Baadhi ya miradi ya uwekezaji inayoweza kufanywa na wastaafu

Lazima tujiandae, ujana ni hatua nzuri ya kujipanga kiuchumi...namfahamu Mzee mmoja ni mwanajeshi mstaafu alikuwa anafanya kazi sehemu very sensitive kiusalama, anaishi maisha safi kabisa, Mzee alipambana miaka hiyo kitambo, alinunua maeneo kitambo sana ambapo maeneo hayo Leo hii Ili uyapate au upangishe lazima mfukoni kwako usiwe mtu wa kipato cha kati cha chini, kipato cha kati cha kati ndo wanaweza himili kulipa....

Hivyo maandalizi nadhani yatakiwa yaanze mapemaaa kabisa.
 
Pesa ya kustaafia sio ya kufanyia maendeleo bali ni ya kufanyia maboresho zaidi kwa kile ulichokianzisha ksbla ya kustaafu na kikawa kunakuletea manufaa hivyo unaboresha ili upate manufaa zaidi
Ni kweli Mkuu, umri wa kufanya Uwekezaji ni sasa ukiwa Kazini.

Ukisubiri kuwekeza na hela za Pension huchelewi kurudisha namba Kwa Sir God
 
Huyo Mzee alikosea hapo kwenye kununua gari used, kwanza inashauriwa usinunue gari used Tanzania ukiwa above 45, utakufa Kwa Presha
Nakwambia alikua hajui hata kudrive akanunua gari ilikua ndogo bora hata passo.mafuta aweke spea sijui service alijuta alikuja uza kwa hasara mno mpaka leo kachoka yule mzee anasubili vikodi vya walimu aliowapangisha vyumba vitano ndo apate kula
 
Huyo alifanya vizuri kukumbuka kuwekeza

Hata sasa Kuna fursa kubwa sana kwenye biashara ya Viwanja

Unanua mapori kuelekea Kisarawe,Kibaha, ama Mkuranga, baada ya muda unavipima kisha kuviuza Kwa bei nzuri tu

Vijana wajifunze kupitia Wazee wastaafu
 
Nakwambia alikua hajui hata kudrive akanunua gari ilikua ndogo bora hata passo.mafuta aweke spea sijui service alijuta alikuja uza kwa hasara mno mpaka leo kachoka yule mzee anasubili vikodi vya walimu aliowapangisha vyumba vitano ndo apate kula
Pole yake aisee

Kuishi Kwa Kodi ya Vyumba vitano tu, mbona changamoto, hapo labda unapata hela ya kula tu
 
Ni kweli Biashara ya Usafirishaji ina changamoto nyingi, lakini ukisajiri kama Uber/Bolt walau ina nafuu.

Ukiweza uwe na ViPasso kama vitatu hivi uvisajiri kama Uber/Bolt utakuwa na uhakika wa kupata hela ya kuliko Bajaj

Bajaj inahitaji Msimamizi Kijana, ambaye ataweza purukushani za Vijana wenzie
 
Kwa msosi huo, huwezi kuwa na afya imara

Maana utakosa hata hela ya matunda hapo kwenye huo Mlo 🙌
Kabisa.tujifunze kuwekeza vyanzo vingi vya mapato.ndo maana bakhresa anauza mpaka mandazi unga na matakataka mengine kibao.iweje mwajiriwa utegemee mshahara ukikata ndo utafute chanzo kingime ni ujinga ujinga mtupu
 
Ukiona kama taifa mtu anawaza kuwekeza baada ya kustaafu (au uwepo wa umuhimu wa kufanya hivyo) fahamu kwamba kama taifa tumepotea njia na tupo kwenye RAT RACE..., na kama hayo uliyosema ni rahisi kuyafanya why wait mpaka ustaafu na usianze leo... Anyway kwa nchi kama yetu Waastafu (Pensioners are better off) what about hawa wabangaizaji wa leo ambao ni wazee wa kesho...

 
Kabisa.tujifunze kuwekeza vyanzo vingi vya mapato.ndo maana bakhresa anauza mpaka mandazi unga na matakataka mengine kibao.iweje mwajiriwa utegemee mshahara ukikata ndo utafute chanzo kingime ni ujinga ujinga mtupu
Ni sahihi Mkuu

Unakuta una miradi yangu miwili mitatu kusukuma maisha

Mradi wa kwanza unakupa return ya 35,000/day
Wa pili 50,000/day
Wa Tatu unakuletea hesabu ya 250,000/day

Hapo una uhakika wa kuvuna milioni 3 hivi Kwa Mwezi.

Ukiokota na kamposho Kako ka Mwezi shilingi 450,000 una kuwa na kama 3.5M hivi

Unaondokana na stress hivyo mapumziko yako ya Uzee yanakuwa poa kabisa

Ni mwendo wa kwenda kucheza Golf na Wazee mwenzio hapo Club Gymkhana
 
Mkuu maisha ya Watanzania wengi ni duni kiuhalisia

Hao wanaopokea mshahara Kwa Mwezi ndiyo walau wanaonekana Wana unafuu wa maisha, maana Wana Bima wakiugua pamoja na Kipato cha uhakika japo hakitoshelezi

Ndiyo maana nimeandika Uzi wa kuwakumbusha waliopo makazini,kukumbuka kujiwekeza

Otherwise, maisha yao ya Uzee yatakuwa ni shida mno
 
Najua kusema ni rahisi sana ila elewa kuwa pension imetengenezwa na serikali na sio matakwa ya mtu na mtu
Kustaafu sawa ila je utaweza kuranda randa kwa wajukuu kila leo?
Hata kama una hela lakini uzee na kukaa kula bata ni shida
Utapata maradhi ya kila aina bila kuwa na harakati yaani activities
Kama niwe na miaka 67 halafu nikae tu kwa kweli siwezi

Ntaacha kufanya kazi mpaka mwili ugome kwenda na likizo itakuwa sina ulazima maana nimeisha tembea sana dunia hii
Pension za huku nitalipwa kama 3m ya bongo kila mwezi
Lakini siwezi kulala tu kila siku lazima nifanye kitu hata kusimamia mijengo itakuwa idea nzuri ila kulala tu na kukaa chini ya mti hapana
Mawazo yatakusumbua sana ukiwa umekaa tu unahitaji kazi isiyo ngumu ila sio biashara za duka au kukimbizana na mifugo
 
Umeleweka mkuu na mimi nikimaanisha hicho.kunaa bwana mmoja ni mwalimu tena yuko kijijini.yule bwana kabla ya kustaafu alikua analima na kununua mashamba na maeneo na kujenga kastaafu miaka msaba iliyopita baba yule ana maisha mazuri mno miaka mitatu nilipata msiba wa dada yangu ndugu yule alikuja na usafiri mpya na gunia za mpunga kwa ajili ya kula waombolezaji wa msiba na ana familia kubwa kasomesha watoto wengine wanafanya kazi wameolewa na wameoa.kiufupi hana stress ana maeka ya mashamba na analimisha watu.ni mwl wa primary mstaafu kijij8ni kabsa
 
Umesema sahihi Mkuu

Kuwa na shughuli baada ya kustaafu kunasaidia kuimarisha afya

Kuna Semina moja niliwahi kukutana na Mstaafu anaitwa Mathias, ndiyo mwenye lile eneo maarufu pale Kibaha (Kibaha Kwa Mathias)

Yule Mzee bado anafanya kazi zake za Ushauri (Consultant) kupitia Kampuni aliyoifungua

Na ukimwona, unaona bado ana nguvu, nafikiri kutokana na kuendelea kujishughulisha

Nina Mzee wangu baada ya kustaafu kazi miaka ya Mwanzoniwa 90, aliamua kujiajiri kupitia kazi za Utaalamu wa fedha, ama Kampuni yake ya Auditing

Yupo hai hadi sasa akifanya kazi ya kufungia hesabu makampuni binafsi pamoja na kufanya Ukaguzi (Auditing)

Bila kujishughulisha, haufiki miaka 65 unakuta umeshaaga Dunia
 
Hongera sana Kwa huyo Mstaafu mwenzetu kuweza kuwekeza mapema

Mtu wa hivyo hakosi milioni 100 hadi 300 Benki

Kwa Vijana waliopo makazini

Kupanga ni Kuchagua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…