Ni kweli kabisa. Mwalimu alijitahidi sana.. hata kama viwanda alivyopewa/uziwa vilikuwa tayari vimepitwa na wakati. Laiti kama Mwalimu angelijuwa kuwa alikuwa anaongoza watu wa aina gani, angeamua tu kula bata kama Mobutu
Mosi.. watz wa nyakati zile, kama walivyo wa sasa hawakuwa watu wa kupiga kazi.. walijaa uvivu tuuu, kulalamika na uzembe. Ili viwanda visonge mbele na kuzalisha faida, ilitakiwa mali ghafi. Katika sekta ya uzalishaji mali ghafi, mambo yaliharibika pindi mkoloni alipoondoka hususa baada ya Azimio la Arusha, 1967. Watz wakiwa na jembe la mkono huko mashambani na wengine wakiwa na elimu duni katika masuala mazima ya uchumi ea viwanda, hakuna cha maana ambacho kingefanýika. Ni uvivu kwa kwenda mbelee..
Baadaye ghafla chama kikashika hatam.. balaa la uharibifu likapanuka.. meneja wa kiwana cha Bucop anapewa amri ya kutoa milioni 30 kugharamia safari ya Kawawa mkoani Kagera, bila vielelezo wala nyaraka stahiki.. naye meneja anajiongezea zake milioni 5.. na kila mahala ilikuwa hivyo..
Kwa muktadha huo, uongozi wa wakati ule unapswa kulaumiwa sehemu kwa kushindwa kufuata miiko ya kiviwanda..
Ikawaje Waasia na waarabu wakavigeuza magodown? Ni uozo tu katika nchi.. Mh Ben (RIP) anarithi mahame/mapango wananchi waliopigika kisawa sawa.. wenye kaunafuu ni wahindi kwa vile wana uwezo wa kupata vijimikopo kutoka India.. ndo ikawa hivyo..
Kazi sana kuendeleza nchi ambako watu wake hawapendi kazi.. wanapenda kula kuliko kazi..