Baadhi ya wanaume kiuhalisia wanatufanya tuonekane wote ni wapumbavu hapa JF

Baadhi ya wanaume kiuhalisia wanatufanya tuonekane wote ni wapumbavu hapa JF

Ukweli usemwe tu kama jiwe gizani haijalisha ataumia nani, Hawa wanawake wa siku hiz hapana kwa kweli.
Ukitelekezwa ndo ukauze uchi kwamba kazi zingine zote hawawezi isipokua kuishi kutegemea kiuno? Basi watuheshim tunaowaweka mjini. Na kwanini utelekezwe ujue kuna shida mahala.
Tusiwatetee hawa wahuni labda useme tupunguze ukali wa maneno.
😎
 
Mkuu Mrs,
Unajua ipo hivi, hichi ni kipindi cha watoto kufahamu teknolojia kuliko hata mtu mzima.
Embu fikiri umri wa 10-18 anapita mitandaoni na kukutana na kauli ya kwamba KATAA NDOA, UMIZA MWANAMKE.

Embu jaribu fikira ni picha gani kizazi kinabeba?
Ndio maana najaribu kusema tuwe tunafikiri cha kuandika sababu vitu hivi vinaishi hapa na athari zake zinakuja taratibu.
Vile unavyomfikiria mtoto wa miaka 10-18 akiona matangazo ya Kataa Ndoa, basi fikiria na kijana wa miaka 25+ akiona mitandaoni na mtaani wake za watu wakisariti, mke akimtusi mume, mke akikosa heshima, mke wa mtu kupenda viserengeti, mke kumroga mume, mke kumuua mumewe (refer issue ya polisi wa arusha)

Ukiwashauri wanaume kuangalia vitu vya kuandika, basi washauri wanawake kuheshimu ndoa zao pamoja na waume zao ili wanaume wakose cha kuandika
 
Wakuu habari za uzima?

Unajua Jamii forums ni ni sehemu ya kuvuna maarifa, kuburudika, na hata kutengeneza marafiki na uhusiano miongoni mwetu.

Ndugu zangu na wapendwa wote jamii forum, kuna baadhi ya mambo huenda yakawa yanachukuliwa katika hali ya utani lakini yakawa na madhara hasi pasi na mtu kulitambua hilo.

Embu Tazama mfano;
Kijana mmoja anasema, singo maza ndio wanaongoza kutoa mbususu hovyo, na pia singo maza ndio wanaongoza kujiuza kwenye madanguro?

Fikiria hii sentensi ameandika akitaka kuonyesha kwamba yupo sahihi lakini kinyume chake ni kuendelea kuvua wanaume nguo.

Kama singo maza chanzo chake kikubwa ni sisi WANAUME, mwanamke mtu kamzalisha wameshindwana labda kwa sababu mwanamke ajatulia sawa, je hayo majukumu ya mtoto wako unamuachia nani?

Huyu singo maza kila atakapoenda kutafuta kazi ataombwa rushwa ya ngono, mwanaume tayari kashakimbia na hakuna huduma yoyote anayoitoa kwa mtoto wake.

Unafikiri huyu mwanamke atafanya nini kuendelea kumpa huduma muhimu mtoto wake? Mwisho wa siku ataishia kutafuta njia za kujirahisisha ili tu aendelee kumtunza mtoto wake kwasababu tu ya mwanaume mpumbavu asiyejua kwamba kuwa mwanaume kuna ambatana na majukumu mazito.

Wanasema chizi hufurahisha anapokuwa si nduguyo, ila kama ni nduguyo hicho ni kilio. Tumuulize tu kama dada yake akamkuta katika madanguro sababu ya mwanaume ambaye alimtelekeza yeye atajisikiaje?

Kama kijana huyu sasahiv ngozi bado imenyooka, damu bado ya moto, ananyoa anapendeza akifikiri kwamba ujana utakuwepo tu basi ni kujidanganya.

Ipo siku mtoto wako wakike na yeye atakuwapo katika madanguro kwa sababu ya mwanaume mpumbavu kama wewe ambaye ulishindwa kutimiza majukumu yakiume.

Embu fikiria huu mfano;
KATAA NDOA, UMIZA MWANAMKE.

Huyu ni mtu ambaye anasema umiza mwanamke, ambaye kaja kwa kupitia kati kati ya mapaja ya mwanamke huyo!
sasa tumuulize kama amesema umiza mwanamke je mama yake aliyemzaa alishamuumiza? Hivi wanaume huwa mnajaribu kufikiri mnachoandika hapa?
Je huyu aliyesema umiza mwanamke yupo tayari kumuona mama yake akinyanyasika mbele yake na akampongeza huyo anayemnyanyasa?

Jamani ndugu zangu embu tujaribu kufikiri japo kwa uchache mambo tunayoongea, hii sehemu inafika watu wengi sana.

Tunaweza kuonekana wengi ni wapumbavu wasio na maana sababu tu ya wachache ambao wanahitaji watu wakuwaweka busy kwa kusoma maoni yao.

Kama unahitaji kuumiza mwanamke aidha kwa kihisia, hawa wanawake wasipokuwapo unafikiri tutaendelea vipi kuongezeka?

Hao watu wakufanya kazi ya kuliendeleza taifa watatoka wapi na tayari mtu anasema umiza mwanamke?

Naomba tu ndugu zangu tujaribu kufikiri tunachokiandika hata kama ID tunazotumia ni feki, embu tujitahidi tu.

Yaani kila siku wanaume tunaendelea kuvuliwa nguo sababu ya watu wachache , tunaendelea kuonekana si lolote sababu ya mambo haya!
Mwanamke ukishazaa nae wana tabia ya kumtumia mtoto kutaka kumuendesha mwanaume na kumlazimisha atoe mahitaji ambayo sometimes unakuta yapo nje ya uwezo wa mwanaume na kuna ambao wanabambikia wanaume watoto, diamond alipelekwa mpaka mahakamani kudaiwa child support na hamisa kumbe mtoto sio wake. Migogoro ya kimahusiano tumempa mwanamke victim status ndio maana mara zote mwanaume anaonekana mkosaji lakini tukipata wasaa wa kuwasikiliza na wanaume wanasemaje hakika utagundua wanawake walio wengi ni mashetani ambao hawapaswi kabisa kuendelea kuishi hata ivyo maamuzi ya kubeba mimba ni ya mwanamke asipotaka basi hauwezi kumtia mimba labda umbake kwaiyo kwa kiasi kikubwa hao singo maza nao wana makosa walishindwa kuwafanyia vetting hao waliowatia mimba, ni sawa sio vizuri kwa mwanaume kutelekeza mwanamke uliemzalisha but a woman she is the one suffer consequences so she must be more carefuly, now days relationship is a trap, women are after mens' money while men are after womens' body kwaiyo ukisikia mmoja kapiga yowe ujue kaingia kwenye mfumo wa mwenzake. Binafsi siwezi kuoa singo maza, first born ndani ya nyumba lazima liwe bao langu.

Kuhusu ndoa ilo suala lipo wazi kabisa. Ndoa ni mkataba wa kitapeli kwa mwanaume. Ukipitia sheria ya ndoa ilo lipo wazi kabisa labda uamue tu kuwa mbishi.
 
Mwanamke ukishazaa nae wana tabia ya kumtumia mtoto kutaka kumuendesha mwanaume na kumlazimisha atoe mahitaji ambayo sometimes unakuta yapo nje ya uwezo wa mwanaume
Mkuu Natafuta,
Si kweli, kwani hufahamu madawati ya kijinsia? Ulishawahi fika?
Changamoto kutokana na takwimu ni wanaume kukimbia moja kwa moja malezi ya watoto bila kuchangia chochote.
Tulee watoto wetu kadri ya uwezo tulionao.
 
Back
Top Bottom