PreGE2025 Baba Levo ajitosa Ubunge Kigoma, anajiweza kweli kuchuana na Zitto Kabwe?

PreGE2025 Baba Levo ajitosa Ubunge Kigoma, anajiweza kweli kuchuana na Zitto Kabwe?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Aloooo, kweli uchawa unaenda kuharibu nchi, na kimasihara anaweza 'kumshinda' Zitto🤣🤣 kama jinsi wagombea 'walivyoshinda' viti 2020! Wana Kigoma tutawashangaa sana kura zikienda kwa chawa, itabudi tuingie kwenye rekodi ya Guiness ya kuwa wapumbavu wa Dunia!

===

Msanii na Mtangazaji maarufu Baba Levo amethibitisha kuwa wiki ijayo atakuwa mkoani Kigoma kwa ajili ya kutangaza nia ya kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2025 kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika nafasi zilizo wazi aidha Jimbo la Kigoma Mjini au Kata ya Mwanga.

Baba Levo amesema kuwa lengo lake kuu la kushiriki uchaguzi huo ni kuwaonyesha viongozi waliowahi kupewa nafasi lakini wakashindwa kuitumia ipasavyo, hususan katika kuwawezesha kujikwamua vijana kiuchumi.

 
Alipokua diwani aliwawezeshaje vijana wa kata yake? Kaogopa kurudi kwa tiketi ya ACT kaona wapinzani wanakula kichapo bora ajiunge na ccm tu. Kakumbuka alivoenda jela akiwa ACT kasema mmmh.
 
Bila Reforms za Tume ya Uchaguzi ni ujinga kushiriki Uchaguzi.
Ukiona chama ambacho si CCM kinakubali kushiriki basi ni chama DILI la CCM....chama famba hicho.
 
Back
Top Bottom