Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Queen Darleen mwenyewe anamuita diamond baba unategemea ndo atamsaodia mzee?
Kifupi Ni kwamba siku mama diamond akiamua kumwambia diamond amsamehe baba yake atamsamehe.
Moyo utalaini bila nguvu Ni simple tu mama kuplay party yake
Sasa kwanini hamlalamikii Darleen au yeye hajamkosea?
Kuna sababu siyo rahisi kijana amtelekeze hivi mzee wake anavyopenda sifa kwa jinsi anavyosemwa angekuwa ashamsaidia huenda kuna kitu huyu mzee alifanya kikamuumiza sana
 
Watajaza wenyewe na maisha yao. Ila niseme tu huyo baba awache kulalamika kwenye vyombo vya habari sababu suluhu haipatikani huko.
Huyu baba anaonekana ni mtu mwenye nguvu za kufanya kazi. Nadhani anaendekeza mteremko. Hivi kama huyo mwanae asingefanikiwa ni nani angemsaidia! Si ajabu ungekuta anaendesha maisha yake vizuri kabisa lakini kwa sasa kwa vile ameshakuweka mawazo yake kwenye ''utajiri wa mtoto'' na akili zake zinajikuta zikiuambia mwili wake uumwe na ajisikie kama hawezi kufanya chochote.
 
Akianza kuwa mahututi ndio watajifanya wanampeleka India. Ila dingi nae anafeli si achukulie Kama Hana mtoto tu
Hii ndio point yeye si kakataa nae dingi akamtae tu maana hawa mama zetu ni miyayusho kama mama anapenda vitoto sababu ya dingi kupiga chini ni halali Kabisa
 
Ila hii ni roho ngumu.
Siku ya kuzaliwa kagawa zawadi na kafungua mradi wa bodaboda kwa watu wa Tandale, baba yake hamjali?

Ingekuwa mwanamke labda ningeelewa katekwa na mama yake, ila yeye ni mwanaume tena ana tabia za ufuska kuliko alivyokuwa kuwa huyo babake anashindwaje kuelewa kuna wakati mwanaume akishikwa na mwanamke mjanja yuko radhi hata kutelekeza familia.
Hebu acheni kuongelea mambo ambayo hamyajui undani wake. Wewe Kama baba usipomjali mtoto wakati ukiwa mdogo usitegemee yeye akujali ukiwa mzee.
Siku zote mtu huvuna alichokipanda. Na hii iwe funzo kwa wazazi wote wazwazwa..hasa wababa
 
Sasa kwanini hamlalamikii Darleen au yeye hajamkosea?
Kuna sababu siyo rahisi kijana amtelekeze hivi mzee wake anavyopenda sifa kwa jinsi anavyosemwa angekuwa ashamsaidia huenda kuna kitu huyu mzee alifanya kikamuumiza sana
Mkuu nadhan analalamikia uhisiano wake na diamond Kama baba na mtoto Wala sio ishu ya kusaidiwa Queen Darleen hajawahi kulalamika alitelekezwa Kama diamond na mama yao Ni tofauti
 
Mkuu nadhan analalamikia uhisiano wake na diamond Kama baba na mtoto Wala sio ishu ya kusaidiwa Queen Darleen hajawahi kulalamika alitelekezwa Kama diamond na mama yao Ni tofauti
Huwezi kuforce mahusiano kwakuwa mahusiano hujengwa uwa hayaji tu hivi hivi... Kama hakuyajenga ndo matokeo yake hayo... Sijui Diamond angebaki kuwa maskni mzee angekuwa anahitaji hayo mahusiano
 
Mkuu nadhan analalamikia uhisiano wake na diamond Kama baba na mtoto Wala sio ishu ya kusaidiwa Queen Darleen hajawahi kulalamika alitelekezwa Kama diamond na mama yao Ni tofauti
Issue ya kukatiwa bima kwa Nini watoto wengine wasifanye hivyo? Huyu mzee Hana ndugu Kila siku kumlaumu mtoto? Unadhani kwa hizo lawama hata km diamond anampango wa kumsamehe atafanya hivyo.
Hlf kwanini alalamike Kila wakati, amuachie Mungu apambane na hali yake.
 
Baba hata kama ana matatizo au mwovu kiasi gani ni baba tu
Ugomvi wa wazazi mtoto haukuhusu
Wajali wazazi wako wote wawili wawapo hai kadri ya uwezo wako.
 
Kuna mzee kamwita mwanae kwenye reality TV talk show kumuomba msamaha na anataka wawe na uhusiano kama baba na mwana. Akaanza kuelezea sababu iliyomfanya amtelekeze yeye na mama yake, akasema alikuwa kijana mdogo na asingeweza kuwahudumia kwa vile alikuwa hana kazi.
Kijana akamuuliza mzee, sasa hivi anafanya kazi gani? Mzee akajibu nimeshakuwa mtu mzima, sifanyi kazi.
Kijana akamwambia mzee, ulitutelekeza kwa vile huna kazi sasa ulivyorudi nilifikiri ushapata kazi?

Sasa ndio haya. Ujana wako ulikuwa wapi, mimi unijie uzeeni?
 
Apo nacho kiona ni mama ali mrisha sana sumu mtoto... ndio maana mtoto hawezi kumwelewa dingi... shida itakuja uyo mzeee aki kata moto
 
Mtoto yoyote yule ambae amelelewa na mzazi mmoja bila kuwa na hekima ya MUNGU ni lazima mahamuzi yake yatakua mabaya juu ya tofauti za wazazi wake zilizowaikutokea siku za nyuma wakati yeye alikua hajifahamu ,na hii tampelekea kuishi maisha mabaya na yenye majuto baada ya mzazi aliedhani ni mbaya kutoweka duniani .
Huu ni ushauri kwa sisi sote tuliopitia maisha au malezi ya namna hii tusipende kuhukumu upande mmoja ilihali hatujui nini chanzo hasa cha tofauti za wazazi wetu wote kupelekea kuisha tulivyoishi .
Balance maisha kwa wote baraka zitaambatana na wewe namaanisha baraka za kweli sio baraka hizi za Mali

Maana MTU ukizungumzia baraka akili na mawazo yanakimbilia kwenye Mali

Ambacho kimemtokea Diamond ndo kinachoendelea kati ya yeye na mtoto wake na Hamisa mobeto
Hizi mambo usipoziweka sawa huwa zinatambaa vizazi hadi vizazi na wale watoto anaodhania watakua wema kwake ndo ambao watakosa msaada kwake kabisa na yule hasiemdhania ndo atakuja kuwa msaada kwake . nimeshuhudia haya Mimi mwenyewe ubaguzi sio mzuri kabisa na roho ya kisasi inamtesa zaidi mwenye kisasi kuliko anaefanyiwa kisasi hicho
Mapigo yanaendaga kwa kizazi chake na vizazi vijavyo.

Cha msingi hapo ni

Kusamehe
Kusahau
Na kurejesha nafasi ya MTU aliekukosea kuwa kama ya awali ,hapo ndipo tunaposem MTU kasamehe au kasamehewa
 
Ikifikia hapo atakua amechelewa..! Watoto anza nao wakiwa wadogo
Kaka unagalia na nature ya kazi yenyewe sasa wewe unataka afanye nini,alafu kazi yake sio kwamba kila siku atakuwa yupo bize kuna kipindi mziki atadrop atakuwa karibu na familia yake sasa hivi ni wakati wake wakutafuta hela kazi nyingine hizi ni za msimu.
 
Sasa kwanini hamlalamikii Darleen au yeye hajamkosea?
Kuna sababu siyo rahisi kijana amtelekeze hivi mzee wake anavyopenda sifa kwa jinsi anavyosemwa angekuwa ashamsaidia huenda kuna kitu huyu mzee alifanya kikamuumiza sana
Mwenyewe nashangaa mbona hamlalamiki Dorleen ?Queen kwenye kipindi cha Shilawadu alimbwenga mpaka matusi mpaka wakawa wanayaminya.
 
Mkuu nadhan analalamikia uhisiano wake na diamond Kama baba na mtoto Wala sio ishu ya kusaidiwa Queen Darleen hajawahi kulalamika alitelekezwa Kama diamond na mama yao Ni tofauti
Kuna kipindi fulani Shilawadu Baba Diamond ashawahi kumlamikia Queen hamjali na Queen akamtukana mpaka matusi kwenye simu wakawa wanaminya,sasa jiulize mtu kama Queen angekuwa yupo vizuri na baba yake asingemtukana vile.Huyu mzee akubali yeye ni tatazo haiwezekani uwe na tatizo moja la malezi kwa watoto wawili tofauti .


 
Tena inabidi diamomd aanzishe kampeni ya kuwanyoosha hao "sperm donor" wanaodonate sperm na kukimbia halafu wanajifanya kumtambua mtoto akishatoboa..

Imagine diamond angekuwa mvuta bangi kitaa mzee angejifanya kumjua.
Kama alimchukulia poa utotoni kwa nini anajileta sasa?
Yaani me pia nimewaza hivi ...hivi mond angekuwa fukara tu huyu mzee angesema diamond mwanangu kila Mara? Kama anataka mtoto amtunze na yeye angemtunza tangu kipindi hicho..hawa wazee wa hivi waantia hasira sana
 
Back
Top Bottom