Hilo nimeshalijibu.
Kama neno Divai kwenye muujiza wa harusi ya kana wewe umelistafiri kuwa ni pombe, hapo utakuwa umekosea sana. Kwanini? Haiwezekani Yesu afanye muujiza wa kutengeneza 'pombe' harusini, halafu watu wote wanyee mpaka watosheke (walewe?) halafu tukio hilo limrumdishie tena Mungu utukufu. Haiwezekani.
Unywaji wa pombe vilivyo unawezaje kumrudishia Mungu utukufu?
Kwa akili ya kawaida kabisa, popote pale, hata leo hii, mahali penye unywaji wa pombe ya kutosha panajaa uovu na kumpa utukufu shetani.