Baadhi ya vyuo vya Ualimu vifutwe na kurekebishwa kuwa vya Kilimo na Ufundi Stadi ili kuendana na soko la ajira

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2019
Posts
9,863
Reaction score
20,806
Ajira mpya za walimu kama 9,800 zimetangazwa nchini hapo jana lakini idadi ya walimu wasio na ajira ni kubwa Sana mtaani kuna haja ya Serikali kufikiria upya kuhusu kuendelea na kufundishwa kozi kozi za ualimu nchini kwani hazina tija tena KWA taifa letu kwa sasa.

Ukijaribu kuchukua idadi ya Wahitimu wa ualimu kwa takriban miaka mitano hivi utagundua sekta ya ajira imezidiwa na wahitimu wa kozi hiyo hata kama wakiajiriwa Ili kukidhi mahitaji ya shule na vyuo bado Walimu watabaki mitaani wengi Sana na kozi za ualimu hazina ujuzi wa kujiajiri ZAIDI ya kusubiri kuajiriwa au kujiajiri KWA KAZI ambayo Mwalimu hajaisomea

Wizara ya Elimu badilisheni vyuo hivi kuwa vyuo VYA kilimo na mifugo Ili vijana wawe na uwezo wakujiajiri watokapo vyuoni kwani kilimo na mifugo ni ajira tosha kabisa kuliko ualimu hata ufundi mbalimbali itasaidia vijana watokapo vyuoni kujiajiri KWA KUTUMIA taaluma walizozisomea

Tupunguze wahitimu wasio na uwezo wa kujiajiri mitaani KWA kuanzisha kozi nyingi zinazokidhi vigezo VYA kujiajiri.

Kozi zisizo na uwezo wa kumsaidia kijana kujiajiri ni kikwazo KWA maendeleo ya uchumi wetu.

Wizara husika itazame upya aina ya vyuo na kozi zinazofundishwa kama zinaenda a na soko la ajira nchini.

Asanteni kwa kusoma.
 
Shule nyingi hasa kule vijijini hazina walimu. Walimu huwa wanastaafu, wanapata magonjwa na wengine kufarki. Sekta ya Elimu na Afya ni waajiri wakuu kwenye factional society. Ukiona ajira za sekta hizi zina dorora ni dalili ya kuwa unaishi kwenye dysfunctional society.
 
Hata kama wakiajiriwa kukidhi mahitaji BADO watabaki wengi mno mtaani!!KWA miaka mitano iliyopita graduates wanaweza fika hata laki sita wa ualimu nchini!!!
 
... sekta ya kilimo inahitaji mkakati wa kipekee kweli kweli. Ni aibu taifa leo linaagiza ngano, sukari, na mafuta ya kula. Serikali iwekeze kwenye mashamba makubwa yaliyotelekezwa miaka na miaka; vifaa vya kisasa vipelekwe huko; wataalamu waajiriwe huko plan iwe miaka mitano ijayo marufuku kuagiza ngano; miaka 8 marufuku kuagiza mafuta ya kula; miaka 10 marufuku kuagiza sukari badala yake tuwe tuna export.

Tutakuwa tumeokoa mabilioni ya dola yanayotumika kuagiza vyakula hivyo; tutakuwa tumetengeneza ajira kwa watu wetu; tutakuwa tunapata fedha za kigeni kwa kuuza nje. Uwezo wa rocket science hatuna basi hata kujitosheleza kwa ngano? Aibu!
 
Na hicho kiiingereza cha kayumba cha which which ni hatari can we compete!!!?
Hii nchi ina walimu wasomi, wapo watu wanasoma hiyo lugha ya malkia kama vile wanaosoma linguistic, wao wanaweza kuwa competent sana,wapo walim wa fani mbalimbali na wameiva . Ninachoona mimi tatizo lipo kwenye wizara husika.Kumbuka kama mwalimu wa kemia, biolojia n.k anaweza kuzalisha pilot, daktari n.k basi anaweza kuishi nchi eyote ile.
 
Na benk ya kilimo inatoa mikopo kwa mkulima mwenye heka si chini ya 100 ivi hii benk ipo kwa lengo gani hasa?
 
utaratibu uliharibika 2015 ajira zilipositishwa, sijui Tamisemi walikuwa wanawaza nini.

walivyolundika watu mtaani miaka 6 hawataweza kuwaajiri tena. sio waalimu tu hata waliosomea afya wanahaha.
 
Ukifanya hivi mkuu,nikuzuri Sana Ila watakupinga nakukuita dikteta nakuanzia kupata upinzani kama alioupata mwendazake , mabadiriko hayajawahi Kua rahisi kiasi hicho tena kwakuchekeana kama ilivyo Leo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…