KERO Baadhi ya Taasisi za Serikali hazilipi tena pesa ya likizo kwa watumishi wake

KERO Baadhi ya Taasisi za Serikali hazilipi tena pesa ya likizo kwa watumishi wake

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Heshima yenu wakuu ,

Rejea kichwa cha habari hapo ,kuna hili jambo limekua sana kwa sasa ,tangu baadhi ya Taasisi kupokea barua ya kufutwa kwa pesa ya likizo maarufu kama mshahara wa 13 kwa mwaka ..Basi na pesa ya nauli ya likizo hawalipi tena .

Kulingana na mwongozo wa serikali ni lazima mtumishi alipwe pesa ya likizo ,kwa nn baadhi wanadai tangu mwaka jana na mwaka huu ulioanza julai, kwamba hakuna allocation za pesa ya likizo kama nauli ,zaidi unapewa tu ruhusu ya kwenda ...Kwenye mfumo wa Ess ,tunajaza kila kitu ,pamoja na tunapotoka na kwenda .


Kimahesabu pale nauli inakuja automatically ila haupati hata shilingi mia ,kwa mwaka jana hatujapata na mwaka huu tulioanza likizo pia hatujapata ...Jamani tunaomba kujua hizi sheria ni maneno tu au lah..Hakuja utekelezaji na tutaenda kudai wapi?

Kama serikali imefuta zile posho za awali ,mtu alikuwa anapewa mshahara wa mwezi mmoja ,ila mbona hata nauli mmefuta kabisa ...Na kama zipo mbona hatulipwi na hizi Taasisi ,huku safari za wakuu zipo kama kawaida ila pesa za nauli hatupati.
 
Mara mwaka huu wanalipa mwaka ujao hawalipi
 
Bongo kila kitu ni magumashi tu.

Kwa sababu ya ujinga wa watanzania na uchawa wa kusifia upumbavu wa viongozi ni haki yenu kunyonywa.

Mtaendelea kunyonywa hadi mpate akili ya kufurusha hao vijwangaibaka mnaowaita viongozi wenu.
 
Back
Top Bottom