Pre GE2025 Baadhi ya Wajumbe Mkutano Mkuu CHADEMA wamkataa Tundu Lissu

Pre GE2025 Baadhi ya Wajumbe Mkutano Mkuu CHADEMA wamkataa Tundu Lissu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yericko Nyerere...Lissu ni msaliti!
Retired...Lissu ni mropokaji!
Molemo...Lissu ni mkurupukaji!
sinza pazuri...Lissu ni muongo!
Quinine...Lissu ni mvurugaji!

Ndugu zangu, really? Mbona hizi ndizo sifa zile zile alizopewa Mh. Tundu Antiphas Lissu kabla ya kumiminiwa risasi na wabaya wake mwaka 2017? Hebu tujikumbushe kidogo kauli ya mmoja wenu Lissu alipogombea urais mwaka 2017?

View attachment 3195688
Yericko Nyerere, kwa nini, kwa mfano, nisiziamini tetesi kwamba hapa pesa, sabuni ya roho, iko kazini?
Wakumbushe waeleza sera za Mbowe
 
Tundu Lissu mwanaharakati na mtetezi mkubwa wa haki za binadamu anapambana kukalia kiti cha Mwenyekiti Chadema Taifa

Molemo Media imefanya utafiti maeneo mbalimbali nchini kwa wajumbe wa mkutano mkuu kutaka kufahamu mwelekeo na mtazamo wao kuelekea mkutano Mkuu wa uchaguzi Januari 21

Tundu Lissu mwenye msimamo mkali wa kisiasa anajadiliwa na watu mbalimbali hasa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uamuzi wake wa kupambana na Freeman Mbowe Mwenyekiti aliyekalia kiti hicho kwa miaka 20

Katika mahojiano na uchunguzi huo Molemo Media imeona uwezekano mkubwa wa Tundu Lissu kushindwa nafasi hiyo kutokana na hoja kadhaa za wajumbe kama ifuatavyo.

1. Wajumbe wengi wameonyesha hofu ya kumchagua Tundu Lissu kutokana na jinsi anavyoongea maneno mengi bila kujitafakaru kwanza ni kipi cha kuzungumza na wakati gani wa kuzungumza.Wanasema kiongozi anapaswa kuwa msikilizaji zaidi na mzungumzaji kwa uchache.

2. Tundu Lissu amelalamikiwa kutokutunza siri za Kamati Kuu na chama, kuna mambo ambayo hayapaswi kuwekwa hadharani mfano uliotolewa ni jinsi alivyolipuka kuzungumzia kikao cha siri kati yake na Mbowe kilichofanyika Msimbazi Centre na kuongozwa na kiongozi mkubwa wa dini.Imeelezwa hiyo ni siri na hatari kubwa kutolewa hadharani kwa maslahi ya chama.

3. Tundu Lissu amelalamikiwa na baadhi ya wajumbe kuwa hakudhamiria kugombea Uenyekiti wa chama bali amegombea kulipa kisasi cha Wenje 'kugombea nafasi yake' kama mwenyewe alivyonukuliwa akisema siku aliporejea kutoka Ubelgiji.

4. Baadhi ya wajumbe wanasema Tundu Lissu ni mtu wa kulipiza visasi na wamesema huenda ameomba nafasi hiyo ili kulipiza visasi kwa maadui zake na kufuta kabisa legacy ya Freeman Mbowe aliyekijenga chama hicho kwa jasho na damu

5. Tundu Lissu pia analalamikiwa kutuhumu kila anayetofautiana naye kwamba ni mla rushwa ndani ya chama na ndiyo maana analalamikia wajumbe wote wanaomuunga mkono Mwenyekiti kwamba walitoa rushwa kushinda uchaguzi.Wajumbe wana hofu endapo akishinda atawafukuza wale wote wanaompinga ili aweke watu wake.Amekuwa akiituhumu mpaka sekretariati ya chama kwamba haimuungi mkono na amesema wazi wazi akishinda atawaondoa wajumbe wote.

6. Tundu Lissu analalamikiwa kumkashifu, kumdharau, kumuandama na kumtungia kila aina ya kashfa Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe kwa lengo la kumuonyesha hafai mbele ya Jamii.Wajumbe hao wamesema kwa hali ya kawaida alipaswa tu kumtunzia heshima Freeman Mbowe kwa jinsi alivyomsaidia mambo mengi ikiwemo kuokoa maisha yake alipopigwa risasi na kumtunza hospitalini Nairobi miezi 4 kama alivyonukuliwa kusema kaka yake Lissu.

7. Wajumbe wengine pia wamesema anatakiwa kuchaguliwa mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kuyaunganisha makundi yote baada ya uchaguzi kitu ambacho Tundu Lissu hawezi kwa sbabu tayari anatukana yeyote anayempinga kwamba ni mla rushwa na kapokea hela za Abdul na mama yake.

8. Tundu Lissu anatuhumiwa kuungwa mkono na makundi yaliyo nje ya Chadema yenye nia ovu ya kutaka kukiteka Chadema.Makundi hayo ni ya wanaharakati na Diaspora ambao kila kukicha wamekuwa wakimshambulia Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho.

9. Wajumbe kadhaa pia wamesema kiongozi yeyote wa Chadema hasa Mwenyekiti anapaswa kuwa mnyenyekevu kwa viongozi wenzake kitu ambacho Tundu Lissu hana, imedaiwa kitendo cha Tundu Lissu kuhutubia Taifa siku ya mwaka mpya ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mwenyekiti wake kwani anayepaswa kuongea kwa niaba ya chama ni Mwenyekiti wa Taifa na si mtu mwingine.

10. Tundu Lissu siyo mtu wa maridhiano na mapatano kitu ambacho ni kibaya sana kwa kiongozi mkuu wa chama.Wajumbe wengi wamesema Mwenyekiti wa chama lazima awe mtu anayeweza kuzungumza na makundi mbalimbali na kukubaliana au kuridhiana na hata kama ikishindikana kukubaliana basi kuheshimiana kitu ambacho Lissu msipokubaliana jambo inakuwa kama uadui.

11. Tundu Lissu amekuwa mtu anayebadili kauli kila siku kutegemeana anataka kupata nini kwa wakati huo, kwa mfano siku za nyuma aliunga mkono maridhiano na akasema ni mazuri sana na kumsifia Rais Samia lakini sasa amegeuka kabisa kauli yake na anatumia kila aina ya lugha mbaya kumkejeli Mwenyekiti wake kuhusu maridhiano.

Kutokana na Tathmini iliyofanywa na Molemo Media Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho Freeman Mbowe anatarajiwa kuchaguliwa tena na wajumbe na anatarajiwa kupata ushindi wa kati ya asilimia 60% mpaka 70% ya kura za wajumbe huku Tundu Lissu akitarajiwa kupata kura kati ya asilimia 30% mpaka 40% ya kura.

Molemo Media inatarajiwa kuwaletea tathmini yake kuhusu wagombea wa kiti cha Makamu Mwenyekiti hasa kwa wagimbea Maarufu Ezekiah Wenje na John Heche.
Molemo aka John Mrema acha kutapatapa
 
Molemo, ninakufahamu kitambo ungekuja na hoja tofauti na hii ningeshangaa sana.
Wewe na FAM ni chura na maji.
 
Mbowe sera zake ni masimango kaishiwa sera kabsa
Anataja hadi tiketi ya ndege aliyonpatia Lissu ,hakika mwaka 2025 umetuonyesha ni jinsi gani huyu Mzee alivyo Mweupe kichwani
 
Kiukweli bila kuegemea upande wowote sbb mimi sio Chadema, Mr. Mbowe ukimlinganisha na Tundu Lissu, bado Mbowe ana upper hand kiuongozi, tatizo kubwa la Lissu ni kutojua kipi cha kusema kwa muda gani, yaani ni mropokaji, kuwa kiongozi lazima uwe na kifua cha kuhifadhi mambo makubwa mengi, Lissu hana kabisa karama ya kuwa kiongozi, Lissu ni purely mwanaharakati..!!

Kuna tofauti kubwa kati ya kiongozi na mwanaharakati..!!

Mr. Mbowe bora aendelee na uenyekiti Chadema..!!
Mzee Mbowe must GO
 
Shida ilianzia hapa..
20241225_165936.jpg
 
Hii counter attack ya Lissu kugombea uenyekiti imewavuruga wamachame kinoma yaani Mbowe alivyokuwa analialia kwenye ile interview ya Kikeke anaonyesha wazi amepigwa na kitu kikali.
Alishazoea kutimua waliokuwa wanataka hii nafasi yake kama Zitto kabwe na Mzee Sumae ,hapa kwa Lissu ni amekanyaga moto wa kifuu huyu Mzee
 
Kiukweli bila kuegemea upande wowote sbb mimi sio Chadema, Mr. Mbowe ukimlinganisha na Tundu Lissu, bado Mbowe ana upper hand kiuongozi, tatizo kubwa la Lissu ni kutojua kipi cha kusema kwa muda gani, yaani ni mropokaji, kuwa kiongozi lazima uwe na kifua cha kuhifadhi mambo makubwa mengi, Lissu hana kabisa karama ya kuwa kiongozi, Lissu ni purely mwanaharakati..!!

Kuna tofauti kubwa kati ya kiongozi na mwanaharakati..!!

Mr. Mbowe bora aendelee na uenyekiti Chadema..!!
Wewe ni mtu mjinga kupindukia, Mbowe ana point ipi? Masimango ya mbowe ndiyo point? Mbowe ndiyo mropokaji, Ukiwa mjinga mjinga utaona Lisu anaropoka, lakini ukiwa na Akili timamu ya kupenda ukweli na haki utamuona Lisu yupo sawa na vizuri, Lisu kaongea ukweli na Lisu hujibu maswali ya wandishi huwezi kumpangia cha kuongea na wapi kwani hiki ni kipindi cha kampeni akiulizwa swali atajibu ingawa chawa wa mbowe kwa ujinga wao huona ni uropokaji, Ukweli unauma kuleni pesa za mbowe lakini kura ni kwa lisu
 
Team FAM inakabiwa kwa juu na team TAL kuhakikisha team FAM haivuki mstari wa katikati na kuleta madhara langoni mwa team TAL.

dk ya 75' team TAL inaongoza.
(FAM 1:4 TAL)
 
Chawa wa mbowe wengi kwa Akili yao ndogo wamekariri kuwa Lisu anaropoka, sasa endelee kukariri ujinga wenu huku wenye Akili Timamu wakichukua ukweli wa Lisu na kuuganyia kazi
 
Mbowe kusema yeye ndo aliokoa uhai wa Lissu ni kama kufuru. Aache huo ungese. Walioshiriki hadi kumfikisha Lissu hospitalini ni wengi na sio Mbowe peke yake. Halafu kama kiongozi mkuu wa CHADEMA ilikuwa lazima awe mstari wa mbele kumsaidia Lissu. Ulikuwa ni wajibu wake.
 
Yericko Nyerere...Lissu ni msaliti!
Retired...Lissu ni mropokaji!
Molemo...Lissu ni mkurupukaji!
sinza pazuri...Lissu ni muongo!
Quinine...Lissu ni mvurugaji!

Ndugu zangu, really? Mbona hizi ndizo sifa zile zile alizopewa Mh. Tundu Antiphas Lissu kabla ya kumiminiwa risasi na wabaya wake mwaka 2017?

Hebu tujikumbushe kidogo kauli ya mmoja wenu Lissu alipogombea urais mwaka 2017?

Yericko Nyerere, kwa nini, kwa mfano, nisiziamini tetesi kwamba hapa pesa, sabuni ya roho, iko kazini?
Si kila kauli ni upotoshaji bali inaweza kufikiliwa ni uropokaji ikitolewa sehemu isiyo sahihi.
 
Team FAM inakabiwa kwa juu na team TAL kuhakikisha team FAM haivuki mstari wa katikati na kuleta madhara langoni mwa team TAL.

dk ya 75' team TAL inaongoza.
(FAM 1:4 TAL)
Hahaha Tena Timu ya mbowe inalipwa mabilioni inakula pesa za mbowe kama mchwa na bado inalemewa na Timu ya Lisu isiyo na Pesa lakini inapenda ukweli na haki
 
Natambua Lissu kama walivyo binadam wengine anayo mapungufu yake, lakini wanachadema walio wengi wanataka yeye ndiye awe mwenyekiti mpya wa chadema...nyingine zote ni porojo tuu!!!.
 
Back
Top Bottom