DOKEZO Baadhi ya wanafunzi waliopata Samia scholarship UDSM wakumbana hali ngumu kufuatia kutopata fedha za kujikimu na ada ya masomo

DOKEZO Baadhi ya wanafunzi waliopata Samia scholarship UDSM wakumbana hali ngumu kufuatia kutopata fedha za kujikimu na ada ya masomo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Samakamba

New Member
Joined
Apr 3, 2023
Posts
2
Reaction score
3
Changamoto za Wanafunzi Walionufaika na Samia Scholarship – Ombi la Msaada

Tunapenda kuwasilisha changamoto zinazowakumba baadhi ya wanafunzi walionufaika na Samia Scholarship katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wanafunzi hawa wanakumbana na hali ngumu kufuatia kutopata fedha za kujikimu wala ada ya masomo, licha ya kuwa walishapokea uthibitisho wa udhamini huu.

Wanafunzi walipojaribu kufuatilia kwa Loan Officer, walisaidiwa, lakini bado hawakupata suluhisho. Walipoenda ofisi za Bodi ya Mikopo, walielezwa kuwa taarifa zao hazipo kwenye mfumo, na wakashauriwa kuomba upya. Hata baada ya kufuata maelekezo hayo, bado hawajapata msaada wowote. Aidha, walijulishwa kuwa fedha zao zipo Wizara ya Elimu, Makao Makuu Dodoma, lakini kutokana na hali duni ya kifedha, hawawezi kufika Dodoma kufuatilia.

Jaribio lao la kuwasiliana na Wizara ya Elimu kwa simu lilikumbana na changamoto za bad customer care service, jambo lililowavunja moyo zaidi. Hali hii imewalazimu wengine kufikiria kusitisha masomo kwa muda, kwani wameshindwa kugharamia mahitaji yao ya kila siku, na badhi yao hawakuruhusiwa kufanya test za baadhi ya masomo kwa kuwa ada haijalipwa licha ya kujieleza lakini bado.

Mzazi anaamini kuwa mtoto wake anasoma "bure," lakini hali halisi ni tofauti. Wanafunzi hawa wengi wametoka mikoani, hawana ndugu Dar es Salaam, na sasa wanategemea kukopa kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine.

Kwa heshima kubwa, tunaomba Wizara ya Elimu kuchukua hatua za haraka kuhakikisha changamoto hizi zinatatuliwa. Tunawasihi mtimize ahadi yenu kwa wanafunzi hawa ili waendelee na masomo yao kwa amani na mafanikio.

Wanafunzi hawa ni rasilimali kubwa kwa taifa letu. Kuwasaidia ni kuwekeza katika mustakabali wa nchi yetu. Tafadhali zingatieni kilio hiki.

Pia soma:
~
Wanafunzi wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC) hatujapata malipo ya Fedha za Kujikimu wiki ya tatu sasa
~ Bodi ya Mikopo yatoa ufafanuzi kuhusu Wanafunzi ambao hawajapata Fedha za Kujikimu "Boom"
 
Back
Top Bottom