill zake humo mwaka hauishi tunamkosa.
Mimi huwa nafanya kazi za Bajaj,juzi tu mwezi wa tisa alinipigia dalali mmoja Tegeta kuna chuma no E inauzwa nilipoona picha sikupoteza muda mimi mbio kufika mule ndani mna pikipiki Boxer na TVs saba nikaambiwa Bajaj zilikuwa sita zimeondoka tano imebaki moja mpyaa,akaja mzee ananisisitiza “kijana wangu,naomba bei nitakayokupa usipunguze hata kidogo nionee huruma hasara isiwe kubwa”,bei anataka 8mill,Bajaj ina bima kubwa siyo chini ya Tsh 641,000/=,LATRA ameshalipa mapato TRA 120,000/= amelipa Bajaj mpya dukani currently 10,700,000/= so kwa haraka haraka ilimkata siyo chini ya 3mill.
Usajili wake ilikuwa may mwaka huu so kama Bajaj zilikuwa sita atakuwa alipata hasara siyo chini ya 18mill ndani ya miezi minne sasa kwa hali hiyo kuna kupona mtu?lalamiko lake kubwa lilikuwa ni vijana hawaleti hela wakati ndiyo walimfata wakimuahidi hiyo kazi ina hela awape vitendea kazi.kuhusu bei nilimshusha kidogo akajaa sijui wenzangu walionitangulia nao walimuumiza vipi.