Baadhi ya watu wanajiuliza kwanini ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu?

Baadhi ya watu wanajiuliza kwanini ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu?

Huna hoja yeyote.

Soon wewe, Erythrocyte na Salary Slip mtaanza kuandika mada zinazofanana.

Maana adui yenu ni mmoja sasa.

Njaa mbaya sana.

Watu mnaangalia matumbo yenu tu.
Hebu usitoke nje ya mada, baki kwenye mada jadili hoja iliyoko mezani, ukisema huyo "bwana yule" haonekani kuwa na mrengo wa huyu wa sasa useme how, binafsi siamini kwanini siri zilizokuwa zinatoka wakati wa awamu ya tano ghafla zisitoke awamu ya sita, kwa move ipi aliyofanya huyu aliyepo madarakani kuzuia wakati anashindwa hata kwenye teuzi tu, anateua sasahivi badae anatengua.
 
77.jpg
 
Hebu usitoke nje ya mada, baki kwenye mada jadili hoja iliyoko mezani, ukisema huyo "bwana yule" haonekani kuwa na mrengo wa huyu wa sasa useme how, binafsi siamini kwanini siri zilizokuwa zinatoka wakati wa awamu ya tano ghafla zisitoke awamu ya sita, kwa move ipi aliyofanya huyu aliyepo madarakani kuzuia wakati anashindwa hata kwenye teuzi tu, anateua sasahivi badae anatengua.
Kwa mtazamo wangu, siri zake zilijikita kwenye "kutabiri", kutafiti ( hasa online ) na kupewa taarifa inbox ( kama ilivyokuwa kwa Mange Kimambi )

In short, Magu mwenyewe alikuwa mropokaji tu. Hakuwa na siri yoyote.

Angekuwa kweli ni mtu wa siri sirini, angesema walipo Ben Saanane, Kanguye, Azory Gwanda.

Kwasababu hakuna silaha aliyobakiza, angekuwa anajua angekwishasema.
 
Tulieni na sio kila jambo la ikulu ni siri hatarishi, pengine Magu ndio akimpa toleo atangaze ili kupima upepo.
 
U bwana yule nae kashapewa cheo ndio maana anamshambulia sadala tu,yaani sasa hv yeye na mange wote ni sawa tu
 
𝚂𝚊𝚜𝚊𝚑𝚒𝚟𝚒 𝚊𝚗𝚊𝚍𝚒𝚕𝚒 𝚗𝚊 𝙳𝙸𝙰𝙼𝙾𝙽𝙳
 
Kwa mtazamo wangu, siri zake zilijikita kwenye "kutabiri", kutafiti ( hasa online ) na kupewa taarifa inbox ( kama ilivyokuwa kwa Mange Kimambi )

In short, Magu mwenyewe alikuwa mropokaji tu. Hakuwa na siri yoyote.

Angekuwa kweli ni mtu wa siri sirini, angesema walipo Ben Saanane, Kanguye, Azory Gwanda.

Kwasababu hakuna silaha aliyobakiza, angekuwa anajua angekwishasema.
Sasa kwanini hizo siri zitoke wakati ule halafu ghafla wakati huu zisitoke? hao waliokuwa wanampa taarifa "inbox" where are they now? hapa ndipo nakubaliana na mleta mada, hawatoi siri kwasababu aliepo madarakani ni rafiki yao, lakini sio kwamba siri hazipo.
 
Sasa kwanini hizo siri zitoke wakati ule halafu ghafla wakati huu zisitoke? hao waliokuwa wanampa taarifa inbox where are they now? hapa ndipo nakubaliana na mleta mada, hawatoi siri kwasababu aliepo madarakani ni rafiki yao, lakini sio kwamba siti hazipo.
Sijasema directly kuna siri alikuwa anapewa. Hizo ni assumptions zangu tu.

Ila kwenye kutabiri hasa kwa kumsoma Magu alikuwa vizuri.

Kumtabiri Samia imekuwa ngumu, alijaribu zaidi ya mbili akashindwa nadhani ndio maana ameamua kupunguza au kuacha.

Scenario ya kwanza ilianzia wakati wa vuguvugu la kumpata makamu wa Rais. Akawa ameshataja watu kibao. Na alivyoona kwenye mkutano wa CCM yupo Kikwete wakiwa na Karume, na kwa kuwa Kikwete alikuwa na ukadibu sana na Nchimbi akasema VP atakuwa Nchimbi

Wakati huo alikuwa anajaribu kuonesha kuwa, kuna makundi mawili yanasigana ndani ya CCM ambayo ni kundi la Kikwete ( Msoga gang ) na kundi la Magu ( Sukuma gang )

Alivyokuja kupatikana Mpango, akaanza kushout kuwa Samia ka-surrender kwa Sukuma gang, na wakati huo huo sasa hivi anashambulia kwamba Samia anasikiliza sana Msoga gang ( Kikwete )

Kitu kingine ni yeye kutabiri zaidi ya 2 kuhusu wakuu wa mikoa na wilaya, then ikawa bila bila.

In short ni utoto utoto tu, haya mambo yasome na yasikilize ukiwa na akili zako timamu.
 
Wakuu Salaam,
Twende kwenye mada,
Katika machweo ya utawala wa Shujaa Mwendazake Hayati JPM kuliibuka wanaharakati wengi sana wakosoaji hasa katika mitandao ya kijamii. Nje ya mwanadada Mange Kimambi aliyejikita sana katika mtandao wa Instagram aliibuka mtu mwingine ama kikundi cha watu kinachotumia mtandao wa Twitter na akaunti yenye jina @kigogo2014 inayotumia picha ya msanii maarufu wa kimarekani Jay Z.
Mtu huyu alijizolea umaarufu mkubwa mno kwa kuvujisha nyaraka mbalilmbali kutoka ofisi nyeti za Serikali ikiwemo Ikulu na TISS, aliweza kwenda hatua moja mbele zaidi kwa kujua mathalani lini Rais atafanya uteuzi ama atafanya jambo fulani, mambo haya yalimfanya akaaminika na umma.

Jambo hili inaonekana dhahiri lilimchanganya sana "Mzee" na asijue afanye nini ili aweze kumdhibiti. Mambo haya yalifanya watu waweze kuhisi huenda ni wasaidizi wa karibu wa "Mzee" mwenyewe ndio wanamzunguka.

Pamoja na mambo mengi hata kuugua mpaka kufariki kwa "Mzee" jamaa huyu ndiye alikua kinara wa kuvujisha taarifa nyeti kabisa hizi za kiusalama ikiwa ni pamoja na kutaja mpaka tarehe za matukio muhimu.

Waswahili wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha, baada ya Mhe. Rais Samia kuingia madarakani tukajionea maajabu, yule aliyeaminika akaanza kuwa mpiga ramli kwa kuanza kubahatisha majina ya wateule wa kiti cha umakamu ya Rais, ikala kwake. Likaja Baraza la Mawaziri kapiga ramli ili aendelee kuwa "relevant" na kutopoteza imani ya wafuasi wake, ikala kwake. Kwa mfululizo huo wa matukio kadhaa alianza kuonekana kabisa kwamba hana anachokijua zaidi ya kubahatisha, na kwa hivi sasa ameachana kabisa na ubashiri amejikita zaidi kwenye kudandia matukio na kujisomea taarifa rasmi zinapotolewa na serikali na kutoa maoni yake kama wananchi wengine.

Hili linatufundisha ya kwamba utawala huu umefanikiwa sana kudhibiti taarifa zake za ndani, na kwa vyombo vya usalama ni wakati sasa wa kufanya upekuzi kwa waliokua wasaidizi wa karibu wa mwendazake kwani tunaweza kujifunza kitu.
Hivi sasa Bwana kigogo amebaki kuwa mpenzi mtazamaji, umaarufu wake umepotea amebaki kuwa mtukanaji na mchambaji hana jipya na soon ataikimbia twitter maana wale waliokuwa wanafadhili hizo harakati hawaoni tena tija ya kumtumia.

Naombeni radhi kwa uandishi mbovu, nawasilisha.
 
Back
Top Bottom