Baba anahitajika sana kwenye familia, asipuuzwe! Nilikuwa naogopa kuwachezea mabinti nikisikia wana baba zao, nilijaribu kwa baadhi chamoto kilinikuta

Baba anahitajika sana kwenye familia, asipuuzwe! Nilikuwa naogopa kuwachezea mabinti nikisikia wana baba zao, nilijaribu kwa baadhi chamoto kilinikuta

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Nakumbuka hapo nyuma 2010 - 2015 kipindi nipo sekondari form 2 hadi 6 nilikuwa nipo active sana linapokuja suala la sketi, nilikuwa dunga dunga.

Ila pamoja na utukutu wangu huu nilianza kuwaogopa mabinti ambao wapo karibu na baba zao.

huko nyuma form 3 niliwahi kuwa kwenye penzi zito na binti wa form 2, mama yake alishanionya mara tatu ila nilikuwa nasahau baada ya siku chache tu narudi kwenye penzi, siku ya siku mshua wa binti tulikutana nahisi yeye ndie alienifatilia ntapita njia ipi, hakunipiga ila ile mikwara yake, sauti yenye kauli, jinsi anavyoonyesha kuwa tayari kumlinda binti yake kwa lolote, dah! kiukweli nilinywea.

Mwengine huyu ilikuwa nilipokuwa form 6, Nilimvusha mtoto wake kwenda geto, dem kafika kwao huko kakamatwa, ilikuja defenda pale nilibebwa mzobe mzobe bila nafasi ya kujitetea huku nakula mabao ya mgongoni, nilikaa kituoni mpaka saa tisa mchana bila kujua kinachoendelea, nilitolewa humo ndani nikiwa peku peku nikapelekwa chumba fulani.

Nikakutana na mshua wa huyo dem, wala hana maneno mengi aliniambia nachezea shilingi kwenye tundu la choo niachane na mtoto wake, nisije kulalamika. Yani hapo kituoni hata viatu nilichanganya nilikimbia.

Hali hii ilinifanya niwe makini sana kujaribu kufatilia backfround za mabinti naotoka nao, nilipokuwa nikisikia baba yake yupo alafu anamjali kusema kweli nilikuwa natafuta exit strategy.
 
Back
Top Bottom