Baba ahukumiwa miaka 40 jela kwa kuzaa na binti yake

Ni mtoto wake wa kumzaa au ni mtoto wa kambo? Watoto wa kambo ni hatari kufanyiwa vitendo vibaya na baba wa kambo kama ndoa ikivurugika mababa mengine wa kambo hukomoa wake zao kwa kuwalala watoto wasiowazaa
 
Miaka 27 ni umri mkubwa kwa msichana, huyo binti ana akili timamu au alitekwa na baba yake kisha akabakwa? Au huyo baba ana akili timamu au alifanya hivyo kama takwa la imani za kishirikina?
 
Sasa najiuliza hapa nani kashitaki? Kwahyo mtoto kaamua kumfunga babake ? Na je alibakwa au ? Hii laana ni kubwa sanaaa
 
Hii ni fasheni mpya ya kula watoto wa kuwazaa au ni ushetani tu ulioibuka? Unakulaje damu yako? Kuna kuchanganyikiwa hapo
 
Mtoto anakosa malezi ya baba na babu kwa pamoja,wakati uzembe ni wa bint,,miaka 25 unashindwa kusepa??umeshajua umenasa na unajua n ya baba yako unakosa cha kufanya??
 
Haya mambo ya DNA wtk mwingine sio ya kayaamini saaaaaaaaaaanaaaaaaaa.

Tena kibongobongo [emoji848][emoji21]
 
Nina wasiwasi sana na hili suala. Usikute kulikuwa na kutokuelewana kati ya wanandoa halafu mama na mtoto wakatumia mbinu za medani mtoto aende kwa baba yake ajilengeshe halafu akinasa wafungue kesi. Unahitajika uchunguzi wa kina hapa kwanza kujua wanandoa hawakuwa na ugomvi. Vipi wanandoa hawakuwa wanagombania mali kama nyumba, mashamba, n.k..

Kwa akili ya kawaida kabisa miaka 25-27 sio mtoto mdogo na ingetokea kabeba mimba ya baba yake bahati mbaya lazima angesepa kupoteza ushahidi ili baba yake asifungwe na kupoteza ushahidi na kumfichia aibu baba yake mzazi. Lakini kama katoa ushirikiano kwa polisi na mahakama basi huo ni mchongo wa huyo mtoto na mamayake. Ndugu wa mume shtukeni na mchukue hatua haraka ndugu yenu huyo wamemfix full stop.
 
Wanaume Kwa kujitetea hamjambo
 
Wanaume Kwa kujitetea hamjambo
Sio suala la kujitetea ni kufanya tu uchunguzi rahisi sana na kujiridhisha maana miaka arobaini aliyofungwa sio kidogo na hasa ikija kugundulika kuwa kulikuwa na ujanja ujanja nyuma yake. Ni kujua tu kama mke yupo hai na alikuwa wapi mpaka mzazi mwenzie? Wanandoa wanaishi pamojana ? Kuna ugomvi wowote kati ya wanandoa? Kuna mali zingombaniwa kati ya wanandoa? Je mtoto aliyepewa mimba ni mtoto halali wa huyo baba na wamempima DNA kumthibitisha isije ikawa baba kazaa na mtoto wake wa kufikia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…