Baadhi ya ndugu wauza nyumba ya familia Kariakoo iliyokuwa na waqfu. Mapanga yatembea nje nje

Nimeona video inatrend ya ugomvi mkubwa wa nyumba ya urithi Kariakoo mtaa wa Manyema.

Nyumba hiyo ya ghorofa 5 ilijengwa na mzee anaeitwa Mohammed Alidina ambae alifariki miaka kazaa iliyopita.

Mzee huyo wakati akiwa hai alitoa sehemu ya nyumba hiyo. Floor ya juu itumike kama madrassa na kufanya taratibu za kukabidhi kwa msikiti ambazo waislamu wanaziita waqfu. Ghorofa zilizobaki aliendelea kuzitumia kuishi na zingine kupangisha appartments na fremu kwa wafanyabiashara Kariakoo.

Baada ya huyo mzee kufariki aliacha watoto 11, ambao watoto wao waligawana hizo appartments na fremu na kuendelea na maisha.

Mbeleni watoto wachache wa kiume wa marehemu mzee huyo wakapendekeza wazo la kutaka nyumba hiyo iuzwe kila mtu akajenge kwake. watoto wengine wakapinga kwamba hawataki nyumba iuzwe maana baba yao enzi za uhai alisema nyumba isiuzwe na akatoa sehemu ya nyumba iwe madrassa inayomilikiwa na waislamu wote. sasa watauzaje nyumba yenye wakfu ambayo ni mali ya waislamu wote.

Watoto wenye wazo la kuuza wakaona hapa kuuza ngumu. wakaamua kwenda kumshirikisha imamu wa msikiti ambao ulipewa wakfu sehemu ya nyumba hiyo. maana msikiti ulikuwa na documents za wakfu walizopewa na marehemu baba yao.

Kimya kimya wakashirikiana na imamu wa msikiti uliopewa hizo documents. wakatafuta mteja Mkinga mmoja wakamuuzia nyumba bila watoto wengine kujua.

Mbeleni mkinga huyo ambae ni mnunuzi aliyonunua hiyo nyumba akaenda kuchukua mali yake. Ndipo watoto wengine wakagundua nyumba imeuzwa. Ndipo ugomvi mkubwa ukaibuka na mapanga juu.

View attachment 2928225
Ndio maana Mimi nawapenda sana mabinti zangu. Si uliona yule binti wa kabwe alivyomkatalia kumsalimia makonda.
 
Nipo Kariakoo, anaesimamia hiyo nyumba ni dd yao. Ishu ni kua anawapiga ndugu zake. Mfano frem ni 1,000,000 anawaambia wenzake kodi ni 600,000. Hiyo ndo shida
Huyu dada inaonekana alitaka kuliuza pekee yake hilo ghorofa au kumkabidhisha mme wake kufaidi yeye na watoto wake kumbe ndugu wakashtuka mapema tuuze kila mtu afe na chake maana watu watakufa je ghorofa wajukuu watahusishwa kurithi mali hiyo akili kumkichwa!!
 
Nimeona video inatrend ya ugomvi mkubwa wa nyumba ya urithi Kariakoo mtaa wa Manyema.

Nyumba hiyo ya ghorofa 5 ilijengwa na mzee anaeitwa Mohammed Alidina ambae alifariki miaka kazaa iliyopita.

Mzee huyo wakati akiwa hai alitoa sehemu ya nyumba hiyo. Floor ya juu itumike kama madrassa na kufanya taratibu za kukabidhi kwa msikiti ambazo waislamu wanaziita waqfu. Ghorofa zilizobaki aliendelea kuzitumia kuishi na zingine kupangisha appartments na fremu kwa wafanyabiashara Kariakoo.

Baada ya huyo mzee kufariki aliacha watoto 11, ambao watoto wao waligawana hizo appartments na fremu na kuendelea na maisha.

Mbeleni watoto wachache wa kiume wa marehemu mzee huyo wakapendekeza wazo la kutaka nyumba hiyo iuzwe kila mtu akajenge kwake. watoto wengine wakapinga kwamba hawataki nyumba iuzwe maana baba yao enzi za uhai alisema nyumba isiuzwe na akatoa sehemu ya nyumba iwe madrassa inayomilikiwa na waislamu wote. sasa watauzaje nyumba yenye wakfu ambayo ni mali ya waislamu wote.

Watoto wenye wazo la kuuza wakaona hapa kuuza ngumu. wakaamua kwenda kumshirikisha imamu wa msikiti ambao ulipewa wakfu sehemu ya nyumba hiyo. maana msikiti ulikuwa na documents za wakfu walizopewa na marehemu baba yao.

Kimya kimya wakashirikiana na imamu wa msikiti uliopewa hizo documents. wakatafuta mteja Mkinga mmoja wakamuuzia nyumba bila watoto wengine kujua.

Mbeleni mkinga huyo ambae ni mnunuzi aliyonunua hiyo nyumba akaenda kuchukua mali yake. Ndipo watoto wengine wakagundua nyumba imeuzwa. Ndipo ugomvi mkubwa ukaibuka na mapanga juu.

View attachment 2928225
Nyumba aiuzwi kama mayai bana yani nyumba ya urithi iuzwe kienyeji we
 
Bongo nyoso!
Kule tunasikia mfanyabiashara aliyekuwa anaidai TRA milioni 980! Ajiua! Huku nyumba inauzwa kinyemela, pesa zinapolwa na polisi wanakaa kama hawaoni!
Richa ya kupewa, taarifa,
 
Akienda kusipokua na mtu mwingine mwenye msimamo km wake wataiuza,
Kwani mzazi alisema isiuzwe? Kwa nini wasitumie mahakama kupata ufafanuzi wa kisheria? Hii tabia ya baadhi ya wanandugu kuuza Mali halafu wanageukiana ili kumtapeli aliyenunua lazima wanasheria waliangalie vizuri.

Mke na mume wanakubaliana kukopa hela kwa dhamana ya nyumba yao, hela zikiisha mume anamtuma mke mahakamani kudai eti nyumba imeuzwa bila ridhaa ya familia, lengo kuwaibia wakopeshaji, hata wanandugu wa kariakoo ndio mchezo wao
 
Huyu dada inaonekana alitaka kuliuza pekee yake hilo ghorofa au kumkabidhisha mme wake kufaidi yeye na watoto wake kumbe ndugu wakashtuka mapema tuuze kila mtu afe na chake maana watu watakufa je ghorofa wajukuu watahusishwa kurithi mali hiyo akili kumkichwa!!
Nyumba ya mirathi ina taratibu zake kuuza.Huwezi kuuza kitu cha watu wengi,kijanja janja.Huyo Sheikh,na huyo mnunuzi wakamatwe,ni wezi hao na ni matapeli,na kama yupo wakili,kahusika na huu utapeli,pia akamatwe.
 
Huyo Mkinga imekula kwake. Mali za urithi ili ziuzike kisheria lazima lazima BENEFICIARIES CONSENT iandaliwe ili kila mnufaika atie sahihi yake. Hiyo inaandaliwa na wakili. Je waliuziana kimila au mbele ya wakili?
Na Wazir Jery Slaa alifika hapo! Mkinga anaulizwa una hati au documents yoyote?, hana, ohh nipo katika mchakato wa kubadilisha jina kwanza....Daah.
 
Umeandika nini? Sijakuelewa klkinahusiana na nilichoandika au umemjibu mtu mwingine kwa bahati mbaya ikaja kwangu. Nimesema MIMI NI MKRISTU ILA NINAKUBALIANA NA MSIMAMO WA HUYU DADA
Amekujibu kwa hisia hakusoma na kuelewa ulicho andika.
Wewe ulimaanisha yule dada mweupe mlalamikaji ambae ni mtoto wa mwenye nyumba.
Yeye alidhani unamzungumzia yule dada mweusi aliyevaa mavazi ya kujifunika Kama hijab bi Theresia Shayo aliyetoa maoni yake pia.
 
Back
Top Bottom