Baba Levo: Huwezi kuwa tajiri kwa kazi ya Ualimu

Baba Levo: Huwezi kuwa tajiri kwa kazi ya Ualimu

Halafu nani amemwambia huyo mtangazaji kuwa walimu Wana ndoto za kuwa matajiri?

Ndoto ya mwalimu ni kuona mwanafunzi anakuwa Rais, engineer, mfanyabiashara, mkulima Bora nk nk
 
Huyu jamaa haishiwi na kuropoka.
Hivi haoni kama hiyo statement yake ina athari kwa jamii kulingana na mapokeo tofauti!?
Pia naona utajiri kau define vibaya.
Wapo walimu matajiri,akamuulizie Saliboko aliyeanza kuwa mwalimu mkuu wa Yemeni schools akaja kuishia kujenga shule yake Daarul Arqam,ameshafariki Mungu amrehemu.
 
Vyama vya walimu walitakiwa kutoa karipio kwa udhalilishaji walio fanyiwa walimu wetu hata kama siyo matajiri hayo ni mambo yao binafsi kwani nchii hii walimu wetu pekee ndiyo masikini? WCB wanapaswa kuwaomba radhi walimu wetu. Huyo anijiita sijuwi baba levo akili zake hazipo sawa ni mwanaume mropokaji. Kama ni muandishi wa habari kweli kuna mambo mengi sana kwenye jamii ya kufatilia na kuzungumzia. Angekuwa na akili azungumzie Tatizo la rushwa kwenye jamii na siyo maisha binafsi ya watu.Watoto wangu wanasoma shule za kata walimu wakigoma ntawapeleka wapi aache ujinga.
 
Tajiri ni nini? Uwe tajiri unatakiwa iweje ? Ukiwa ajira unaweza kuwa tajiri ? Tuanzie hapo......
 
Vyama vya walimu walitakiwa kutoa karipio kwa udhalilishaji walio fanyiwa walimu wetu hata kama siyo matajiri hayo ni mambo yao binafsi kwani nchii hii walimu wetu pekee ndiyo masikini? WCB wanapaswa kuwaomba radhi walimu wetu. Huyo anijiita sijuwi baba levo akili zake hazipo sawa ni mwanaume mropokaji. Kama ni muandishi wa habari kweli kuna mambo mengi sana kwenye jamii ya kufatilia na kuzungumzia. Angekuwa na akili azungumzie Tatizo la rushwa kwenye jamii na siyo maisha binafsi ya watu.Watoto wangu wanasoma shule za kata walimu wakigoma ntawapeleka wapi aache ujinga.
TAtizo mnasoma habari kwa juu juu itafute interview nzima ndoutaelewa alichokuwa anamaanisha simtetei lakini kwa fact alizotoa yuko sahihi zama youtube itafute utaelewa
 
Mtangazaji wa kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi Fm, Baba Levo amenukuliwa akisema huwezi kuwa tajiri kwa kazi ya ualimu kwasababu kazi hiyo ni ya kipato cha chini sana kwenye mishahara na posho zao ni ndogo.

Kujenga hata nyumba ya kisasa kwa kazi ya ualimu ni changamoto sana sahau kuhusu utajiri, aliongeza Baba Levo.

Una maoni gani?View attachment 3004709
Sasa kwa nini siku zote alikuwa hasemi kama yeye ndiye Mpwayungu?
 
Back
Top Bottom