Mwenye akili timamu hujibidiisha katika kuwatendea wengine wema na kuwaombea kheri na sio kuwaletea na kuwauzia madawa ya kulevya ili wafe,
Lakini pia, unachokisahau mkuu, aliyeanzaga kufa ni Habili baada ya kaini kumuua, na hivyo, Dunia haijawahi kupumzika kumeza watu, na hata Mimi na wewe, ni swala la muda tu, na Kwa sababu hiyo, litakuwa Jambo la kipumbavu na kijinga kuliko chochote akiwako mtu mwenye kufurahia mtu mmoja afapo Wakati huohuo naye muda wake wa kufa ungalipo na asijue ni lini na saa ngapi atakufa
Kivyovyote, Hayati JPM kama ilivyotokea Kwa wengine kufa, Ilibidi tu aondoke Kwa maaana muda wa yeye kuishi duniani ulikuwa tayari umeshakwisha, ama ni Kwa sababu Mungu alimwita ama tu pengine shetani alihusika, lakini Kwa sababu Mungu ndiye mwenye mamlaka na umauti, aliruhusu Hilo litendeke ili tu iwe tamati ya kila kitu alichokipanga kwenye maisha ya Mtumishi wake
Sasa kazi kwenu, kudhihaki kazi ya Mungu ama mnyamaze Kwa kuwa, hakutakuwa na ujanja wa yeyote kukwepa umauti,
Lililobora zaidi, Ishi, Kwa sababu Mungu bado anataka uishi, Watendee wema waja wake na sio wewe uwe sababu ya kuwaangamiza kuwaletea sumu na madawa ya kulevya ili kuuwahisha uhai wao na wakati walustahili kuendelea kuishi
Mungu bariki Tanzania, na uwamlike wote wanaosababisha kumwaga damu na kuuwa wengine