Mishahara kama mishahara bila mkataba kuna ukakasi kidogo hapo, lakini pia tunatakiwa jiuliza, je unapoongelea mishahara ina maana inajumuisha stahiki zote ambazo mfanyakazi wa kawaida anastahili?
Naweza nikasahihishwa lakini taasisi za kidini zina kawaida ya kuwa na watu wengi ambao ni waumini na wanafanya kazi kwa kujitolea, hivyo ni muhimu kuangalia kwanza hilo kabla ya kufikia kuongelea mikataba ya ajira.
Pia katika kuangalia kuna umuhimu wa kuangalia historia ya ajira za hao watumishi.