Baadhi ya Viongozi waliokufa vifo tata

Baadhi ya Viongozi waliokufa vifo tata

Kifo cha raisi jpmagu kilinifikirisha sana, kwanza kabisa hakuna alie amini kama jpm katuacha sio wabaya wake wala sio wapenzi wake, ilikua patashika sana

Kifo cha membe japo sijawahi kua shabiki yake ila nacho kina nadharia tata mbili tatu
 
Lissu ilibaki nukta apitishwe hivi. Ben saane, japo hakuwa wa sirikali ya ccm lakini duniani hayupo na mbinguni hajaoneka. Azory gwanda hakuwa kiongozi lakini hajulikani alipo mpaka kesho. JIWE LINAUNGUZWA SANA SAA HII.
Usicjokijua ni kuwa, wakati wa JPM, kuna mjanja mmoja aliendesha vitendo viovu ili kumchafua JPM.

Ndiyo maana JPM alisema msitufanye watanzania wajinga kiasi hiki. Ni kufuatia kutekwa kwa MO, aligundua mchezo mzima aliokuwa akichezewa.
 
1. Dr. Omary Ali Juma
Huyu alikuwa ni Makamu wa Rais katika Serikali ya Rais Benjamin Mkapa. Alienda kufungua maonyeshi ya sabasaba akiwa na Rais Kabila wa Kongo, kesho yake tukapata tanzia.

2. Benjamin Mkapa
Rais wa awamu ya tatu, jioni moja ya mwezi july mwaka 2020 ikiwa imebaki miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 tulitangaziwa kifo chake cha kushtusha. Maswali yakawa mengi

3. Edward Sokoine
Waziri Mkuu mzalendo pengine kuwahi kutokea. Alifariki katika ajali ya gari huko Dumila. Mpaka leo watu wanajiuliza gari ya Dumisan Dube iliwezaje kuifikia gari ya Sokoine?

4. Horace Kolimba
Alikuwa ni katibu mkuu wa ccm, akateleza kwakusema ccm imepoteza dira. Akaitwa Kizota Dodoma kujieleza mbele ya CC ya CCM baada ya kumalizia kuongea akadondoka na kufariki dunia.

5. Mchungaji Christopher Mtikila
Mwenyekiti wa chama cha DP, zikiwa zimebaki siki chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 alipata ajali huku mkanda wake ukikutwa shingoni mwake.

Itaendeleaaaa....
John Kijazi, Mahiga
 
Usicjokijua ni kuwa, wakati wa JPM, kuna mjanja mmoja aliendesha vitendo viovu ili kumchafua JPM.

Ndiyo maana JPM alisema msitufanye watanzania wajinga kiasi hiki. Ni kufuatia kutekwa kwa MO, aligundua mchezo mzima aliokuwa akichezewa.
Yaani magufuli ajue mtu katekwa na mbaya wake akae kimya? Wewe utakuwa ulimjua ukiwa mkubwa ? Unakumbuka alichokisema kuhusu kisiju? Nn kilimtokea gwanda? Au unafikiri sisi tunaishi ulaya?
Peekaboo propaganda zako usukumani huko
 
Back
Top Bottom