Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Remember Mwanakijiji na kainzi!~!!!!Nimeona sehemu nyingi baadhi ya watu wakijadili kuhusu ''bwana yule'' huku wengine wakimbeza lakini wengine wakiuliza kimetokea nini kwa sasa ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu...
Mkuu, yaani wewe huwa nakuelewaga Sana, najua kuwa wewe ni mpinzani na moyo wako unapenda mageuzi, cha ajabu ni Kwamba, unapenda zaidi kujadili hoja na sio ushabiki,Hebu usitoke nje ya mada, baki kwenye mada jadili hoja iliyoko mezani, ukisema huyo "bwana yule" haonekani kuwa na mrengo wa huyu wa sasa useme how, binafsi siamini kwanini siri zilizokuwa zinatoka wakati wa awamu ya tano ghafla zisitoke awamu ya sita, kwa move ipi aliyofanya huyu aliyepo madarakani kuzuia wakati anashindwa hata kwenye teuzi tu, anateua sasahivi badae anatengua.
Kwani huyo Kigogo alikua anatoa Siri za nchi.?Nadhani hujui maana ya siri za nchi!
Lakini kafanikiwa kumuangusha magufuli[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sasa hivi wamejikita kupambana na diamond!
Kweli ccm ni jabali
kwahio kumbe ni internal job??Napenda niwasaidie kwa kuwaambia kuwa hakuna siri za Ikulu zilizozibitiwa ila wale waliokuwa wanatoa siri za Ikulu na kuzipeleka kwa ''bwana yule'' kwa sasa ndio hawa ambao wako madarakani. Kwa maana nyingine, kwa sasa ndio walioshika Ikulu/utawala moja kwa moja. Yaani sio tena watoa ushauri bali kwa sasa ni wabunifu na wasimamia utekelezaji.
Kwa namna moja ama nyingine, lengo la kigogo Kwa mtizamo wake na wa Baadhi ya wengine, pengine ulikuwa ni zuri Sana,Sio kwamba utawala wa Samia umefanikiwa kuzuia siri za serikali zisimfikie Kigogo, issue ni kwamba wale waliokuwa wanavujisha hizo siri awamu iliyopita ndio marafiki wa Samia...
Pumbavu kaa kimyaKwani huyo Kigogo alikua anatoa Siri za nchi.?
Mijinga Sana Wewe.
Tofautisha Siri za nchi na Siri za uovu wa Mtawala.
Una udugu na Akwilina?Bahati nzuri mimi natumia sana internet. Natumia akili zangu timamu.
Huyu mtu alikuja humu 2015 ( sababu za ujio wake zinafahamika)..
Sina. Ila ni muumini wa utu na ubinadamu.Una udugu na Akwilina?
Labda yeye alikuwa muwazi tu katika kuonesha furaha yake. Lakini kwa yaliyotokea na yanayoendelea sasa, ni wazi kabisa watanzania wengi zaidi walifurahi (ukiacha mtoa mada hii, "mimi", mataga, na sukuma gang) na wengine labda walifurahi zaidi ya hata huyo 'chigogo'.Kwa namna moja ama nyingine, lengo la kigogo Kwa mtizamo wake na wa Baadhi ya wengine, pengine ulikuwa ni zuri Sana...
Nenda instagram usome siri alizovujisha za sabaya leo ujue jamaa ni nomaNilicholeta hapa sio theory bali ni ukweli halisi! Tofautisha ukweli halisi na theory!
Mkuu MsemajiUkweli, umefanya analysis moja matata sana, kuna wakati na mimi nilikuwa najiuliza hivi, "Bwana yule" na haya mapenzi na CHADEMA yameanza anzaje? Kuna nini ameshaona amekikosa?Nimeona sehemu nyingi baadhi ya watu wakijadili kuhusu ''bwana yule'' huku wengine wakimbeza lakini wengine wakiuliza kimetokea nini kwa sasa ''bwana yule'' hapati tena siri za Ikulu.
Kwa wasiojua vizuri wameenda mbali zaidi na kudai eti kwa sasa siri za Ikulu zimethibitiwa na uongozi mpya!
Napenda niwasaidie kwa kuwaambia kuwa hakuna siri za Ikulu zilizozibitiwa ila wale waliokuwa wanatoa siri za Ikulu na kuzipeleka kwa ''bwana yule'' kwa sasa ndio hawa ambao wako madarakani. Kwa maana nyingine, kwa sasa ndio walioshika Ikulu/utawala moja kwa moja. Yaani sio tena watoa ushauri bali kwa sasa ni wabunifu na wasimamia utekelezaji.
Biashara yao na ''bwana yule'' ya kumpa siri za Ikulu iliisha siku ambayo Rais Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania!
Haishangazi kuona kwa sasa ''bwana yule'' anawashambulia sana baadhi ya wale waliokuwa wanampa siri za Ikulu baada ya kugundua hawataki tena mahusiano naye. Yaani kwa sasa wamemalizana naye!
Nasikia kwa sasa wale wale waliokuwa wanampatia siri za Ikulu wana mpango wa ''kumnyamazisha'' ili huko mbeleni asije akatumia umaarufu waliomuwezesha wao wenyewe kuichafua serikali yao. Kibaya zaidi, wanamjua vizuri kwa maana kuwa, wanazijua nguvu zake na udhaifu wake(strengh and weakness) kwa sababu ndio walimuwezesha kupata umaarufu kwenye mitandao ya kijamii. Hata kupata kitambulisho cha ''blue tick'' ilikuwa ni jitihada za baadhi ya wale waliokuwa wanampatia siri za Ikulu.
Baada ya kukosa ushirikiano kwa sasa ''bwana yule'' anafanya jitihada za kuwa karibu na wenyeCHADEMA ili apate uungwaji mkono kwenye mitandao! Kwa wanaofahamu historia ya ''bwana yule'' watajua kuwa huko nyuma hakuwahi kuipenda/kuishabikia CHADEMA hasa hakumpenda Mwenyekiti Mbowe na aliwahi kumshambulia sana akidai mwizi wa pesa za chama.
Huko mwanzo, ''bwana yule'' alikuwa ni mwanaCCM lakini baadaye akawa ''mwanaACT-Wazalendo'' kabla ya ujio wa Maalim Seif na kundi lake! Wakongwe wa siasa nchini wanajua kuwa ACT-Wazalendo ni ''stepping stone'' kwa wanaCCM! Kwa maana nyingine, ACT-Wazalendo ni kama fimbo ya kuchapiana wanaCCM kwa wanaCCM!
Hasira za ''kutoswa'' zinamfanya aanze ''revenge'' kwa waliomtosa kwa kutumia ''platform'' za CHADEMA. ''bwana yule'' anajua bila kupata sapoti ya wanaCHADEMA hawezi kuendelea kuwa ''relevency'' kisiasa katika dunia ya mitandao!
Hoja iliyopo kwa sasa ni kujua kama ''kinyago'' walichokichonga walioko madarakani kwa sasa kitawatisha au watakiangamiza kabla hakijaanza kuleta madhara!
Kigogo alikuwa anakosoa au alikuwa anachafua? kwa sababu hakuna utawala ambao upo perfect ndio maana hata marais wote waliyopita kabla ya Magufuli walikuwa wanafanya makosa na walikuwepo wa kuwakosoa, kwahiyo kama kutoa siri za serikali kama alivyokuwa anafanya Kigogo ndio kukosoa basi tutegemee siri za serikali kuendelea kutoka maana hata sasa makosa yapo.Sijaelewa.
Kwani lengo la Kigogo2014 kilikua Ni kutoa Siri za Ikulu ama kufichua mwovu ya Mtawala dhalimu.
Kama utawala wa Sasa unatenda mema Atafichua wema?
Nakuambia Hivi watu kama Kigogo huja kama utawala huminya haki za wananchi.
Watu kama Kigogo hupewa sapoti na watu wa mifumo kukosoa na kufichua uovu wa watawala wanapigana uhuru wa kutoa maoni.
Kwa huyo Mama karuhusu kukosolewa,Kigogo Hana kazi tena.
Mama akinyima uhuru Kigogo au Vigo wengine wataibuka tena.
Suala la kumnyamazisha hakina mashiko kwa sababu watu waaliomuona nuksi hawapo madarakani tena,na siku zinavyokwenda wanazidi kupoteza nguvu.mwisho wataishia kbs.
Ok nilidhani una udugu nawe, unajua kwenye uhalisia wa maisha sio kila kitu kitamgusa kila mtu pamoja huo utu na ubinadamu.Sina. Ila ni muumini wa utu na ubinadamu.
Nalijua hilo. Lakini watu wasio na utu ni wa kuwaweka mbali sana.Ok nilidhani una udugu nawe, unajua kwenye uhalisia wa maisha sio kila kitu kitamgusa kila mtu pamoja huo utu na ubinadamu.