Mbunge wa Kigoma Mjini Clayton Chipando Maarufu Baba Levo ametimiza ahadi yake ya kuwakabidhi pikipiki vijana wawili waliojitolea kumsaidia kwenye kampeni kwa kujipaka rangi kama ishara ya sapoti. Ahadi hiyo imetekelezwa rasmi jana wakati wa Mkutano wake wa Shukrani, ambapo vijana hao walipokea pikipiki mpya mbele ya umati wa wananchi.