Hasty generalization kabisa hii.
Hivi hujiulizi JKN kahudumu miaka 24
AHM miaka 10.
BWM miaka 10.
JK miaka 10.
Na JPM miaka 5 unusu .
Kati ya wote hao kibinadamu wote wana mapungufu hata mazuri yao ila haiondoi chama walichopo/kuwepo kimetufikisha hapa tulipo na ninakichukia hasa.
Tuje kwa JPM aliyehudumu kipindi kifupi kupita wote hujiulizi kwanini ndio anasemwa vibaya kuliko wote je watu wanaomsema unafikiri kila kitu wanatunga japo vya kutunga kuhusu ubaya vipo ila vyenye ukweli vipo mfano hebu kumbuka kauli hii
"Mkimchagua mpinzani sileti maji" je unadhani watu wote wa pale Tunduma watampenda JPM kwa kauli hii?
Hebu angalia hapa wanahabari na hata wakosoaji waliomsema walivyopigwa mkwara mzitohttps://www.reuters.com/article/us-tanzania-media-idUSKBN16V25S
Je unafikiri kama aliwakata kumsema akiwa hai sababu aliwatisha wataacha kumsema akiwa amekufa.
Watu kama Ben Saanane , Azory Gwanda na Tundu Lissu walifanyiwa ukatii katika awamu ile na wengineo wengi walio hai , waliopotezwa bila kujulikana , waliokimbilia uhamishoni unataka wampende kama unavyompenda usiwanyime haki yao ya kutokumpenda pia.
Mwisho tu mjiulize kifo cha JPM na Mkapa kilitofautiana miezi 10 tu ila kwanini humu hakuna thread za kumnanga Mkapa ambaye alihudumu miaka 10 na JPM miaka 5 unusu?