Baba JPM hajafa ila amelala ufunguzi wa ikulu leo alikuwepo japo hakuongea😭🤐

Kuna vitu vinashangaza pale watu wanapokumbushwa na kusisitizwa kusoma na kuyatafakari mambo kwa kina ila huleta kebehi. Huyu mtu hata kama ana ubaya unaosemwa, vipi tahadhari aziletazo kwanini kuipuuza!? Mara ngapi tahadhari zake zimekuja kuwa kweli harafu ushupaze tu shingo kuwa huyu ni mbaya? Hivi mtu ukiamini ni mbaya na anauwezo wa kukufanyia ubaya ila anakuonya kwanza, busara ni kumkimbia ubaya usikupate au kushupaza tu then ubaya ukukute!? Bahati mbaya ni kuwa ubaya ukikupata tutaishia kusema na kumsema mbaya ila za zaidi hakuna.
TUSIMPUUZE HUYU MTU.
 
Kwanza naunga mkono yote uliyosema hapa, naomba nami kupitia hapa niongeze machache kuhusu mapungufu ya tukio la jana...
Moja, Hivi ni kwa nini hakukuwepo watoto wetu yaani wanafunzi wa shule na vyuo, tena pengine ilitakiwa wawepo kuanzia wale pre nursery..kwa sabab ikulu ni urithi wao na si wa hao walioalikana, tunashindwa kuonyesha thamani ya uwepo wa watoto wa Taifa hili kwa nini lakini..kuna faida gani kumualika Mpoto na Bella ili hali kila leo tunawaona na wanayosema wala si mageni masikioni mwetu, wangealikwa wanafunzi shule hata 3 tu wakaimba nyimbo nzuri kwa niaba ya wenzao ingeleta furaha, baraka na faraja, watoto mahali popote wana nafasi ya pekee, hata penye mifarakano watoto huleta mapatano..kama tunawatoa watoto kwenye matukio muhimu kama la jana, hivi ni wapi tena tunaweza kuwafundisha kupenda taifa lao, kujitegemea, utii, kupenda vitu vya kwetu nk, wapi??
Tatizo kubwa la wasaidizi wa viongozi kwanza ni mentality ya anasa, pili uchovu wa akili na ulevi wa kuaminiwa! Mambo mengi sana wanatukosea tena mara kwa mara..hivi kuna mzazi huwa anahangaika wakati wa sherehe za kiimani kuandaa mavazi, chakula, mapambo kwa ajili ya wageni halafu watoto wako wachafu, hawajaandaliwa kushiriki pasaka au idd, ndio hivyo kweli? wageni wanaojitambua wakikuta hali ya namna hiyo watatoa udhuru wa kuondoka mapema wakuachie hayo yote uliyoandaa utumie peke yako! Sababu utakuwa umekosea pakubwa mno! Watoto wanapaswa kuwa waalikwa namba moja!
Kuonyesha uungwana waandaji mtutake radhi tafadhali, sisi hatutoi kodi yetu zitumike kufadhili anasa za watu wazima kama sisi!
Jambo la pili, Mh. Rais alisema itajengwa complex ikulu hadi viwanja vya gofu, hivi jamani kwa nini tuna fikiria sana burudani kuliko kazi? Ikulu ni sehem ya kazi, hayo mengine yote ya nini? Tuna uhakika gani baada ya miaka 40 ijayo watakaokuwepo watatumia? Haina haja kabisa, hivyo ilivyo inatosha, madam nafasi ipo ya kutosha, huko mbele kama wataona hayo ni ya maana wataweka wao, hata mzazi anapojenga nyumba huweka vile vitu vya msingi tu, siku hayupo yule atakayerithi akiona anayotaka yeye yanakosekana ataweka yeye ili pia awe na uchungu wa kutunza, ukiweka kila kitu unaweza jikuta unapoteza nguvu, muda na rasilimali bure sabab siku haupo hakuna atayetumia tena, sasa si bora nguvu ulizotumia ungetoa sadaka zisaidie wahitaji..tusiweke mbele sana mtazamo wa kuonyesha ufahari hata kama haihitajiki..TUJIREKEBISHE!
 
Kama kuna mtu mpumbavu niliyewahi kukutana nae hapa jamii forums wewe ni namba moja! nani aliyekwambia kutokukubaliana na mtu ni kumpinga?kuna binadamu ambae amekamilika?pita hivi...
 
😊⁉️
 
Reactions: Tsh
Usinitishe. Enzi za giza za kutishana ziliondoka na yule fascist wenu. Ujue na wewe hujui unasema niende Mahakamani kwa utaratibu gani wa.kisheria za nchi hii?
Hadithi ya nyoka alie angukiwa na msumeno sijuwi kama umewahi kusoma. Punguza jazba ktk kuujuwa ukweli. Nasoma mabandiko yako naona kama nyoka alie amua jiviringisha kwenye msumeno ulio muangukia akafa kwa hasira zake.
 
Vipi kuhusu Ben Saanane, Mzee alimfanya nini?
 
Kaunda ni Baba wa Taifa wa Zambia ambapo hapa Tanzania Baba wa Taifa ni Nyerere.
 
Katibu Mwenezi na Itaki mpya wa CCM Komredi pcm kama msemaji wa chama mwenye uthubutu na baada ya kutembelea Chato na Butiama ukapewa baraka za uongozi wito wa wananchi wa Tanzania kipenzi cha JPM wnnataka uchunguzi wa kifo chake cha utata tena wanasema kama utanyamazishwa kwa sababu zozote kusudio lao halitakufa hadi kizazi cha nne kwa kuwa watuhumuiwa wapo mitaani

Ujumbe ukufikie Komredi @ Paul Christian Makonda #KifotatachaJPM
 
Kweli kabisa
 
Mkuu TumainiEl , naunga mkono hoja,
JPM yupo Nikimwangalia Makonda, mambo anayoyafanya namuona kama Magufuli
P
 
John Pombe Magufuli aliishi, anaishi na ataendelea kuishi, japo mwili wake upo ardhini. Viongozi wengine waliishi na kisha wakafariki mwili, roho na fikra.

Hayati Rais John Pombe Magufuli ,tunakukumbuka sana, kwa sababu ya uadilifu, ukweli kwa nafsi yako, upendo wako wa kweli kwa Taifa lako.

Kama walivyo wanadamu wote, pamoja na mengi mazuri uliyoyatenda, yawezekana kuna mahali ulipungukiwa,kama alivyowahi kunena Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere;-

"Tulifanya mazuri lakini tulifanya makosa pia. Tusifanye makosa, sisi ni malaika?"

Mungu wetu, uliye tajiri wa msamaha, pale mtumishi wako alipopujgukiwa, umjalie John Pombe Joseph Magufuli msamaha kamili ili naye awe miongoni mwa watakatifu wako, wanaoizunguka meza yako, wakikusujudia na kukusifu usiku na mchana, na sala zake zikalete baraka kwa Taifa la Tanzania alilolipenda bila hila bali kwa moyo uliokamili usio na unafiki. Tunaomba uliepusha Taifa lako dhidi ya viongozi wanafiki na walaghai wanotaka waliongoze Taifa lako kwa hila, uwongo, vitisho na ulaghai. Huo uovu waufanyao, ukawe adhabu yao ya Duniani na Mbinguni.
 
Remembering Ben Saa nane..
Magufuli hakuwahi kumjua Ben Saanane,hata ungemuuliza Ben Saanane ni nani hasingemjua sembuse kupotea kwake,Kubenea aliandika kwenye gazeti la Mwanahalisi kwamba Ben Saanane yupo anadunda mtaani,anaonekana kwenye vibanda vya kahawa,akasema uwa anakuja kumwekea ujumbe chini ya mlango wa nyumba yake,Hilda Newton aliandika kwenye account yake alisema Ben Saanane ametumwa na Mbowe kwenda Afrika kusini,sasa sijui wahuni wanamwingiza vipi Rais Magufuli,wapo wanasema eti Ben Saanane alihoji PhD ya Magufuli,sasa niulizie je UDSM ilitoa PhD feki?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…