Wakuu bora mtu wazo kuliko hela. Binafsi nilipokuwa nasoma niliamni cku nikiajiriwa basi shida kwaheli.chakushangaza ziliongeka maradufu. Baada ya mda mrefu sana maisha yalizidi kuwa magumu maraodufu.siku moja nkaamua kuwa mjasilia mali nilianza nilikuwa na laki moja ikabidi nikope na hela kidogo kwa mdogo wangu ambae nilimsomesha mwenyewe ila yy alikuwa tayari kawa mjasilia mali japo m
Kidogo.
Nilianza kuuza vifaa vidogovido kama flash,badae nikajifunza na kurepair could comp,baadae ikaanza kunisumbua ilipotakiwa mitoe ushauri wa kitaalamu kwakuwa mwanzo nilijifunza kijanja tuu.kutokana na hilo ikabidi nisome diploma ya IT.na nimeunganisha na degree kabisa ya INFORMATICS kabisa hapa SUA ili nitoe huduma bora zaidi kwa wateja wangu.nashukuru mungu mpaka sasa ninaweza kujisomesha taaluma yenye mlengo wa ujasiliamali wangu,naendesha familia na biashara yangu ina mtaji wa mlioni 14.na hapo imeathirika kidogo na pirika zangu za shule ila sio mbaya inaendelea. Ninachosisitiza ni idea uthubutu.tatizo la wasomi ni tunafungwa na hali ya watanionaje?
Angalizo: Si kwamba mpaka naweza fanya yote haya nimejikita kwenye shughuli moja tuu,ila baada ya kamtaji kukua kidogo ikabidi nianze kuwekeza hata kwenye maeneo mengine kama kilimo.juzi hapa nimetoka kuvuna matikiti yangu kufika soko wanunuzi wakaanza kuleta za kuleta ikabidi nikomae mwenyewe kuyachuuza mpaka yakaisha gari zima.kwahiyo wakuyatetea
Maisha yetu ni sisi wenyewe.kama utajifunza kitu kitu basi ni jambo jema.