Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Baba Diamond aomba mwanae amkatie angalau bima ya afya

Lakini huduma anatoa. Alafu Diamond sio kwamba atakuwa busy au namba moja milele Kuna kipindi mziki utamkataa na atakuwa karibu na watoto wake zaidi. Juma nature yule enzi zake alikuwa busy, sasa hivi yupo analea mtoto wake.
[emoji38][emoji38][emoji38]sir nature kibra analea sio
Diamond muda wa kuwalea watoto wake Ni Sasa kwasababu siku zijazo ataoa automatic atakuwa bize na mke na watoto wake wajao kwa mkewe. Wale wa sasahivi muda was ndo huu ukipita alafu akioa wale ndo imekula kwao ukaribu ndo utapungua zaidi
 
Mkuu hapa tunaongea na kuelewana Kama watu wazima ndo maana unaona inawezekana watoto watamuelewa Diamond kutokana labda na ubize wa kazi yake ila trust me
Mama akikaa na mtoto wake kashapata akili Apo mfano Zari kakaa na mwanae anamsimulia kipindi anakuwa jinsi alivyokuwa anamsumbua kwenye malezi labda kuumwa usiku yeye pekee yake anaangaika baba yupo bize na kazi huku machozi yanamtoka unadhani dogo atamuelewa mshua?
Dogo anataona Dingi alikuwa sio.
Unangalia na nature ya kazi sasa mondi ana show na sasa hivi yupo hot, unataka aache show akalee mtoto au dereva wa Lori ina maana utageuza ukampeleke mtoto hospitalini, wakati malezi ya mtoto yanategemea kazi yako, huu mondi ni wakati wake wakutengeneza hela.
 
Ampotezee vipi wakati hajawahi kuwa na ukaribu naye ?
Toa akili zako fupi hapa, wewe mwenyewe hujawahi kukosea Watu wanaokuzunguka?

Kila ulichowakosea walikuadhibu na kukataa kabisa kukusamehe?

Hivi kwanini wakati mwingine mnaropoka tu ilimradi muonekane mmechangia mada hata kama hamna hoja za msingi?
 
[emoji38][emoji38][emoji38]sir nature kibra analea sio
Diamond muda wa kuwalea watoto wake Ni Sasa kwasababu siku zijazo ataoa automatic atakuwa bize na mke na watoto wake wajao kwa mkewe. Wale wa sasahivi muda was ndo huu ukipita alafu akioa wale ndo imekula kwao ukaribu ndo utapungua zaidi
Hivi Majizo amezaa watoto wangapi na kwa wanawake wangapi na sasa hivi anajiandaa kumuoa Lulu, ina maana akimuoa Lulu ndio kapoteza upendo kwa watoto wake. Kiba kuzaa na wanawake watatu tofauti kaoa mwanamke mwengine ina maana kiba kapoteza upendo kwa watoto wake. Manake nakuona unatia ugumu upande wa Mondi, manake unavyo ongea utazani Mondi ndiye wa kwanza kufanya hivyo.
 
Akifanya mahojiano na gazeti mwananchi baba mzazi wa msanii diamond platnumz ambemuomba mwanae angalau amkatie bima ya afya kwani Hali yake kwa Sasa sio nzuri. Ilinichukua muda kumshawishi na baadaye kufanya mahojiano na Abdul Juma Isack ambaye ni baba wa msanii wa maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz. Ungeweza kukata tamaa ya kuendelea kumshawishi kwa sababu ana hoja nyingi na pengine nzito.

“Sioni mabadiliko kwangu,” anasema baba huyo mwenye umri wa miaka 52 wakati akieleza sababu za kukataa kufanya mahojiano. “Tangu nianze kuhojiwa, nilikuwa nikiamini kuwa ningeweza kubadili msimamo wa mwanangu anayetajwa kuwa msanii tajiri namba moja Tanzania. “Badala yake naonekana kama nalilia kusaidiwa na mtoto wangu. Pamoja na kuwa na mtoto maarufu ndani na nje ya nchi, maisha yangu ndio kama hivi unavyoyaona. Naishi Magomeni Kagera na nyumba yangu ya kawaida tu, ambayo naamini hata siku Diamond akikwama kimaisha atakuja kuishi kwa kuwa hapa ni kwao, japokuwa simuombei hilo.”

Abdul anasema kwa muda mrefu Diamond amekuwa hafanyi mawasiliano naye na hajui sababu . “Najiuliza ni nini kikubwa namna hiyo nilichomkosea?” anahoji baba huyo. “Ninatamani siku moja nikutanishwe katika mahojiano na Diamond na mama yake ili kila mmoja atoe alilonalo moyoni.“Huyu mtoto kanipa majina mengi kutokana na yanayoongelewa mtaani kwamba nilimtelekeza, wakati hakuna ukweli wowote. Mimi niliachana na mama yake wakati akiwa kidato cha kwanza.

Kwa umri hu alikuwa anajielewa na anajua sababu za kuachana kwetu. Kama kuna jingine wanalolijua wao kwamba nimewakosea, basi tuhojiwe hata mbele za watu ili lifahamike na kuyamaliza kuliko hiki wanachofanya kwangu. “Kasababisha kila kona ninayopita nanyooshewa vidole kuwa niliwatosa. Ifike mahali haya mambo tuyaweke sawa kwa kuwa naumia sana, hawajui tu. Si kwamba, labda ni kwa kutaka msaada wao, hapana. Bali kila mtu awe ameitakasa nafsi yake na kuondokana na vinyongo.”

Baba huyo wa Diamond anasema hata mawasiliano na mzazi mwenzake ni pale anapojisikia. “Tena wakati mwingine na maneno ya karaha, lakini ana afadhali kuliko mtoto ambaye mara ya mwisho tuliwasiliana akiwa na Wema Sepetu ambaye alikuwa akija naye hapa mara kwa mara kunisalimia,” anasema.

Kwa sasa maisha si mazuri. Abdul anajihusisha na biashara ya viatu. Huchukua viatu kwa malikauli katika soko la Karume na kuvipeleka kwa wateja wake mahali walipo. “Lakini maisha kwa sasa si mazuri kwa kuwa nasumbuliwa na tatizo la miguu. Inanifanya wakati mwingine nishindwe kutembea muda mrefu,” anasema mzazi huyo.“Kama unavyoniona miguu inaniuma na wakati mwingine nashindwa kuinuka hata kitandani.

“Naona ni wakati sasa na mimi kuwa na eneo la kufanya biashara hii, lakini ndio hivyo uwezo, walau ningekuwa na gari ningeweza kuzunguka nalo hata kwa kuendeshwa ili nisiwapoteze wateja wangu, lakini sina namna.” Anasema hata uwezi wa kugharimia matibabu, hana. “Labda ningekuwa na bima ya afya ingekuwa msaada kwangu lakini ndio hivyo sina,” anasema.
Apata msaada mtandaoni

Hata hivyo, msaada wake mkubwa uko kwa mtoto wake wa hiari anayeishi London, Uingereza anayeitwa Zubeda. Walijuana na mtoto huyo katika mitandao ya kijamii baada ya kuona mahojiano yake akielezea maisha anayoishi.


Mwananchi sourceView attachment 968793
nasikia huruma sana, mara nyingi wazazi wakihitilafiana chuki hujengwa kwa watoto.huyu mzee aondoe malalamiko aendelee na maisha yake, kijana naamini ameumbwa iko siku tu mtaniambia kama ana roho ya kibinadamu atamkumbuka. mzazi ukizaa usitegemee mtoto atarudisha upendo au fadhira chapakazi mzee achana na malalamiko shida zipo kabiliana nazo mungu atakusaidia. je inakuwaje kama usingekuwa na mtoto wa hivyo ungelalamika kwa nani.komaa tunakuombea kwa mungu atakusaidia
 
Hivi Majizo amezaa watoto wangapi na kwa wanawake wangapi na sasa hivi anajiandaa kumuoa Lulu, ina maana akimuoa Lulu ndio kapoteza upendo kwa watoto wake. Kiba kuzaa na wanawake watatu tofauti kaoa mwanamke mwengine ina maana kiba kapoteza upendo kwa watoto wake. Manake nakuona unatia ugumu upande wa Mondi.
Alafu majizo na kiba jinsi wanavyoishi na maex wake Ni tofauti na diamond, Diamond anaacha kwa kebehi na madharau hivi unadhani mtu Kama Hamisa amuachie mtoto akaishi kwa Diamond?
 
Alafu majizo na kiba jinsi wanavyoishi na maex wake Ni tofauti na diamond, Diamond anaacha kwa kebehi na madharau hivi unadhani mtu Kama Hamisa amuachie mtoto akaishi kwa Diamond?
Hivi ww unajua maex wa Kiba, Kiba anaishi nao vipi? Mwishoni wakati akielekea kuoa Kuna ex wake mmoja akalamika kiba hatoi hela ya matumizi na familia yao haimwangalii au unajua Majizo na maex wake wanaishi vipi au kwa kuwa unaona wapo kimya ndio unazani wapo shwari.
 
Hivi Anavyolalamika Mzee Wangu Hapo Kuhusu Utajiri Wa Mwanae Usiomnufaisha Kwa Chochote Niombe Kuuliza Je Ingetokea Mondi Asingekuwa Maarufu Wala Asingekuwa Tajiri Huyu Mzee Angemlalamikia Nan Au Angeishije Bila Kufanyiwa Interview Na Waandishi Wa Habari Km Wote?
 
Toa akili zako fupi hapa, wewe mwenyewe hujawahi kukosea Watu wanaokuzunguka?

Kila ulichowakosea walikuadhibu na kukataa kabisa kukusamehe?

Hivi kwanini wakati mwingine mnaropoka tu ilimradi muonekane mmechangia mada hata kama hamna hoja za msingi?
Wewe zwazwa nani kakuambia kuna mtu kakataliwa kusamehewa ???

Umetoka kula gambe unadandia train kwa mbele.
 
Walahi,sijui kwa nini nahisi dogo domo kalishwa maneno na lenyewe lilivyo puuzi kakubali,
Yaani baba mzaz anateseka hv wakati wa2 tunaombea hta baba zetu wafufuke no matter what happened km tuliwahi kukwaruzana.
Pumbavu kabisa diamond,SHAME ON YOU!!!
Yaani bhas tu,this is so stupid at its best, last time 2po nae mexcana diamond nltamani hta nimchane amalizana na babake sio eti baadae mzee arest n peace ndo wakatafute kiki msiban.
bigUp mrembo zu kwa kumtek care mzee,ila hii ishu sio poa kabisa,washauri wa domo mpeni good advise kwnye hili,wengine sisi ni wapenzi watazamaji.
 
Huyu mzee ni mpuuzi sana...[emoji16] [emoji16]
Yaani kila anapo taka kupaza sauti, ni lazima aongee na watu wa media...[emoji55] [emoji55]
Na mbaya zaidi ni kwamba anajiskaha kama hao wanao muhoji ni watafuta fursa. Yaani wanatumia jina la Diamond na kumuhoji baba yake, kisha wanaanika kwenye public ili wapate pesa....[emoji57] [emoji57]
Ww naye akili ka piliton hivi yeye ndo kawaita au wenyewe ndo wamemfata kumuhoji au ukitaka asifanye mahojiano. Punguani wa head ww.
 
Back
Top Bottom