Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Mkuu hapa umepiga PENTAGON!! Hii kitu asilimia 90% hawathubutu wanaendelea kuwa na FIKRA ya biashara bila ya kuifanyia kazi!!

UOGA nia adui mkubwa wa maendeleo ila watu hawalielewi hili!!!

Kwa msemo wa Lema uoga ni zambi mbaya sana, kila mtu utakaye kutana naye ana wazo la biashara sasa mwambie aaanze.

Mimi kwa kweli kwa sasa sina mpango wa kuajiriwa kamwe, nimefanya kazi miaka kama minne hakuna cha maana nilicho pata, so nishaamua kuchom meli moto na sitarudi nyuma pamoja na changamoto za kufa mtu ninazo kutana nazo, sitakua na U-TURN
 
Chashaa nafarijika sana maana mimi niliamua kujiripua nikaacha kazi so far naendelea vizuri na ujasiriamali ingawa sijaanza kupata faida but sijajutia uamuzi wangu hata kidogo, sasa kwa kusikiliza maneno ya watu kama nyie ya kutia moyo, not even the sky will be my limit. We kaka nimekupenda sana
 
Last edited by a moderator:

Vizuri sana, nafarijika kuona umeamua kuchoma meli moto, hakuna kisicho wezekana chini ya jua ukiwa na nia dhabiti,kikubwa ni kuto kata tamaa n usikubali hata siku moja kukatishwa tamaa na kwa walewenye muelekeo wa kukatisha tamaaa hata kama ni ndugu wapotezee mbali sana,

Ujasiriamali ni sawa na mbio za Marathoni, unazuguka uwanja mara 40 nainabakia mita 300 kumaliza mbio unaamua kujitoa,

Fikilia umetumia mudamwigi sana, pesa, kuanzisha project and then unakuja kusalimu amri baadae, inasikitisha sana, so wewe pambana kwa njia yoyote ile, jamii inaweza isikuewe kwa sasa, ila ipo siku watakuelewa hata kama ni baada ya miaka kadhaa,

Unapo lala ota biashara yako, ukiamka wakati wa kuswaki fikilia bishara yako,wakati wakati wa chai, waza biashara yako, mchana hivyo hivyo, wazungu wanasema kufall in love katika biashara, ushawahi sikia hii? so ipo hiyo ya kufall in love katika bishara yako

So dada optional uliyo nayo kwa sasa ni moja tu, only business, so uko kisiwani na umeachwa peke yako, so u need to fight kufa na kupona, na dont accept U-TURN,
 
Uko sawa mkuu! umenipa kitu, wacha namimi nijiripuwe.
 
Uko sawa mkuu! umenipa kitu, wacha namimi nijiripuwe.

Ya mkuu ni wewe tu, Watu engi uoga tulio nao uko ktika sehemu hizi

1. Kuchekwa
2. Kudharauliwa mtaani,
3. Kuhofia kama ukiflisika mpenzi wako unaye mpeda sana atakula kona,
4. Majirani wenzako watakupiku make ushazoea kushindana kimaisha hapo mtaani
5. Kuhofia kupoteza pesa zote
6. Kufofia lawama kutoka kw wazazi make ulishazoea kuwatoa na sasa hutakuwa unawatoa kwa wingi kama zamani,

7. Kuhofia kupoteza washikaji wa mtaa ambao mlikuwa mnabadili viwanja kila siku,

8. Kazini kwangu watanishaangaa sana na kuniona kama nimechanganyikiwa vile,

9. Nilikuwa napiga sana misere na gari la ofisi sasa itanibidi niwe na piga mguu au kupanda Toyo,

UKIYAZINGATIA HAYA HAKIKA, UJASIRIAMALI SI SEHEMU YAKO, NA HUTAWEZA KAMWE
 

Mkuu Chasha maneno yako yameshanikamata, ninapita kwenye kipindi cha mpito, nimeshakiona kisiwa na meli nimeshaipaki tayari! Nachoma moto meli mieeeeee !!!:

1. Kuchekwa: kwa akili yangu nikipiga mahesabu nimejiridhisha hii kitu nikiifanya vizuri natapiga hela kubwa kama ikitokea nikapiga mweleka atakaecheka na acheke salama, maana hata hivyo nitakuwa nimeshajifunza kitu ambacho anaenicheka hajui, na nikijinyanyua na kusimama tena baada ya mieleka kadhaa iko siku nitasimama imara na hapo wanichekao ndiyo watatafuta njia ya kupita kwa aibu na wivu! Na hili ndilo linalonitia nguvu zaidi badala ya kunitia hofu ya kuchekwa! Kama ni kuchekwa kwa ajili ya biashara ya mkaa afadhari nipate pesa kuliko kuendekeza ubishoo huku pesa ya kujirusha sina.

2. Kudharauliwa mtaani: acha wanidharau najua kudharauliwa ni jambo la muda mfupi tu, mimi natazama miaka mingi mbeleni, najua hii ni safari na ninaijua mimi mwenyewe, wao hawaijui, shida ninazopata mimi wao hawazijui na haziwahusu, nafuu yao ya maisha mimi hainihusu, siku nikifika safari yangu wao wale wale wataanza kusema tulipiga nae soga mtaani kwetu siku hizi anaringa!

3. Kuhofia kama ukiflisika mpenzi wako unaye mpeda sana atakula kona: Ndiyo ninalijua hilo kwamba mpenzi wangu kinachotuunganisha nae hivi sasa ni pesa tu, ni kweli kwamba nikifilisika atanikimbia, so sasa nachukua maamuzi magumu ya kuchoma meli moto! Maana nimeshaona kwa hali ya maisha inavyobadilika kama nisipichangamka leo kwa hali jinsi inavyokwenda huko mbeleni ni wazi atanikimbia tu, kama noma na iwe noma, nachoma meli sasa kama ni wa kunikimbia na anikimbie hivi sasa!

4. Majirani wenzako watakupiku make ushazoea kushindana kimaisha hapo mtaani: ni kweli tumekuwa na ka ushindani wa kuangusha vipati vya komonio na ubatizo wa watoto wetu, mavazi krisimasi na iddi na kukaangiza samaki SATO, ila sasa naamua kubadilika, maana kama nisipobadilika kila kitu kitaendelea hivi hivi maisha yangu yote, kama nataka kutajirika yapasa kubadilika ili nipate matokeo tofauti! Ushindani huo ninataka niuache na wao acha wajisikie washindi ingawa mambo yangu yakienda kulingana na vision yangu najua watakuja kunikubali tu na ingawa najua nitapitia mieleka kadhaa kabla sijasimama ila najua hii ni njia ambayo wengi waliofanikiwa walipitia!

5. Kuhofia kupoteza pesa zote: nitatumia akili na maarifa pia maana pamoja na kuwa ninakwenda kuwa mjasilia mali haimaanishi niingie kichwa kichwa tu. Ila hata kama nitapoteza pesa zote lakini nitakuwa nimebadilika ki-fikra na utajiri siyo kupata pesa tu bali kuwa na mwenendo unaovuta pesa (attracting wealth) kuwa na nidhamu ya pesa na kubadilika tabia kabisa niweze kuongea, kufikiri, na kutenda kama wanavyofanya matajiri! Nimeona matajiri wengi biashara zao zinaungua moto na kuteketea kabisa lakini punde wanasimama tena na kuja juu, ni kwa sababu utajiri wao umejichimbia ndani ya vichwa vyao, wao wanawaza tofauti, mipangilio ya mambo yao ni tofauti na sisi wapokea mishahara, yaani matajiri wanafanya mambo yao tofauti na kinyume ya kila jambo vile tunafanya sisi.

6. Kuhofia lawama kutoka kwa wazazi make ulishazoea kuwatoa na sasa hutakuwa unawatoa kwa wingi kama zamani: hawa wazazi wangu ndiyo kichocheo cha mimi kutafuta zaidi ili nisiwatoe kwa kuwapeleka out Coco beach pekee sasa nataka niwapeleke hadi Hawaii, kama niliweza huko nyuma ninajiamini nitaweza kwenda hatua kubwa zaidi! Itabidi wanivumilie tu.

7. Kuhofia kupoteza washikaji wa mtaa ambao mlikuwa mnabadili viwanja kila siku: ni kweli nimekuwa na washikaji ila hivi sasa nataka kubadili maisha yangu, washikaji kama ilivyo kwa mke wangu watakaonikimbia tutakutana mbele, nachoma meli!!

8. Kazini kwangu watanishaangaa sana na kuniona kama nimechanganyikiwa vile: kwa kweli nakubali kila mtu kazini hatanielewa, kila mtu atacheka kwa vile mshahara wangu kwa sasa umeshakuwa mkubwa sana, nimechoka kupimiwa pesa kwenye kijiko, nimeshapiga mahesabu pesa ninayolipwa kwa sasa ni kidogo sana ukilinganisha na ninachokiona mbele ya safari! Ninajiamini ninaweza kusimama na ninajua nitapata kipato kikubwa sana kuliko hiki cha sasa!! Ninakwenda kufanya jambo ambalo ndiyo fani yangu na nitahama na wateja na utaalamu na uzoefu niuhamishie kwenye ishu zangu. Kwa vile wao hawaelewi ninachokiona acha waendelee kunishangaa na kunicheka!! Ninajiamini kuwa mimi sifikiri kama wao ninachokiona mimi wao hawakioni!! Inawezekana wameridhika na wanachokipata acha wacheke tu.

9. Nilikuwa napiga sana misere na gari la ofisi sasa itanibidi niwe na piga mguu au kupanda Toyo: Yees ni kweli gari la ofisi lilinipa tafu na umaarufu sana. Ila gari la ofisi kwa sasa linanikera sana, nimeona wakubwa wangu wa kazi wanastaafu hawana gari shauri ya kubweteka na vya kazini. Gari la ofisi linaniletea kelele sana na majungu mengi! Siwezi kujivunia gari la ofisi, likionekana bar napigwa majungu, nikibebea majani ya ng'ombe inakuwa kesi, nisipompa mtu lift inakuwa masimango, gari la ofisi si la kujivunia!! Sasa hilo gari ndiyo imekuwa Fimbo ya kunitishia, oh tumekupa gari tunataka uchape kazi ukiwa mzembe tutampa mwingine, ooh toka tukupe gari siku hizi hutulii, ohh tumekupa nyumba ukizembea tutakunyang'anya looooh!!! Changu ni changu nitanunua tu, nachoma moto meli mie.......
 
Mkuu safi sana, hizo ndo sababu kuu za kwa nini watu hawataki kujiingiz kwenye ajira binafisi, mimi mwenye nilikuwa hivyo ila nisha sahau siku nyingi sana ishu za kuajiriwa, kwa sasa naweza jipangia ratiba yangu bila shida, yoyote ile,

Ni kweli kabisa kuna changamoto kibao kwenye swala zima la kujiajiri ila sio sababu ya kukimbia
 
Ya kinacho takiwa ni watu kuchoma Meli moto, Watu wengi wa subili mpaka Cotact z kazi ziishe, wapunguzwe, au wafukuzwe kazi ndo waanze kukurupuka na biashara, Unatakiwa kuanza sasa, na wala si kesho.
 


Ngoja niongezee kidogo,kwa sisi wanaume hela nyingi pia huenda kwenye POMBE na MABIBI,Mtu akishinda kwenye maeneo haya kwa maana ya kuacha kabisa au kupunguza basi ataokoa fedha nyingi sana!! Tamaa zetu za Ngono na wanawake tofautitofauti huzikondesha sana waleti zetu mpaka hufikia mahali hupata Kwashiorkor,yaai kwa maneno mengine Umalaya aghali na hatari!!!!:hatari:
 

Ya mkuu this is true kabisa.
 
Ndg yangu CHASHA FARMING

Ninachoweza kusema ni MUNGU AKUBARIKI sana.Umeonesha ni jinsi gani usivyo mchoyo na mbinafsi lakini badala yake umekuwa ume share what you know to the public,kiukweli nakupongeza sana.Nadhani umeleta jambo ambalo ni la msaada kwa watu wengi nikiwamo mimi.

Nimesoma michango ya wenzangu na wengi wameonesha kuwa na woga na namna ya kupata mitaji.Ninachoweza kusema ni kwamba kukosa mitaji inaweza kuwa kikomo cha fikra zetu kwani Maandiko katika Biblia yanasema PESA HUFUATA MAONO, that is to say unapokuwa na wazo ambalo lipo sawa basi uwe na uhakika pesa italifuata wazo hilo.Nawatia moyo wote wanaopenda kuanzihsa biashara wasikatishwe tamaa na swala la pesa,pesa zitakuja immmediately baada ya wewe kuwa na wazo.

Ni kweli inawezekana kuwa zipo njia zaidi ya hizi ulizozitaja lakini umeonesha njia na sisi wengine ambao tunao uwezo wa kuleta nyongeza basi fursa ipo na tututmie nafasi hii kuyaleta mbele ya wengine kwaajili ya kubadilisha kizazi chetu haswa katika eneo la kiuchumi.

Naomba kuwasilisha
 

Mkuu pamoja sana,
 
Hivi Kina Bill gates, Nwanko kanu,(mcheza mpira) David Beckham, mwanzilishi wa Facebook, walianza na mitaji ya shs Ngapi Jamani. Mi navyojua walikuwa Na mawazo, wakayafanyia Kazi Sasa ona walipo.

Kuna kinamama kinakaka Wengi tu wameanza Na Tshs chini ya laki, unashangaa baada ya miaka miwili anao wa Zaidi ya milioni, Kuna wanaoamua kubadili biashara, Kuna wanaoamua kuanzisha biashara ya pili.

Nnachojaribu kuelezea ni ulimbukeni wa watu wenye vielim vya kawaida kabisa eti kuchagua kazi ama biashara, unashangaa kabisa Eti undergraduate anajigamba kabisa ye hawezi kufanya kazi flan kisa inamlipa laki tatu Kwa mwezi, badala afikirie jinsi gani baada ya miaka miwili atakuwa amehifadhi Akiba ya kuweza kumfanya apate wazo la biashara ye anafikiri zilivyo ndogo, na jinsi atakavyoshindwa kuhonga na kupiga laga Kila siku Jioni.

Mtaji wa maskini ni nguvu zake Na mtaji wa aliyeenda shule ni akili yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…