Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mtoto wake wa kumzaa.Ni mtoto wake wa kumzaa au ni mtoto wa kambo? Watoto wa kambo ni hatari kufanyiwa vitendo vibaya na baba wa kambo kama ndoa ikivurugika mababa mengine wa kambo hukomoa wake zao kwa kuwalala watoto wasiowazaa
Umbea tu wa Jamuhuri.Aliyeshitaki ni nani?
Ashazaliwa. Yuko fit.Kuna hatari ya huyo mtoto kuzaliwa akiwa ana ulemavu au matatizo ya kiafya kwa kuwa ni damu moja imetunga mimba hiyo
utata, baba wa mama ni babu na pia ni baba yakeAshazaliwa. Yuko fit.
Babu baba simpre.Mtoto atamuitaje mzazi ME .... Babu, baba au Babu Baba.?
Mtoto anakosa malezi ya baba na babu kwa pamoja,wakati uzembe ni wa bint,,miaka 25 unashindwa kusepa??umeshajua umenasa na unajua n ya baba yako unakosa cha kufanya??Kibaha. Hakimu Mwandamizi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Yudith Lyimo amemhukumu kifungo cha miaka 40 jela, na viboko 12 mkazi wa ‘Kwa Mfipa’ Kibaha, Fadhiri Msham kwa kosa la kufanya mapenzi na mwanawe wa kumzaa na kumpa ujauzito.
Mbali na adhabu hiyo pia Msham ambaye ni mtumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kama dereva, atatakiwa kulipa kiasi cha Sh4 milioni kama fidia kwa mwanawe huyo mwenye umri wa miaka 27, kutokana na kitendo alichomfanyia kilichosababisha kushika ujauzito na kupata mtoto.
Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatatu Mei 8, 2023 mahakamani hapo baada ya hakimu kuridhishwa na ushahidi uliotolewa wakati wa mwenendo wa kesi hiyo.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa Msham alitenda kosa hilo 2021 huko Kwa Mfipa wakati alipotembelewa na mwanawe huyo aliyekuwa anaishi maeneo mengine na mama yake mzazi.
Kwa mujibu wa mwenendo wa kesi hiyo ya jinai namba 23 ya mwaka 2021, imeelezwa kuwa baada ya kuletwa Mahakamani kwaajili ya kusikilizwa kipindi hicho; ilibidi iliondolewa ili kusubiri hadi mtoto atakapo zaliwa kwa lengo la kupata uthibitisho wa kipimo cha vinasaba (DNA).
Baada ya kuzaliwa mtoto ndipo shauri hilo lilirudishwa mahakamani kwa mara ya pili ambapo taratibu za kipimo hicho zilifanyika na kubaini kwa asilimia 99.99 kuwa Msham anahusika kumpa ujauzito mwanawe huyo.
MWANANCHI
SI KWELIKuna hatari ya huyo mtoto kuzaliwa akiwa ana ulemavu au matatizo ya kiafya kwa kuwa ni damu moja imetunga mimba hiyo
Wanaume Kwa kujitetea hamjamboNina wasiwasi sana na hili suala. Usikute kulikuwa na kutokuelewana kati ya wanandoa halafu mama na mtoto wakatumia mbinu za medani mtoto aende kwa baba yake ajilengeshe halafu akinasa wafungue kesi. Unahitajika uchunguzi wa kina hapa kwanza kujua wanandoa hawakuwa na ugomvi. Vipi wanandoa hawakuwa wanagombania mali kama nyumba, mashamba, n.k..
Kwa akili ya kawaida kabisa miaka 25-27 sio mtoto mdogo na ingetokea kabeba mimba ya baba yake bahati mbaya lazima angesepa kupoteza ushahidi ili baba yake asifungwe na kupoteza ushahidi na kumfichia aibu baba yake mzazi. Lakini kama katoa ushirikiano kwa polisi na mahakama basi huo ni mchongo wa huyo mtoto na mamayake. Ndugu wa mume shtukeni na mchukue hatua haraka ndugu yenu huyo wamemfix full stop.
Hakuna uhalisiaKuna hatari ya huyo mtoto kuzaliwa akiwa ana ulemavu au matatizo ya kiafya kwa kuwa ni damu moja imetunga mimba hiyo
Sio suala la kujitetea ni kufanya tu uchunguzi rahisi sana na kujiridhisha maana miaka arobaini aliyofungwa sio kidogo na hasa ikija kugundulika kuwa kulikuwa na ujanja ujanja nyuma yake. Ni kujua tu kama mke yupo hai na alikuwa wapi mpaka mzazi mwenzie? Wanandoa wanaishi pamojana ? Kuna ugomvi wowote kati ya wanandoa? Kuna mali zingombaniwa kati ya wanandoa? Je mtoto aliyepewa mimba ni mtoto halali wa huyo baba na wamempima DNA kumthibitisha isije ikawa baba kazaa na mtoto wake wa kufikia?Wanaume Kwa kujitetea hamjambo