Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Kubota,
Hapa ndo ninapotatizwa, nataka niheshimu mawazo yao lakini naona kama vile yanafuta fursa zilizopo; kwa mfano wengi wana mwelekeo mmoja wanawaza niashara zinazofanana. ninahisi kuwa zitaongeza ushindani wa wenyewe kwa wenyewe kwanza kwenye soko na pili kwenye upatikanaji wa malighafi kwa sababu ni kijijini kuna limited resources na markets.

Ila hili la kuwapa fursa ya kuona wengine wanafanya nini (by Chasha) ntalizingatia
 
Kitumbo,
Mheshimiwa Kitumbo nimeijiwa na wazo lingine! Kuna dhana moja kwenye suala la kuleta maendeleo vijijini inaitwa, one village one product au one district one product!

Yaani kijiji au wilaya nzima inajikita kwenye uzalishaji wa kitu kimoja tu! Hii iko zaidi kwenye uzalishaji kuanzia mashambani, majumbani (viwanda vidogo), uvunaji mali asili hadi kuchonga vinyago. Kama biashara waliyoipendelea watu wako ni ya aina moja yaani uzalishaji wa kitu aina moja basi mnaangalia soko la mbali ambako biashara hiyo inaweza uzika!

Kwa kuwa na product moja kijijini kutasaidia kuwa na nguvu ya kufikia masoko ya mbali na kuvuta wanunuzi kufuata hiyo mali hapo kijijini! Kunamaeneo ni maarufu kwa kusuka na kuuza mikeka, kuchoma mkaa, kuchonga vinyago, kilimo cha nyanya, vitunguu, kufinyanga vyungu etc! One village one product! Unaionaje hiyo!

Nazingatia angalizo lako kuwa kunaufinyu wa upatikanaji wa malighafi hiyo nayo ni changamoto!
 
Kubota,
Hili wazo la Wilaya sijui Kijiji kimoja zao moja, liko kisiasa zaidi na haliwezi fanikiwa kamwe, na sijui ni watu gani walikuja na haya mawazo.

Ukingalia karibia nchi nzima wanalima Mazao yanayo fanana, Chukulia mfano Mahindi, Kila sehemu yanalimwa, maharage hivyo hivyo, na mazao mengine hivyo hivyo, Ukija kwenye Mazoa ya Biashara kama Karanga utakuta Ukanda wote wa kati wanalima, Ukija kwenye Kahawa inalimwa Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Tarime, Bukoba, Chai inalimwa Mbeya, mitaa ya Ilinga na Tanga.

Vijijini kinacho takiwa ni watu wenyewe kuwezeshwa kulima kilimo cha biashara hata kama Vijiji vuote vitalima mazao na kuzalisha vitu vinavyo fanana si mbaya ilimuradi vizalishwe kibiashara zaidi.

Na tatizo kubwa linalo tusumbua ni hii substance Ecomy yetu tuliyo nayo, yaani Substance economy ni kikwaza sana kwa biashara kusonga mbele, kwa sababu Unaweza amua kufuga kuku na utashangaa mtaani kila mtu anakuku anawafuga kwa ajili ya kitoweo chake so hii tiyali ni tatizo kubwa sana.
 
Chasha thanks so much, nilikuwa sijaisoma hii.

Kuna mtu anauliza mitaji, mie naona wengi wetu hapa ni wafanyakazi, mitaji itapatikana kwa kuwa na good saving habits, ukiGoogle wenzetu wanambinu nyingi nilizojifunza chache.

1. kupunguza matumizi kwa kubeba lunch box yako badala ya kununua kila siku (3500 - 10000)

2. Kupunguza matumizi ya simu yasiyo lazima

3. Kupunguza manunuzi ya mavazi na au outing zilizo costly au frequency, badala ya hoteli ghali weekend waweza kwenda beach, fellowships, meet family, friends etc

4. Kupunguza namba ya helping hands au wasaidizi mfano kila weekend salon waweza suka au tengeneza mwenyewe, kulima maua au bustani ndogo, tuition ukafanya mwenyewe au siblings, car washing yaani mshahara wetu huu tunaulipa kwa watu kibao kwa kazi ambazo mkiamua kama family weekend mnaifanya bila shida

5. Kupunguza matumizi ya petrol kwa kutumia usafiri wa basi inapowezekana mfano kuna basi za 1000 kuliko petrol 15000-30000 daily

Ukiangalia mianya mingi yakubana matumizi kwa mwezi unajikuta umepata mtaji wa kuanzia kitu kidogo tatizo watu hawataki shida....
 
Unacho sema Mama Joe ni kweli kabisa, Kuna Rafiki yangu Juzi alikuwa ananipatia full story za Maisha ya Wachina, kwa kweli Tanania tunayo kazi sana Bila kubadilika maendeleo tutayasikia kwenye redio, Wachina wana nidhamu ya Hali ya Juu kabisa katika maswala ya fedha na kwa wachina Familia nzima ni lazima ifanye kazi si kwamba Baba na Mama waende kutafuta Huku nyuma watoto wanabakia kula tu ma kutazama TV kutwa nzima, China Kijana akimalzia Chuo ni lazima achacharike hata kwa kuuza pipi, na si kwamba auze pipi then pesa ale no ni pesa ya familia,

- Chiana biashara ya kupigana offa hawaijui
- China Biashara ya kutafuta sifa kwenye Mavazi na magari hawaijui, kuna public transport na zinatosha kabisa sasa garila nini
-
Watanzania kwenye swala la Saving tunaweza kuwa tunaongoza Duniani na si dhani kama kuna nchi nyingine ambayo wanachi wake wana poor Money managment kama sisi.

- Unaweza amka asubuhi kwenda kazini bila kuwa na plan ya kununua chocjote lakini utarudi na viatu kisa tu umekutana na Machinga akiuza viatu,
- Offa zakutafuta sifa
- Sifa za kumilika Gari, unakuta kuna staff Buss lakini mtu anaona bora aende na gari lake mwenyewe kuliko kupanda staff bus

So katika ile wealth Equation bado tunakazi sana
 
Ni kweli wadau yaani kama watu tunataka kuwa wafanyabiashara inabidi tubadilike uku kwenye ajira kuna kipato tu hatujui kinatoka wapi.

Kwenye biashara kipato ukitafute basi itabidi ujue kukitunza pia.

Nimebahatika kufanya kazi na wageni wengi na wamataifa tofauti Africa, America, Ulaya na hata Middle east, jamani wakati wenzetu wanalipwa vizuri sana na wanapension kubwa, mishahara yao wangeweza kutulipa hata sie staff 6 hivi wa juu lakini wapi kwenye matumizi...

Sie watanzanzia tunaongoza yaani hawa wengine hata from African countries watanunua kitu chochote kwa uangalifu sana na mara nyingi wanakataa tu...sisi kila kitu kiletwe office tumo, vya kukopesha tumo, cash tumo, lunch expensive... tena utashangaa wale wakipato cha chini ndo wateja wakubwa wa impulse buying kama anayosema Chasha.

Nadhani ujasiriamali uendane na ujuzi wa bajeti na savings, vinginevyo utaanza biashara ila na matumizi haya utaishia kufilisika bure. Ukiwaangalia matajiri wengi wana maisha simple sana ukilinganisha na wafanyakazi wasiojua 10 years later watakuwa wapi. Mwenye nondo za utunzaji mahesabu na bajeti watuletee hapa maana sie wengine scientist by nature
 
Mama Joe

Ni kweli kabisa, Nakumbuka Kuna Directa Mmoja hivi ni Mzungu wa Sjirika Moja la Kimataifa ambalo lina Oparate na huku Bongo, Huyu Jamaa Mshahara wake ukithaminisha na pesa ya Kibongo ni swa na Milioni 18 kwa mwezi, lakini cha ajabu Mchana anakula chakula kinacho pikwa na wapishi walio kuwa wanapikia staafu na wanauzia kwa Buku Mbili, hebu fikilia mtua mshahara wake ni milioni 18 ukijumlisha na alowance na kila kitu ni milini karibia 26 ila anakula msosi wa Buku Mbili, Hapo tungekuwa ni wabongo ni Bufe za kufa mtu huko Kitaa
 
Last edited by a moderator:
Mama Joe na Chasha, nimeipenda hii. Tunapaswa kubadilika ila naamini haya mabadiliko yatachuku muda kupatikana. Tayari mfumo wa maisha umesha waadhiri watanzania wengi. TUTASHINDA

Hii ni personer ishu kila mtu anao uwezo wa kubadilika, Na tatizo kubwa linalo tusumbua wabongo ni KUISHI WATU WANAVYO TAKA, Tunapenda sana maisha ya kuonekana, kusifiwa kwamba fulani kanunua gari kari sana, Fulani anamiliki usafili mkari mtaa mzima,

Watu weupe kwenye ishu Ya pesa wana nidhamu ya hali ya juu kabisa na hata wanavyo kuja kutalii huku si kwamba wana pesa sana bali ni nidhamu yao ndo inawafanya wawe na pesa nyingi sana za kuja huku,

Mzungu akienda Super Marketi anakuwa na List ya Vitu vya Kununua, na kila anacho nunua anatiki, na vikiisha anakula kona, Sasa njoo kwa Wabongo mtyu anaweza enda Supermarket kwa minajili ya kununua sukari ila atatoka na vitu vingine,

Wazungu kama hajaplan kununua kitu fulani na hata kama anakihitaji sana , kama hajapanga hawezi nunua hata ukimtembezea na kumuuzia kwa bei ya chini kabisa hata nunua, Sisi asubuhi tunaenda kazini lakini utashangaa jioni mtu anarudi na Nguo, kisa alikutana na watu wanatembeza akatamani.
 
Dah! mi huwa nachungulia 2 hili jukwaa,nakuwa busy na jukwaa la siasa!ila kwa uzi huu nashukuru sana mmenibadirisha mawazo yangu,nimejifunza mengi, kiukweli hasa nidham ya pesa na kubana matumizi yasiyo ya lazima!

Nasema asanteni sana...japokuwa nilikuwa nahangaika kusaka ajira mwaka wa 3 ss,lkn basi kutokana na jukwaa hili nimegundua nina uwezo wa kufanya kitu/bnes na nikaajiri watz wenzangu km kuna seriousness!
 

Ni kweli kabisa, Tatizo liko katika Udhubutu, hapo ndo watu wengi sana tunapo shindiwa, Kila mtu ana penda sana kuwa Mjasirimali, ila tatizo linakuja kwenye Kuchoma Meli Moto, inahitajika ujasiri wa ziada, Ila Kitu kmoja nilicho gundua ni kwamba Uoga wa kuingia katika Ujasiriamali ni sawa na Uoga tunao kuwa nao tunapo anza Paper, Ila ukisha piga paper kama mbili tatu hivi Uoga huisha, hata kwenye Ujasirimali ni hivyo tu, kuna time uoga huisha kabisa
 

Mkuu hapa umepiga PENTAGON!! Hii kitu asilimia 90% hawathubutu wanaendelea kuwa na FIKRA ya biashara bila ya kuifanyia kazi!!

UOGA nia adui mkubwa wa maendeleo ila watu hawalielewi hili!!!
 
Chasha wewe kaka/dada huwa nakukubali sana. Una mind set tulivu. Usichoke kutuelimisha wa tz wenzio

Aisee mimi ni Kaka, Ok, ni kweli tuko hapa kusaidiana, Ila kiukweli inatakiwa watu wabadilike, kusoma thread kama hizi nakuishia kusifia haisaidii chochote, unatakiwa kuchukua maamuzi magumu kabisa, mimi naamini watu waote wano pita/kuingiaknye hili jukwaa ni wale wenye nia au tiyari ni wajasirimali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…