Baadhi ya Waumini wa Kanisa Katoliki waonekana wakinywa Konyagi nje ya Kanisa la Mt. Joseph

Leta ushahidi wakanisa lako likiwa limemfikisha muumin wake huko kwababa mungu
Haaa bwasheee, YESU ndio Njia ,Kweli na Uzima ,MTU haendi Kwa Baba Mungu bila kupita Kwa YESU.

Je wajua YESU ni MSABATO?.

KANISA LA kweli ambalo hata RC leaders wanajua ndio Kanisa la Kweli, ni SABATO -SDA.
 
Ukristo halisi ukoje?
 
Mlio... tatizo kamdomo
 
Andiko hilo halihalarishi pombe, wala halisemi Yesu alikuwa mnywaji wa pombe, bali linatoa tafsiri ya maisha ya ujumla jumla ya Yohana vs Yesu.
kwa hiyo pia halisemi pia kuwa alikuwa rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi, au sio?
 
nikweli nimeshuhudia kuna jirani yangu ni mkatoliki akiwa anaenda kanisani anapita vilabuni anakunywa pombe wakitoka anapita tena anakunywa pombe nilikuwa nafikiria sipati majibu leo nimepata ukweli nikama chanda na pete.
 
Dini ya Uyahudi pombe ni sehemu ya ibada yao na chakula chao. Divai ni pombe siku zote, sio juice ya zabibu.
 
Hahahah Biblia ya Wakatoliki, Ina vitabu 72 πŸ˜‚πŸ˜‚ utasikia Sira, Sijui nani nani, vitabu vya kininadam vyenye Maneno yaloandikwa yoyote na WANADAM.
Biblia ya Mungu Ina vitabu 66 tu.
Hata hivyo 66 unavyoita vya Mungu ni subset ya vitabu 72 ambavyo Luther alivichukua kama vilivyo kwa Wakatoliki.
Kwa ufupi (kama hujui), si kwamba Wakatoliki waliongeza vitabu, ila Luther alipunguza vitabu!
 
Dogo mimi nimeandika yaliyomo kwenye Biblia Takatifu. Wewe unaandika kwa hisia. Huoni tofauti hapo?
Habari zote za Nuhu nimetoa kwenye biblia. Habari kamili za ukatoliki zipo kwenye vitabu na maandiko ya kikatoliki, kwa kuwa ukatoliki umejengwa katika maandiko tofauti tofauti, na sio lazima yawe maandiko ya kibiblia. Msingi mkuu wa ukatoliki upo kwenye mapokeo (matamko, maagizo, matangazo, mafundisho ya wakuu wa kanisa katoliki kule Italy)
 
Hahahah Biblia ya Wakatoliki, Ina vitabu 72 πŸ˜‚πŸ˜‚ utasikia Sira, Sijui nani nani, vitabu vya kininadam vyenye Maneno yaloandikwa yoyote na WANADAM.


Biblia ya Mungu Ina vitabu 66 tu.
Hata ibada zao zinatumia kiswahili tofauti
  1. Kitubio
  2. Mafungo
  3. Komunyio (kuna makabila hilo ni jina la sehemu ya mwili)
  4. Dominika
  5. Homilia
  6. Komunika
Ukiingia muumini mwingine unaweza kutoka kapa
 
Biblia ya Mungu Ina vitabu 66 tu.
Mathayo na Yohana ni miongoni mwa hivyo vitabu 66 vya Mungu au ni miongoni mwa vile vya kibadamu vya Wakatoliki?

Mathayo 11:18-19
18 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo
19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.

Yohana 2:7-11
7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
 
Sasa ndugu yangu Mungu mwenye Rehema atashindwaje kuwa na huruma na kiumbe chake alichokiumba mwenyewe na kukipa mzigo wa utashi? Mawazo, shida, chuki na misuguano mingine ya kibinadamu inahitaji walau mara moja moja nati zilegezwe; nyinyi wenzetu naona bado mnaishi kwa misingi ya agano la kale ambapo Baba muumba ilibidi awe mkali sana maana kumstaarabisha binadamu kwa mazingira ya jangwani sio kazi ndogo
 
wale hawajaokoka, habari za wokovu wako mbali nazo, dhambi zimewajaa, kunywa pombe kwao ni kawaida na dhamiri zao haziwashitaki kuwa wanatenda dhambi kwa ulevi
Waliookoka ni wale wanauza maji na udongo wa uzima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…