Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)

Tunashukuru ila shida inakujaga pale kwenye CAPITAL tuuuu...
Komaa Mkuu...., hiyo dalili ya kushindwa
 
Mkuu ni kweli kabisa, Hoby na Skills uliyo nayo ndo Idea zako za kwanza kabisa, Na huwa inasikitisha sana kukuta mtu amesomea syansi ya wanyama, na baadae unmkuta anauza bidhaa za jumla,

Mara nyingi sehemu ya kwanza ya kupata Experiens ya Business ni kazini kwako kwa walio ajiliwa na hii ni kutokana na ukweli kwamba wengi wanao acha kazi hufanya biashara zinazo fanana na kazi walizo kuwa wakifanya, Kama Ilikuwa Mpishi wa Hoteli fulani tunategemea ufungue mgahawa wa Chakula, na kama ulikuwa umeajiriwa kama mchomeraji wa Vyuma tunatarajia uanzishe ofisi yako ya Kuchomerea,

Na je kama ulikuwa umeajiriwa ualimu msingi, unaweza kujiajiri kwa kufanya kitu gani inayoendana na fani hii.
 
Na je kama ulikuwa umeajiriwa ualimu msingi, unaweza kujiajiri kwa kufanya kitu gani inayoendana na fani hii.

Vya kufanya viko vingi mkuu ni wewe tu kaungalia mazingira yako uliko, Yule Muguku wa Kenya sasa Marehemu alikuwa ni mwalimu lakini aliacha na akaingia kwenye ufugaji wa kuku na mapaka anafariki 2010 alikuwa ni Bilionare namba 5 nchini Kenya,
 
BUSIMINET COMPANY LIMITED
Po.box 12659
Kinondoni-Dar es salaam

Tanzania
Mob: 07 65 90 10 93 / 06 58 12 31 58
E-mail: busiminet@gmail.com
Website: busiminet.blogspot.com
OUR SERVICES: Tax, Business, IT, Accounting &Bookkeeping and Other services
TAX
1.Assist in preparation and submission of Returns to TRA
2.
Assist in estimation and determination of tax liabilities.
3.Online Returns submission and Payment Registration with TRA.
4.
Assist in Tax Payment processing.
5.Reminding about due dates for Tax payment and Other Tax/Statutory compliance.
6.
Tax health-checks
7.
Processing transfer or change of ownership with TRA
8.
Assist in filing and submission of TRA forms.
9.
Assist in Applications for Requesting Tax exemption.
10.
Tax consultation and advisory.
BUSINESS

1.
Assist in business licenses registration with municipals, ministries and other Government bodies.
2. Assist in business name, NGO’s, Succoss and Company registration with BRELA.
3.
Preparation of Business Proposal, Constitution, Memorandum, Article of Association and Company Profile

4.Preparation of business plans
5.
Business Restructuring
6.Loan processing
7
.
Business consultations
8.
Preparation of Research proposals

IT AND RELATED SERVICES
GRAPHIC DESIGN
1.
Logo,Bill boards, Posters.
2.
Business cards, Identity cards (ID).
3.
Brochures Flyers, Invitation cards.
4.
Calendar,Product label Magazines
5.
Photo Editing and Retouching Special Envelope, Movie covers
6.
Website, Blogs and Systemdesign and development
7.
Computer maintenance
8.
Computer software installation
9.
Network designing and installation
10.CCTV installation
11.
AC installation and maintenance

ACCOUNTING AND BOOK-KEEPING SERVICES
1.Stock counting
2.
Preparation of bank reconciliations
3.
Preparation of annual financial statements complying with International Financial Reporting Standards.

4.Posting of financial transactions from source documents , (IFRS).
5.
Preparation of budgets and management reports.
6.
Payroll services (preparation of the payroll including pay slips)
7.
How to keep books of account

OTHER SERVICES
1.
Mining
2.
Marketing and advertisement
3.
Education
4.
Agricultural activities
5.
Gas activities
6.
Cargo clearing
7.
Legal consultancy
8.
Staff recruitment & Out-Sourcing
9.
Project management and analysis
10. Training and workshops to Enterpreneurs, scholars and other groups that need to excel in their business


Business in the smooth environment ensures growth


okoa muda,okoa pesa na kuza biashara yako kwakuhudumiwa na Busiminet co.ltd

 
Nice thread people can got something that will change their norms life.
 
Wakuu bora mtu wazo kuliko hela. Binafsi nilipokuwa nasoma niliamni cku nikiajiriwa basi shida kwaheli.chakushangaza ziliongeka maradufu. Baada ya mda mrefu sana maisha yalizidi kuwa magumu maraodufu.siku moja nkaamua kuwa mjasilia mali nilianza nilikuwa na laki moja ikabidi nikope na hela kidogo kwa mdogo wangu ambae nilimsomesha mwenyewe ila yy alikuwa tayari kawa mjasilia mali japo m
Kidogo.

Nilianza kuuza vifaa vidogovido kama flash, badae nikajifunza na kurepair could comp,baadae ikaanza kunisumbua ilipotakiwa mitoe ushauri wa kitaalamu kwakuwa mwanzo nilijifunza kijanja tuu.kutokana na hilo ikabidi nisome diploma ya IT.na nimeunganisha na degree kabisa ya INFORMATICS kabisa hapa SUA ili nitoe huduma bora zaidi kwa wateja wangu.

Nashukuru mungu mpaka sasa ninaweza kujisomesha taaluma yenye mlengo wa ujasiliamali wangu,naendesha familia na biashara yangu ina mtaji wa mlioni 14.na hapo imeathirika kidogo na pirika zangu za shule ila sio mbaya inaendelea. Ninachosisitiza ni idea uthubutu.tatizo la wasomi ni tunafungwa na hali ya watanionaje?

Angalizo: Si kwamba mpaka naweza fanya yote haya nimejikita kwenye shughuli moja tuu, ila baada ya kamtaji kukua kidogo ikabidi nianze kuwekeza hata kwenye maeneo mengine kama kilimo.juzi hapa nimetoka kuvuna matikiti yangu kufika soko wanunuzi wakaanza kuleta za kuleta ikabidi nikomae mwenyewe kuyachuuza mpaka yakaisha gari zima.kwahiyo wakuyatetea
Maisha yetu ni sisi wenyewe. kama utajifunza kitu kitu basi ni jambo jema.
 
Hahaha, of course hii ndo elimu inayoweza kumbadilisha mtu. Siyo ile elimu ambaayo iko colonial based,unameza madesa mengi, ukinda ktk labour market ni shida. Elimu haimsaidiui kijana kuleta mabadiliko ktk jamii yake. Yaani si siasa tu. Walau mawazo yanabadilika kwa kusoma threads like these.
 
IDEA ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo lenye tija kwako na kwa jamii nzima,

HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA

1. TUMIA UJUZI ULIO NAO
Ujuzi ulionao ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji yako?

Ujuzi ulianao ndo hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe


2. BADILISHA HOBBY YAKO KUWA PESA

Hobby ni moja ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?

Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening

3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYARI IPO
Ukishindwa kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali so unaweza nunua nu kuendelea nayo

4. Kununua Franchise
Hii ni moja ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA MENGINE

Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa,
Na ilisha wahi kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado wanalitumia

5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kazalika

6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo enda kustarehe
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?

7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.

8. TUMIA TEKNOLOJIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza kukuongoza kuja na wazo la Biashara

9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI NYINGINE WANAHITAJI NINI
Unaweza tumia uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama Viwanda Migodi na kazalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa wanahitaji kwa wingi

10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza


11. ANGALIA HABARI NA MAKALA MBALIMBALI
Kuna chaneli huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa ina makala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la biashara

12. COPY BUSINESS IDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copy idea kutoka hata India, China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika


13. TUMIA NJIZA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA biashara- maonyesho ya biashara
-Magazeti,
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
-Kwa marafiki


14. UNAWEZA GUNDUA KITU?
Unaweza ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikio kwako


SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUPATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA

Mkuu naomba unitumie hii post katika email yangu ya kinondoniilala@gmail.com natanguliza shukrani...!
 
Kweli mtaji sio tatizo,kama idea ipo excellent basi mtaji utapatikana with no doubt.Kuna sekta mbalimbali zinazosaidia watu kuboresha innovative ideas.kwa mfano:-DTBi(Dar Teknohama Business incubators-for technological ideas).From then idea yako ikishakamilika unaweza kui present kwa investors,sometimes hata kama haijakamilika kunakuwaga na workshops ambazo zinakaribisha investors wavutiwe na concept yako.(Hizi ni baadhi ya huduma zinazotolewa:-
  • Business Planning Capacity Building and Support
  • Establishment of the company
  • Support towards concept pilot testing
  • Mentoring and Coaching
  • Development of revenue model and financial projections
  • Linkage to potential markets
  • Exposure to expert talks, training and marketing events
  • Evaluation for transition into the next stage
  • In some cases, access to seed capital (finance/grants).
  • The startup incubatees can be resident or non- resident (virtual).
  • Access to high speed internet.
  • Networking events.
  • Exhibitions, workshops and hackerthons.
Watu wana pesa kibao sema wanasubiria yule mtu mwenye excellent idea ili pesa yao isipotee bure.Mi ningeshauri watu wajijenge sana,someni vitu mbalimbali,tembeleeni sehemu tofauti mbadilishe mandhari,pia ni vizuri kuwa open to new business ideas.Pia watu wengi wanaofanikiwa kwenye maisha ni watu wanaothubutu kufanya vitu ambavyo sio watu wengi wangefikiria kufanya.Mimi ni mfanyabiashara na nimezungukwa na wafanyabiashara wakubwa ambao kati yao kuna wanaotengeneza atleast 40million profit on monthly basis.I'm learning from them na kama unapenda nikuunganishe nao ili ujifunze kutengeneza pesa kwa akili kupitia mifano hai,just check on me.Nisingependa kufaidi mwenyewe wakati wengine wanateseka.Kumbuka:-
"Ukitaka kufanikiwa,kaa na watu waliofanikiwa."
C
heck me through this number:-
0659143784
Can I Pm you for serious talks pliz???
 
Unataka nilie au? maana naona kama mnanisema mimi tu humu. Kubana matumizi kwangu mtihani lakini nimewasoma, nitajitahidi. Ni leo tu nimetoka kupokea kodi ya "fremu" - nimei-sublet baada ya biashara kunishinda. Nimefanya biashara miaka 3, hivi karibuni imeyumba weee mpaka nikaanza kutumia mshahara kuiendesha. Nikafika mahali nikaona isiwe tabu - hela iliyokuwa imebaki nimepeleka benki lakini niulize basi nataka kuifanyia nini sijui!!!! Ngoja nitulie kidogo kisha nitawa-pm mnisaidie. Mbarikiwe.

Dada don't ever give up. Press on. Umekaribia kutoboza ngangana utashinda. By Riltz in Pm nitakuelewesha Zaidi.
 
Ningependa kufahamu zaidi kwani ninawazo la kuanzisha biashara ambayo nimejaribu kuchunguza nikaona ina mafanikio lakini tatizo lipo kwenye mtaji kwani ninaishi maisha ya chini sana. Ahsante sana
 
Mitaa mingine noma kwa kamati za ufundi, mfano huku kwetu nilifungua biashara ya duka lakini ilibidi nilifunge. Utakuta kwa wiki pesa zinapotea kimiujiza hasa elfu kumi kumi. Unauza kisha nazitenga elfu kumi peke yake kwa sababu siyo chenji. Lakini nikija kucheki baadaye nakuta hazimo wakati full time nakuwemo mimi mwenyewe dukani! Nilinyoosha mikono kwani sikutaka kuanza kumtafuta mbaya wangu labda ningeua mtu ningemtambua.

Hao wanaitwa 'chuma ulete' hata kwenye makanisa wanaingia kupiga sadaka sembuse bness ya mtu WA kawaida!!
Km in Mkristo.

Hiyo bness yako unapoanza uliikabidhi kwa Mungu?!fungu la kumi je?ulikuwa unatoa?!
Manaake km hutoi church unatoa upande WA pili ndo kanuni. ni mawili either kwa Mungu o kwa shetani!!
 
Kuanza ujasiriamali si swala la kuwa na mtaji mkubwa,bali utayari au udhubutu wa mtu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom