Baadhi ya Viongozi waliokufa vifo tata

Baadhi ya Viongozi waliokufa vifo tata

Wewe kama unaenda kanisani au msikitini usiende maana huna imani? Mungu kuchukua kiumbe chake alichoumba mwenyewe wewe unaweweseka? Hujawahi kufiwa wewe? Tuseme hata ndugu zako waliofariki nao kuna watu wamewaua?
Mtaacha lini mambo ya kuzushia watu uongo kwa manufaa ya kikabila, dini na siasa za kikanda.?
Kifo cha membe na magufuli ni vifo kama vingine tu wewe hivyo vitisho kwa wengine walio hai unavitoa wapi?
Mbona hata nyerere na sokoine waliofanya makubwa walikufa? Nani aliwaua?
Kumbe hata John Kennedy Rais wa Marekani alijiuwawa eti .... KARUME, Gandhi, si ndio unachokisema hapa...ficha ujinga huo ...vipo vifo vya kuamini matendo ya Mungu na vipo vifo binadamu wanawatanguliza wenzao...Lumumba!!
 
1. Dr. Omary Ali Juma
Huyu alikuwa ni Makamu wa Rais katika Serikali ya Rais Benjamin Mkapa. Alienda kufungua maonyeshi ya sabasaba akiwa na Rais Kabila wa Kongo, kesho yake tukapata tanzia.

2. Benjamin Mkapa
Rais wa awamu ya tatu, jioni moja ya mwezi july mwaka 2020 ikiwa imebaki miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 tulitangaziwa kifo chake cha kushtusha. Maswali yakawa mengi

3. Edward Sokoine
Waziri Mkuu mzalendo pengine kuwahi kutokea. Alifariki katika ajali ya gari huko Dumila. Mpaka leo watu wanajiuliza gari ya Dumisan Dube iliwezaje kuifikia gari ya Sokoine?

4. Horace Kolimba
Alikuwa ni katibu mkuu wa ccm, akateleza kwakusema ccm imepoteza dira. Akaitwa Kizota Dodoma kujieleza mbele ya CC ya CCM baada ya kumalizia kuongea akadondoka na kufariki dunia.

5. Mchungaji Christopher Mtikila
Mwenyekiti wa chama cha DP, zikiwa zimebaki siki chache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 alipata ajali huku mkanda wake ukikutwa shingoni mwake.

Itaendeleaaaa....
Namba moja nasikia aliji overdose viagra
 
Back
Top Bottom