Biblia ya Mungu Ina vitabu 66 tu.
Mathayo na Yohana ni miongoni mwa hivyo vitabu 66 vya Mungu au ni miongoni mwa vile vya kibadamu vya Wakatoliki?
Mathayo 11:18-19
18 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Yuna pepo
19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Yohana 2:7-11
7 Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.
8 Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.
9 Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,
10 akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.
11 Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.