Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Never....Never....Never....waliojaribu kufan6a wamechokaje...na mbinguni waangalie wasijekufika hoi taabaniUntil it happens to you[emoji23]
Nasikia hizo bidhaa ni dili sana mkuuKama tukiweza kusimamisha na kuzuia kabisa supply ya damu na nyama kwa washirikina tutaokoa roho nyingi sana...!
Kama tutaweza kudhibiti matumizi ya maji ya mochwari kishirikina tutaokoa mapooza mengi sana! LAKINI kuna wakati ili kuokoa wengine hatuna budi kuyatumia.. Tena sometimes kwa kufanya na ibada ya 40 kabisa na kuanua tanga... Kuna baadhi wanajifanya moto sana.. Hawa dawa yao ni kupoozwa tuu...
Serious....?Yeah .. Yana oda kabisa
Kaka samahani kwakutoka nje ya mada... ivi kuota ndoto za wafu inasababishwa na nini [emoji120][emoji120]Ndio
Sasa rafiki yangu Mshana Jr tangu umestaafu umekuwa baba mchungaji au nani? Hapo kwenye maombi umenikosha. Kumbe hata nyie wachawi huwa mnaogopa maombi?Hatua za kuwa mshirikina (combine ya uchawi, uganga, ulozi, kuwanga, kuroga na kuwanga)...! Haya yote ndio yanatengeneza neno USHIRIKINA!
Hatua ya chini kabisa ni kuweza kupaa na ungo na kuingia kwenye majumba ya watu na kuwachezea... Katika hatua hii pia kuna masomo mengine kama chuma ulete, kuchukua kitu cha mtu mbele yake bila mwenyewe kukuona, kupiga zongo nk
Hatua ya pili ni uwezo wa kujigeuza maumbile, kuvaa sura ya mtu mwingine au kujigeuza kuwa mnyama... Na hii mara nyingi hufanyika bila hata kiza kuingia
Hatua ya tatu ni uwezo wa kufika mbali kwa kitendo cha kufumba na kufumbua macho, kumvuta mtu umtakaye aje mbele yako na uwezo wa kuua ukiwa mbali
Kwahiyo kati ya wanga wanaowasumbueni usiku wengine ni wpagazi wa kutumwa vitu mbalimbali kama kucha, nywele, nguo, kuchanja chale, kwenda kuchukua wafu mahospitalini ama kukusanya damu na nyama maeneo ya ajali ambapo mara nyingi ndio wao wanakuwa wamezisababisha ama aliyewatuma
Wale washirikina makonki wa madaraja ya juu huwa hawajihangaishi kutoka kwenda kutafuta chochote hata kana wana huo uwezo bali huwatumia vijana wanaowafundisha kazi ama wasaidizi wao kwa hiari!
Je na hawa watumwa ni akina nani? Watumwa wa kishirikina namaanisha! Hawa ni watu walioko huko si kwa ridhaa yao bali kwa matendo ya binadamu wengine na wengi wao huwa kiasili ni misukule.. Hawa hutokana na Kukosana na 'wazee wa busara kisha wakakukomoa.
Ugomvi wa familia au ndugu
Kugombea mirathi ama mali
Vyeo na nafasi kazini
Umaarufu na utajiri pia
Kuna namna tatu ya kupata watumwa
1. Kumtia mtu wendawazimu/ kumfanya chizi
2. Kumpoteza asionekane tena
3. Kumchukua msukule/ kumuua kishikirina hasa hasa kupitia ajali
Ushirikina ni sayansi ya ajabu kabisa na iko deep sana...!
Unaenda kumfanyizia mtu kwa mganga kwa nia yoyote ile.. Ukifika unapewa karai lenye maji kisha anaitishwa pale nawe unamuona live kabisa sura yake.. Kisha unapewa kisu umchome! Ukishafanya hivyo tu maji yote kwenye karai yanageuka damu na huko aliko mhusika anapata ajali yoyote na kufa!
Kwanini kuchoma uso? Sio popote bali unatakiwa kuchoma sehemu ya koromeo...
Kwanini huchomi sehemu nyingine za mwili? Inawezekana kabisa ila kama hutaki afe bali apate tu ajali mbaya .. Hapo ataumia zaidi sehemu husika
Magonjwa je?
Washirikina mara nyingi hawatumii magonjwa kwakuwa unaweza kupata tiba na kupona...lakini akikukamia ili akutese muda mrefu anakupiga na maradhi ambayo utamaliza hospital zote bila tatizo kuonekana
Dawa na kinga kwa washirikina ni hizi mbili zisizo na madhara ya baadae
1. Maombi na dua.. Usiache kufanya maombi wala dua kwa kila ufanyacho iwe chakula, iwe kinywaji, iwe ukitoka ndani, iwe ukipanda chombo cha usafiri, iwe ukiingia ofisini, iwe ukiingia nyumbani nknk
2. Tumia chumvi ya mabonge kadiri uwezavyo..itangulize popote unapotaka kwenda au chochote unachotaka kufanya na ukiweza inenee au nuia..!!!
Ulimwengu usioonekana una mengi mabaya na washirikina ni sehemu yao!
Laleni salama! Na Mungu awalinde na kuwapigania...!!!
Witchdoctor mstaafu.
Umemkabidhi mtoto wako au mke wako?Bado makabiZiano tuu
Kwa hiyo unamwuzia au unampa bure? Sasa mtaalam kabla hujagawa ndumba unaonaje ukinisaidia kuwanyoosha hawa waliokimbia ha hela yangu?😁😁😁😂😂Mdau toka Sumbawanga
Aah... Kakimbia na bei gani?Kwa hiyo unamwuzia au unampa bure? Sasa mtaalam kabla hujagawa ndumba unaonaje ukinisaidia kuwanyoosha hawa waliokimbia ha hela yangu?[emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23]