Baba anataka kunidhulumu Nyumba yangu. Kesi bado inanguruma Mahakamani

Baba anataka kunidhulumu Nyumba yangu. Kesi bado inanguruma Mahakamani

Hiyo kesi utapoteza nakwambia, ila kama ukiendelea kupanic hivyo, keshi iko upande wako ila baba yako kakuzidi akili sana,
Haileti maana kuwa hujui ukubwa wa kiwanja chako na pia hujui fundi alieijenga, ata kama ipite miaka 40 lazima fundi wa nyumba yako pendwa akumbukwe sio vitu vya kuuliza, na ata ipite mda gan huwezi kusahau kuwa umenunua nyumba hiyo kwa nani, yawezekana kweli kiwanja ni cha mzee tangu awali na ww ulifatilia hati na kumtumia mzee hella ya kujenga kidogokidogo na hukuhusika direct kujenga
Kuna vitu vingine havisahauliki
Mzee kakushinda akili na utulivu, watu wengi wanaopanic ndo huwa mnapoteza kesi na huyo mzee anaonekana kabisa ana haki yake pia

Ata mchanganuo uliotoa pia umebase upande wako tu na ili tukuonee huruma, upande wa pili hujasema
Na pia hujatueleza stori nzima imekuaje
We kilichokuuma ni kukosa milion40 na si kuhusu mzee kuoa, kuuza viwanja vyake ni atapata hella kubwa sana kulko hyo na kutoa mahari na wenda ata hujui katoa sh ngapi

Kuna jinsi ya kuishinda hyo keshi nikikueleza, ila wacha mpambane maana mzee pia inaonesha ana haki yake, mtoto wa miaka 22 huwez ukawa umenunua kiwanja
Ata mzee akileta watu ishirini na moja ndo mmiliki kabla hutaweza kumtambua
 
Nyie Wazee mnatudhulumu Vijana wenu.

Mimi sikubali
 
Nchi inachezewa mpaka na wanaoheshimika. Sote tumekubaliana tuichezee nchi yetu.
 
Mwenyezi Mungu anasema ‘Waheshimu baba na mama upate…….,,
Hivyo hakunaga excuse yoyote ile kugombana na mzazi wako
 
Fundisho,
Vijana ukijenga jenga na usimruhusu ndugu kuishi wala kupanga, kwenye nyumba yako!
Utadumisha undugu hata kama ni kwa unafiki! Utaitwa majina yote kubali, Ila utakuwa na amani.
Kesi inafilisi kama kuuguza mgonjwa wa Cancer. Na makesi ya ardhi na familia ndiyo huisha mmoja akifa! Haziishagi
 
🙏🙏🙏
 
BABA ANATAKA KUNIDHULUMU NYUMBA YANGU. KESI BADO INAENDELEA MAHAKAMANI.

Anaandika Robert Heriel.

Namheshimu Kama Baba yangu, ni mzazi wangu. Nilikuwa nampenda lakini sasa naona chuki inamea nafsini mwangu.

Kisa Mimi mtoto wake ndio anikandamize, anidhulumu Mali yangu. Ananinyang'anya Nyumba ili Mimi niishi wapi.
Yeye Kama Baba alipaswa aniachie Urithi, kuichukua Nyumba yangu ni uonevu. Na sipo tayari Kwa hili.

Baada ya kuhamia Dar nilirudi Makanya kuuza Nyumba yangu, yenye hati yangu kabisa, ambayo ndani yake alikuwa akiisha Baba na wadogo zangu. Nilifanya hivi baada ya Baba kuuza viwanja vyake ambavyo nilitegemea angewapa wadogo zangu Urithi, sasa kaviuza ili apate mahari ya kuongeza mke mwingine ambaye ni Mama Mdogo yetu.
Sikatai Baba yangu kuoa mke mwingine lakini nimechukizwa na Kitendo cha Baba kuuza Mali alizochuma na Mama yangu, ati ili apate mahari za kuoa mke mwingine.

Nikawaambia wadogo zangu wawili, nitauza Ile Nyumba kisha tutaamia DSM, Madalali wakaingia mzigoni, wateja wakamiminika, mpaka aliyefika Bei, Nyumba tungeiuza Kwa 40Milioni. Lakini Baba hataki niiuze Nyumba yangu mwenyewe.

Tukaenda Mahakamani, hapo ikaamrishwa Hati itolewe ya Nyumba, nikaitoa hati ya Nyumba yenye Majina yangu, mahakama ikatoa uamuzi kuwa Nyumba ni yangu.

Lakini Baba akaiomba Mahakama ahojiane na Mimi. Mahakama Kwa kutaka kumsikiliza na kumtendea haki Baba, ikaruhusu mahojiano baina ya Baba na Mimi; na hivi ndivyo ilivyokuwa;

Baba; hujambo mwanangu!
Mimi: Sijambo, shikamoo Baba.
Baba: Iambie mahakama unaitwa Nani?
Mimi: Naitwa Robert Ng'apos Heriel
Baba: Mr. Robert unamiaka mingapi?
Mimi: Nina miaka 32
Baba: hongera Sana Kwa kumiliki Nyumba ukiwa kijana Mdogo.
Mimi: Kumiliki Nyumba ni mipango tuu.
Baba: Ulianza lini kuwa na mipango ya kujenga Nyumba nzuri Kama Ile?
Mimi: muda mrefu tuu.
Baba: Kama miaka miangapi hivi?
Mimi: miaka 10 iliyopita?
Baba: Unafanya kazi gani Mr. Robert?
Mimi: Ninafanya biashara na ujasiriamali.

Baba: Biashara inahitaji miaka mingapi ili isimame?
Mimi: Inategemeana,
Baba: unauzoefu wa biashara wa miaka mingapi?
Mimi: miaka Saba sasa.
Baba: Uliwahi nitumia hata Mia ya matumizi?
Mimi: Nakutumiaga mara moja moja, Ila ni hiyari yangu kukutumia, hakuna sheria inayonilazimisha kufanya hivyo.

Baba: nakumbuka nilikupeleka shule ya Msingi ukiwa na miaka saba? Je ulimaliza chuo ukiwa na miaka mingapi?
Mimi: umesahau, nilianza shule ya Msingi nikiwa na miaka sita na nimemaliza shahada ya Kwanza nikiwa na miaka 22

Baba: wakati unasoma shule ya sekondari ulikuwa unaishi wapi?
Mimi: nilikuwa naishi Makanya.
Baba: Ulikuwa unaishi Kwa Nani? Kwenye Nyumba ipi?
Mimi; kimya
Hakimu; Jibu swali
Mimi: Nilikuwa naishi Kwa wazazi wangu
Baba: Wazazi wako ni kina Nani?
Mimi: Lakini...!
Hakimu: Hakuna cha lakini jibu swali.
Mimi: Baba na Mama
Baba: Kwenye Nyumba ipi?
Mimi: Nyumba ya matofali
Baba: anacheka
Baba: anyway! Nyumba unayosema ni yako unajua ukubwa wake wa kiwanja ni ngapi Kwa ngapi?
Mimi: (Nafikiri kidogo alafu najaribu kukipima kiwanja cha nyumba yangu akilini) Nafikiri ni 30*40
Baba: Una uhakika
Mimi: Kama sijasahau nafikiri hivyo.
Baba: wakati unajenga nyumba yako hiyo, bei ya tofali ilikuwa shilingi ngapi miaka 15 iliyopita? Na imebeba tofalo ngapi mpaka kupaua?
Mimi: Mimi sio fundi, nilitoa tuu hela ikajengwa.
Baba: unaweza nieleza upana wa madirisha na milango ikiwa ni nyumba yako?
Mimi: nimeshasema Mimi sio fundi. Hati inajieleza maswali yako hayana umuhimu wowote.

Baba: Mhe. hakimu, naomba Mwanangu Robert atuambie alinunua kiwanja kile kutoka Kwa Nani na mwaka gani?
Mimi: nilinunua miaka kumi iliyopita,
Hakimu: kutoka Kwa Nani?
Mimi: Kimya!

Hakimu: Sasa utaithibitishia vipi mahakama hii ni Mali yako?
Mimi: Mhe. Jaji, uthibitisho mkubwa wa uhalali WA umiliki WA nyumba ni Hati, hati hii ndio kielelezo cha muhimu kuliko maelezo ya mdomoni.

Baba: Mhe. Hakimu, Nahitaji Robert amlete fundi aliyeijenga nyumba yake, Mimi nimekuja na mashahidi akiwemo Aliyeniuzia kiwanja pamoja na Fundi aliyejenga nyumba yangu hiyo.

Mimi: HAO ni mashahidi wa uongo, hata Mimi ningeweza kuleta mashahidi hao, ungeleta hati ya mauziano ya kiwanja na aliyekuuzia mahakama huende ingeweza kushawishika, hao mashahidi ni wamchongo.

Baba: Mhe. Hakimu, Nyumba nyingi za kijijini hazina hati, nyumba yangu Kama zilivyonyumba nyingi za Makanya na vijiji vingine Tanzania hazina hati, mwanangu huyu alifanya hila na kuja kuikatia hati nyumba yangu Kwa majina yake, Ila nyumba ni yakwangu mhe. hakimu.

Baba: Mhe. Hakimu, huyu kijana kamaliza Chuo juzi tuu hapa, haya hizo biashara anaozifanya bado hazijatengemaa, Hana uwezo wa kujitegemea achilia mbali kujenga nyumba nzuri Kama yangu ambayo ameiandika jina lake kwenye hati ya Nyumba yangu.

Mimi: Baba nikuulize Swali?
Baba: Uliza tuu mwanangu.
Mimi: Hii ni nini?(nikiwa nampelekea)
Baba: Ni hati ya Nyumba.
Mimi: embu soma jina la mmiliki
Baba: Robert Ng'apos Heriel
Mimi: huyo Robert ni wewe?
Baba: Hapana ni wewe mwanangu, lakini..
Mimi: Hakuna cha lakini.

Hakimu anahairisha kesi mpaka February 3

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Makanya
Tatizo liliyopo hapo Ni kwamba umejenga nyumba kwenye kiwanja Cha Baba yako,Kisha ukazunguka kukikatia hati,hesabu umeumia.
Siku hizi umehama mvomelo Morogoro?
 
Back
Top Bottom